Help Children
Love them
Saidia Watoto

Friday, March 16, 2012

Wateja wa Tigo Rusha waichangia Hassan Majaar Trust Milioni 26.



Zaidi ya watu wapatao mia moja walishiriki katika matembezi ya kujitolea katika ufunguzi wa kampeni ya Tigo Tuchange kwa ajili ya kukusanya hela ya kuchangia sekta ya elimu nchini Tanzania. 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi, Mh. Shukuru Kawambwa alizindua matembezi hayo Machi 3, 2012, kwa kukata utepe na kuwaongoza watembeaji kutoka Shekilango Millenium Bussiness Complex hadi Ubungo mataa. Nchini kote, maelfu ya watu walijitokeza na kuongeza muda wa maongezi kupitia Tigo Rusha ili kuchangia kampeni hii.

“ Ningependa kuwashukuru wote walioshiriki kuchangia kampeni ya mwaka huu” alisema Bw. Diego Gutierrez, ambaye ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kampuni ya Tigo. “ Tunafuraha kufahamu kuwa matokeo ya juhudi zetu za pamoja zitaleta mabadiliko kwamamia ya watoto wa shule nchini” alisema.

Shiling milioni 26  zimekusanywa kupitia muda wa maongezo ulionunuliwa kupitia Tigo Rusha Kati ya saa tano na saa sita mchana wa siku hiyo. 

Wateja walionunua muda wa maongezi kati ya muda huo, waliweza kutumia muda wao wa maongezi  kama kawaida wakati Tigo ilirudufu kiasi hicho na kuingiza katika kampeni hiyo ya uboreshaji wa Elimu.

 Fedha zote zilizopatikana katika tukio hilo zitapelekwa kwa Hassan Majaar Trust (HTM), programu endelevu yenye lengo la kuboresha mazingira ya upatikanaji wa elimu   kwa kutoa madawati kwa shule mbalimbali zenye uhitaji.

Mwenyekiti wa HTM, Balozi Mwanaidi Maajar, alisema “Tumefarijika sana na kampeni hii na tungependa kuwashukuru Tigo kwa mchango huu utakaosaidia mahitaji ya elimu kwa watoto wa Tanzania. 

Msaada huu tulioupata leo utatumika katika kununulia madawati kwa shule mbalimbali ambazo tunazo na tumethibitisha kuwa na uhitaji. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati. Tunaona kwamba hii ni hatua kubwa katika kufikia malengo yetu”.

0 comments:

Post a Comment