Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, March 29, 2015

Black Fox yaja tena kuelimisha vijana kuhusiana na Mitindo


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Black Fox Model, Aj Mynah akizungumza na vijana waliojitokeza kujifunza fani ya uanamitindo katika klabu ya Paparazi iliyopo Sleep way Masaki.

Somo likiendelea na Aj kwa sasa anawafundisha kuhusiana na fursa zilizopo kwenye fani hiyo kuanzia maslahi na mengineo

Wanafunzo wa uanamitindo wakiwa wamepozi wakionesha njonjo zao baada ya kunolewa na AJ


Wanafunzo wa uanamitindo wakiwa wamepozi wakionesha njonjo zao baada ya kunolewa na AJ

I really like her initiatives, she so amazing


AJ akiwa amepozi na wanamitindo hao wanafunzi katika klabu hiyo ambapo hukutana kila Jumapili kuanzia saa tatu asubuhi kujifunza mambo yote yahusuyo uanamitindo










Na Mwandishi Wetu
MWANAMITINDO AJ Mynah ameanzisha mpango wa kutoa mafunzo ya bure kwa vijana mbalimbali wenye vigezo vya kuwa wanamitindo katika klabu ya Paparazi iliyopo Sleep Way Masaki. 

Aj anatoa mafunzo hayo kupitia kampuni yake ya Black Fox  Model ambapo akizungumzia kuhusiana na sababu zilizopelekea kuanzisha mafunzo hayo alisema kuwa kampuni yake hiyo imeamua kutoa mafunzo hayo bure kwa vijana baada ya kutoridhishwa na maendeleo ya fani hiyo hapa nchini.

Mwanadada huyo ambae aliwakuwa mwanamitindo wa Tanzania nje ya nchini akifanya kazi zaidi nchi za Ulaya alisema kuwa wapo vijana wengi wana sifa nzuri za kuwa wanamitindo lakini wanashindwa kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha wa fani hiyo na pia hawajahamasishwa.

Aliongeza kuwa anaona kuwa vijana wa kitanzania wakijihusisha na fani hiyo wanaweza kufika mbali pia hata kufikia hatua ya kuiwakilisha Tanzania kimataifa zaidi.

Alisema kuwa "Unaweza kuwaona wadada au wakaka ambao wanavutia kuwa wanamitindo na ukiwauliza kama wamewahi kufikiria kujihusisha na fani hiyo utakuta labda hata wazo hawana na wengine hawaoni fursa za zitokanazo na fani hiyo"

Aliongeza kuwa " Kwa sasa nimeamua kuanzisha kampuni hii kwa lengo la kuhakikisha kuwa vijana wanaandaliwa vema na kuja kuwa wanamitindo wakubwa ambao wanaweza kutangaza bidhaa mbalimbali za ndani na nje ya nchi na kila Jumapili tunakuwapo hapa klabu ya Paparazi, Sleep Way Masaki na ni bure kabisa kwa vijana kuja kujifunza".

Aliongeza kwa sasa kampuni hiyo ina wanamitindo 40 wakiwamo wa ndani na nje ya Mkoa wa Dar es salaam.

Akizungumzia kuhusiana na fursa zilizopo kwenye fani hiyo alisema kuwa yapo makampuni mengi ambayo yanaweza kuwalipa vijana mamilioni ya fedha ili kutangaza bidhaa zao na vijana wanamitindo ndio pekee wenye kuweza kufanya kazi hiyo.
====================