Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, July 30, 2012

Usaili wa EBSS mikoani wamalizika elimu ya kutosha yatolewa kwa washiriki

 Umati wa vijana ambao walihudhuria usaili wa EBSS mkoani Tanga ambao pia walipata fursa ya kufundishwa muziki na majaji wa EBSS
                                  Jaji Salama akitoa somo lake kwa baadhi ya washiriki wa siku hiyio
Madam Ritha hakusita kutoa somo kwa mshiriki huyu aliyekuwa nje ya ukumbi wa La Casa Chika ambapo mlemavu huyu alielekezwa naman ya kuendeleza kazi zake za sanaa, kijana huyu alishiriki BSS mwaka juzi





Saturday, July 28, 2012

Ukiwa una picha za Chuo, Shule za sekondari, msingi na chekechea tutumie tuweke humu bure

                                Sehemu ya mbele ya kuingilia geti la Chuo Kikuu cha Mzumbe Tawi la Mbeya
                                               Madhari ni nzuri na ya kuvutia sana
                                                 Baadhi ya majengo wanayoishi wafanyakazi
                                             Jengo la utawala wa chuo hicho cha Mzumbe
                                                   Mabweni ya wanafunzi
                                         Sehemu ya madarasa ya wanafunzi wa chuo hicho

Thursday, July 26, 2012

Walimu tumieni hekima katika kuamua kugoma au la


WALIMU nchini kupitia chama chao wanatarajia kupiga kura ya kuamua kugoma au kuendelea na kazi kufuatia kushindwa kwa kufikiwa kwa mwafaka kati yao na serikali.

Uamuzi huo umekuja baada ya tume ya usuluhishi iliyokuwa ikisikiliza madai ya walimu hao kushindwa kuwasuluhisha walimu na serikali ambao kwa pamoja walikuwa katika mjadala wa kuhusiana na suala la ongezeko la mshahara.

Upigaji huo wa kura utaanzia tarehe 25 mwezi huu mpaka 27 ambapo idadi ya kura zao ndio zitaamua kuendelea kwa mgomo au la.

Mtandano huu wa elimuboratanzani unasisitiza suala la hekima kutumika zaidi katika kuamua nini kifanyike

Monday, July 23, 2012

Mlale mahala pema wanafunzi mliopoteza maisha katika ajali ya MV SKAGIT

HIVI karibuni ilitokea ajali ya meli iliyokuwa  ikitokea bandari ya Dar es salaam kuelekea kisiwani Zanzibar ambapo watu wengi walipoteza maisha yao wakiwamo watoto wadogo.

Mtandao huu wa elimu (elimuboratanzania.blogspot.com) unachukua fursa hii kuungana na watanzania kwa ujumla kuomboleza ajali hiyo.

Ni dhahiri kuwa katika ajali hiyo kuna wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na hata vyuo ambao walipoteza maisha hivyo kuacha pengo katika sekta ya elimu.

Pia ajali hii imekatiza ndoto za wanafunzi hao waliopoteza maisha ambazo pengine zingeweza kuleta tija kwa maendeleo ya taifa hili.

Ni vyema vyombo husika vikasisitizia suala la ueledi pamoja na kiufuatilia maadili na taratibu za usafiri wa nyombo vya majini ili kuondoa uwezekano wa kujirudia kwa suala hili.

Suala la elimu lilivyogusiwa leo bungeni


Serikali imeongeza kiwango cha alama za kuwachagua wanafunzi wanaotakiwa kwenda kujiunga na elimu ya vyuo vya ualimu.

Awali ilikuwa ni mhitumu wa kidato cha nne mwenye alama division 4.28 alikuwa anaweza kujiunga na elimu ya ualimu lakini kwa sasa ni wale wenye division 4.27 tu.

Hatua hii ni nzuri kwa kuwa inawapatia nafasi wanaojiunga na ualimu kuwa katika mazingira mazuri ya kuwafundisha wanafunzi kwa kuwa nao wanakuwa ni wenye uelewa zaidi.

Hayo yalisemwa leo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa wakati akijibu maswali bungeni.

Tutaendelea kuwajulisha yanayojili bungeni Dodoma katika sekta hii ya elimu ambayo ni muhimu kabisa hapa nchini.

Tuiunge mkono Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)


Tangazo hili litakuwa rasmi kesho katika kurasa wa matangazo wa blog hii ya Elimuboratanzania

Sunday, July 22, 2012

Majaji wa EBSS waomboleza msiba wa meli Zanzibar, pia waendeleza somo la muziki

 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Zantel Awaichi Mawalla kulia akiwa pamoja na majaji wa EBSS 2012 wakiwa wamesimama kuomboleza msiba wa meli wa Zanzibar
 Washiriki nao wakiwa wamesimama kuomboleza msiba huo
Baadae waliendeleza zoezi la kufuatilia vipaji ambapo pia walitoa elimu kwa washiriki waliojitokeza katika usaili mkoani hapo.

Na Mwandishi wa elimuboratanzania, Mbeya
WASICHANA wawili pamoja na wavulana watatu wamechaguliwa kuuwakilisha mkoa wa Mbeya katika fainali za taifa za shindano la kusaka vipaji la Epiq Bongo Star Search (EBSS 2012)

Washindi hao ambao kwa sasa majina yao wala picha zao havitakiwi kutangazwa kwenye vyombo vya habari walionesha uwezo mkubwa katika kuimba nyimbo mbalimbali.

Akizungumzia vipaji vya Mbeya jaji mkuu wa EBSS 2012 Ritha Paulsen alisema kuwa washindi hao wametoka katika kundi la vijana zaidi ya 500 waliojitokeza mkoani hapa.

Alisema kuwa mbali na mkoa wa Mbeya kusifika kwa kuimba nyimbo za injili lakini wameweza pia kuonesha uwezo katika nyimbo nyingine mbalimbali za kidunia.

Alisema kuwa wamefanikiwa kuwafundisha muziki vijana wengi ikiwa pamoja na kuwaelimisha juu ya namna ya kutoka zaidi sit u kimuziki bali pia hata katika masuala mengine ya sanaa.

“ Mbali na washiriki kuja kwa nia ya kuimba lakini pia wapo ambao wamegundulika kuwa na uwezo wa kuigiza na kufanya aina nyingine za sanaa ambazo tumewaelekeza kuzifanya” alisema Ritha.

Alisema kuwa tofauti na mikoa mingine katika mkoa wa Mbeya ameshuhudia akinamama wenye vipaji wakishiriki kuimba kitu ambacho alisema kuwa ni tofauti na mikoa mingine walioenda.


Friday, July 20, 2012

Kipindi cha kufundisha vijana maisha kimerudi tena







Na Mwandishi wa Elimuboratanzania 
SHINDANO la Maisha Plus ambalo huendeshwa kwa kuonyeshwa katika televisheni kila siku, limerudi baada ya kutofanyika kwa mwaka mmoja.


Kipindi hicho chenye kuelimisha, kuburudisha na kuhamasisha masuala mbalimbali ya maisha kipo tena hewani baada ya kukosekana kwa muda wa mwaka mmoja.\
 
Mratibu wa kipindi shindano hilo, Masoud Ali (Kipanya) amesema shindano hilo litaanza kurushwa tena mara baada ya kukamilika kwa usaili wa washiriki unaotarajia kuanzia mkoani Arusha.

Masoud amesema shindano hilo ambalo liliwahi kufanyika mara mbili, safari hii linakuja na nguvu mpya na burudani ya aina yake.

"Maisha Plus hatukuifanya mwaka jana, kuna marekebisho makubwa tumeyafanya ambayo yatalifanya hili liwe bora kuliko yaliyopita,"anasema Masoud maarufu kwa jina la Kipanya.

Ameongeza kuwa shindano hilo mwaka huu litaambatana na shindano dada la Mama Shujaa wa Chakula ambalo pia liliwahi kufanyika mwaka jana.

Katika muungano huo amesema Washiriki wa Mama Shujaa wa Chakula wataingia katika kijiji cha Maisha Plus wiki mbili kabla ya kuanza rasmi kwa shindano hilo.

"Safari hii shindano tunaliunganisha na hili la Mashujaa wa Chakula linaloandaliwa na Oxfam ambao pia ni wafadhili wetu mwaka huu," anasema Kipanya.

Safari hii shindano hilo litawakusanya vijana kutoka mikoa 14 ya Tanzania Bara na Visiwani, baadhi ya mikoa itakayoshiriki ni pamoja na Morogoro, Dodoma, Tanga, Arusha, Moshi, Mbeya, Mtwara, Dar es Salaam, Zanzibar n.k

Tuesday, July 17, 2012

Hassan Maajar Trust (HMT) yakabidhiwa milioni 23 na Tigo kununulia madawati 745

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa (kushoto), akikadidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. mil 26, Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee wa Taasisi ya Hasaam Maajar Trust (HMT), Dk Sinare Yusufu, kwa ajili ya kununa madawati 745 yatakayogawiwa katika shule za msingi zilizopo wilaya ya Njombe na Makete. Anayeshuhudia katikati ni Kaimu Meneja Mkuu wa Tigo, Andrew Hogdson ambayo imetoa Fedha hizo zilizotokana na michange ya matembezi ya hiari ya ‘Tigo Tuchange.’

 Na Mwandishi wa Elimubora

Tigo imekabidhi  fedha zilizopatikana katika mfuko wa matembezi ya hiari ya Tigo Tuchange kwa Hassan Maajar Trust ( HMT),  ni mpango wa muda mrefu uliyoundwa ili kuboresha mazingira ya kusoma mashuleni kwa kugawa madawati katika shule mbalimbali za wahitaji.

Sherehe za makabidhiano zilihudhuriwa na Mheshimiwa Dr. Shukuru Kawambwa , waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi, wanachama wa HMT , mwandamizi mtendaji wa Tigo na wafanyakazi.

“Moja ya lengo letu ni kuhakikisha wanafunzi wana vifaa vya kujifunzia na mazingira tulivu ya kusomea”alisema Mh. Dk  Kawambwa. Tunawapongeza Tigo kwa kutoa ushirikiano mzuri kwa raia na tunaomba makampuni mengine kuisaidia serikali katika kuleta maendeleo endelevu  katika nchi” hii alisema.

Hundi ya Sh. 26, 000,000 iliwasilishwa  kwa niaba ya Tigo na Andrew Hudgson,Kaimu meneja Mkuu , kwenda kwa Mkurugenzi mtendaji wa HMT, Zena M Tenga. Fedha zilipatikana kwa njia ya  ukusanyaji wa Tigo rusha top ups iliyofanywa mida ya saa 5 asubuhi na 12 jioni siku ya tarehe 3 March.Wateja ambao waliweka muda wa mawasiliano kwa muda huo walitumia muda wao wa mawasiliano wakati kuenda kiasi kama hicho kwa mpango huo

Mpango huu ni kulingana na dhamira yetu  ya kushirikiana na jamii  katika kuelewa mahitaji ya jamii zinazotuzunguka maeneo tunayofanyia biashara, ili kutengeneza mchango mzuri na endelevu katika kuwainua” alisema Bw.Hudson “ Tungependa kuwashukuru tena wote kwa mchango wenu katika mfuko huu muhimu’ alisema

Chini ya mradi wa shule 5 (tano) kutoka wilaya mbili (Njombe & Makete) zilizoko wa  mkoa wa Iringa zitapokea madawati kama ifuatavyo: Maendeleo: 135, Umoja: 196,Kumbila: 200, Makonde: 152 na  Mbela: 37.

Shule zilichaguliwa kulingana na kuwepo kwa haja kubwa zaidi. Mradi hautafaidhisha tu shule na wanafunzi, bali kwa kununua madawati ndani ya nchi kutasaidia katika kutengeneza nafasi za ajira kwa wafanyabiashara na vijana katika maeneo hayo na hivyo kuleta maendeleo ya kiuchumi katika sehemu hizo.

“Ningependa kutoa shukrani  za dhati kwa niaba ya HMT kwenda kwa Tigo katika kushiriki kwao kuwapatia watoto hawa  fursa itakayowafanya  ya kuweza kujitegemea na kwa upande wa kuwawezesha na kuwaruhusu wale kuhitaji misaada yao katika siku zijazo,” Bi. Tenga. “ Mwanafunzi anaposoma katika mazingira mazuri na tulivu wanakuwa na umakini zaidi na kuzalisha matokeo mazuri zaidi na hyivyo kupata maisha bora baadaye, na kwa  kupitia miradi endelevu ya namna hii tunaweza kuleta jitihada kubwa katika kuleta maendeleo ya uchumi  ndani ya jamii, “ alisema.


Monday, July 16, 2012

Pazia la uchangiaji wa ujenzi wa hosteli za wasichana lilipofunguliwa rasmi huko KIbaigwa Dodoma

 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Watoto Ummy Mwalimu akicheza ‘kwaito” na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kibaigwa katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa mabweni 30 nchi nzima kwa mtoto wa kike
 
Waziri kivuli wa Elimu na mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Susan Lyimo akiongea katika hafla ya uchangiaji wa mabweni. Katika hafla hiyo jumla ya shilingi 37,214,000/= zilipatikana ikiwa ni ahadi pamoja na fedha taslim.
 
Mgeni Rasmi, Waziri kivuli wa Elimu na mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Susan Lyimo akipokea mkasi kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya TEA Dkt Naomi Katunzi kwa ajili ya kuzindua rasmi harambee ya ujenzi wa mabweni 30 kwa ajili ya watoto wa kike wa sekondari nchini.
 Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Kibaigwa Job Ndugai Akivuta utepe uliokatwa na mgeni rasmi Mh. Suzan Lyimo huku tukio hilo likishangiliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na TEA

Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Sylvia Lupembe Gunze (kushoto) akijadiliana mambo mawili matatu na diwani wa Kibaigwa Richard Kapinye na Afisa Elimu Taaluma wa Kongwa bi Emilia Litunguru.

Sunday, July 15, 2012

Majaji EBSS waendeleza elimu ya muziki kwa washiriki wa EBSS

 Jaji Master Jay akitoa elimu kwa mmoja kati ya washiriki waliojitokeza katika usaili wa Mwanza
Mshiriki akiwa anasikilizia elimu hiyo mara baada ya kumaliza kuimba na kuambiwa kuwa alichemka.



Na Mdau wa elimuboratanzania, Mwanza.
VIJANA wa mkoa wa Mwanza wameelezea kufurahishwa kwao na elimu ya bure iliyotolewa na majaji wa EBSS mkoani Mwanza ambapo waliahidi kufanyia kazi elimu hiyo.

Elimu hiyo ni kuhusiana na namna ambavyo wanaweza kujifunza kupandisha sauti zao, kupanga vina na kuimba aina zote za sauti.

Wakati huohuo katika hali isiyokuwa ya kawaida wakazi  wa  mkoa wa Mwanza juzi walijitokeza kwa wingi katika usaili wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) mkoani hapa hali iliyosababisha wengi wao kukosa  nafasi ya kuimba na kulazimika kurudi tena jana.

Katika usaili huo uliofanyikia katika uwanja wa CCM Kirumba ulihudhuriwa kwa mamia ya wasichana na wavulana huku wengine wakiwa wamebeba  vifaa mbalimbali vya muziki kuashiria kuwa wanaifahamu vema fani hiyo.

Zoezi la kuimba lilianza majira ya saa mbii asubuhi ambapo majaji walianza kusikiliza vipaji hivyo na ilipofika majira ya saa kumi na moja jioni bado kulikuwa na watu wengi waliokuwa bado wanahitaji nafasi ya kuendelea kuimba.

Kutokana na muda kuwa umeenda walilazimika kuambiwa kurudia tena jana huku wengi baadhi yao walikuwa wamefanya siku ya kwanza vema waliitwa tena kuimba kwa mara ya pili ili kuchaguliwa.

Mmoja kati ya wafanyakazi wa kampuni ya Benchmark  Production inayoandaa shindano hilo alisikika akisema kuwa hali hiyo haijawahi kutokea kwa mkoa wa Mwanza kwa kuwa watu wamekuwa wakijitokeza kila mwaka lakini sio kwa idadi hiyo.

Mkoa wa Mwanza ambao mwaka juzi ulitoa mshindi wa shindano hilo Paschal Casian umekuwa na hamasa kubwa ya wakazi wake kujitokeza kwa wingi kushiriki katika shindano hili kubwa na la aina yake linalodhamiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel.

Thursday, July 12, 2012

TEA kuchangisha bilioni 2.3 kusaidia ujenzi wa hosteli za wasichana

 Meneja wa mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Slyivia Lupembe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
 Waandishi wa habari wakichukua habari ya kuhusiana na uchangiaji huo wa hosteli za wanafunzi wasichana


Kaimu Mkuu wa TEA Esther Bayo akisisitizia jambo kuhusiana na uchangiaji huo
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) kesho itazindua rasmi kampeni ya kuchangua ujenzi wa hosteli za wanafunzi wasichana kwa shule nane za sekondari nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA Esther Bayo alisema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika wilaya ya Kibaigwa ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Philip Mulugo.
Alisema kuwa kampeni hiyo inalenga kujenga hosteli 30 ambapo kiasi cha fedha kilicholenga ni shilingi bilioni 2.3 huku kila bweni likiwa li nagharimu milioni 78 bila samani.
Alisema kuwa ujenzi huo ukikamilika utawanufaisha wanafunzi wa kike 1,504 na kuwaepusha dhidi ya hatari mbalimbali zinazowakabili kwa sasa.
Alisema kuwa shule ambazo zitanufaika na mradi huu ni pamoja na sekondari za Ufana iliyopo Manyara, Mibukwe iliyopo Tanga, Kibaigwa iliyopo Dodoma, Milola iliyopo Lindi, Nyihara iliyopo Mara, Lundo iliyopo Ruvuma, Butundwe Mwanza na Buseko Hill iliyopo mkoani Kigoma.
Akizungumzia mikakati ya muda mrefu ya serikali katika kufanikisha ujenzi wa hosteli hizo alisema kuwa serikali inakusudia kujenga hosteli 100 katika maeneo mbalimbali nchini.
Alisema kuwa katika mpango huo mpya wa ujenzi wa hosteli hizo 100 wanafunzi 4800 watanufaika nazo na zinatarajiwa kukamilika mwaka 2015.
“ Hivyo tunaomba kuwa kila mwenye nia ya kusaidia katika hio ajitaidi kufanya hivyo kwa kuwa ndio tutawasaidia hawa wanafunzi wetu wa kike ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali” alisema Esther.
Mwisho

Thursday, July 5, 2012

Tangaza nasi kwa bei poa

Kama inavyofahamika kuwa kwa sasa habari kwa njia ya mtandao ndio zinawafikia watu wengi kwa haraka zaidi, hivyo kwa kulitambua hilo blog hii imeamua kuanzisha njia hii kwa wadau kutangaza nasi kwa bei poa zaidi.

Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0714 43 65 94

Ukifika Sabasaba usikose kutembelea banda la Global Education Link LTD upate ushauri wa elimu nje ya nchi

                                                   Kwa  nje banda hilo linaonekana kama hivi
Hapa ni ndani ya banda hilo ambapo utakutana na maofisa watakaokupatia ushauri mzuri wa masuala ya elimu nje ya nchi wanashughulikia elimu kwa nchi za India, Malasyia, Ukraine na Uingereza.

Kesho ntaingia hapo na kutoa taarifa zaidi

Sunday, July 1, 2012

EBSS mbali na kutafuta vipaji pia inatoa somo kwa washiriki

Jaji Mkuu wa EBSS 2012 Ritha Paulsen akitoa elimu ya muziki kwa mshiriki huyu ambae hakuchaguliwa kupita 
                                     Master J akimpa somo mshirii aliyechemsha kuimba
Mwanadada ahuyu alikuwa mmoja kati ya waliojitokeza kushiriki katika kinyang’anyiro cha kuwatafuta wakali wa Lindi