Help Children
Love them
Saidia Watoto

Thursday, November 28, 2013

Nkenge Foundation kusaidia upatikanaji wa madawati

Waandishi wakifuatilia mkutano huo


Mbunge wa Nkenge Assumpter Mshama akiwa na msaidizi wake marabaada ya kuzungumza na waandishi wa habari jana


Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Asa Mwambene akiangalia harakati za Nkenge Foundation.

Habari Kamili
Mbunge wa jimbo la Nkenge mkoani Kagera, Assumpter Mshama kupitia Taasisi yake ya Nkenge,  leo anaendesha hafla ya chakula cha usiku kuchangia upatikanaji wa madawati ya wanafunzi wa mkoa huo pamoja na masuala mengi ye kimaendeleo.

Katika  hafla hiyo mgeni rasmi ni Makamu wa Rais Garib Billal 


Thursday, November 21, 2013

Kifaa cha kuzima moto bora zaidi mashuleni










KAMPUNI ya Simba Logistic Equipment Supply jana ilizindua kifaa cha kuzimia moto kwa kurusha kiitwacho Bonex ambacho vinatumia kuzimia moto katika majumba, magari na sehemu nyinginezo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa vifaa hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simba Logistic Equipment Supply Co Limited, Fareed Nahdi alisema kuwa vifaa hivyo ni rahisi kutumika katika matukio mbalimbai ya kuzimia moto.

Alisema kuwa havihitaji matengezo ya mara kwa mara kwa kuwa vikinunuliwa vinatumika kwa mara moja kwa tukio moja.

Alisema kuwa ni vifaa ambavyo ni rahisi kubebeka na kutumika katika mazingira yoyote kutokana na udogo wake ambao unaumuhimu mkubwa katika kuzima moto.

"Hii ni aina mpya ya uzimaji  moto kwa kutumia vifaa hivi muhimu ambapo ukitofautisha na vifaa vingine ambapo kunakuwa kuna maelekezo mengi ya kufuata lakini hiki unarusha tu hivyo hata watoto wanaweza kutumia"alisema Nahdi.

Alisema kuwa hakina madhara kama vile moshi wala aina nyingineyo ya madhara na kinasaidia harakati za uokozi wa watu.

Naye Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga aliyekuwepo kushuhudia uzinduzi huo alisema kuwa kifaa hicho kinaweza kusaidia zaidi hata katika kuzima motoo wa magari.
Alisema kuwa wenye magari wanapaswa kwua na kifa hicho kwa kuwa ni rahisi kutumika pia.
Mwisho

Monday, November 18, 2013

Jery Silaa achangisha milioni 16 za madawati














Habari Kamili
The First of its kind mayoral ball aims to raise TZS 4.98 Billion towards providing desk to 30,487 primary and secondary schools in Ilala Municipality by end of financial year 2013/14. 100% of all funds shall proceeds towards realization of this project.
To assist towards the Fund raising for the Desks, The Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel has led the path by Hosting A charity art Auction Brunch, where by proceeds from this event will go towards procuring the desks

Ten Local Tanzania Artiste were hosted by Hyatt Regency for 5 days where the artiste created their works of Art at the hotel premises. Some of the art created was later auctioned off to the guests attending the Brunch on 16 November hosted By Hyatt Regency Kilimanjaro hotel.

The guest of honour for the brunch was Mama Asha Bilal, wife of the Vice President, who together with her husband donated TZS 2 Million towards Mayor Jerry Silaa Cause of Dawati Ni Elimu

Robert Ntilo, one of Tanzania’s leading artists, who spoke on behalf of all artists stated, “This is a very great initiative by Mayor Silaa and we are very proud to have been invited to participate towards this goal and using our creative Talent, we can make a difference”

The artistes who participated in this event are
  • ROBINO NTILA
  • AGGREY MWASHA
  • SALUM KAMBI
  • CUTHBERT SEMGOJA
  • JAMES HAULE
  • HAJI CHILONGA
  • THOBIAS MINZI
  • MOSES LUHANGA
  • PONI YENGI MISS
  • VITA MALULU

A total of 16.2 million gross was raised at the Brunch

This event is sponsored by Hyatt regency Kilimanjaro and 361 degrees.

WHAT IS MAYORS BALL?
 A Charity fundraising cum advocacy event aimed at not only fundraising but advocating the need for a right of Tanzanians to various basic human needs. This Annual event shall be the Mayor of Ilala signature event where by it shall bring all leaders from various sectors in Tanzania under one roof for one purpose, serving the society
Honoring the intentions of its founders, the Ilala Mayor’s Charity Ball., a non-profit organisation, is committed to raising money to directly benefit residents of Ilala Municipality. Proceeds from the annual Mayor’s Charity Ball will be awarded to charities chosen annually.

ABOUT DAWATI Ni ELIMU.
DAWATI Ni ELIMU is a project towards the Mayors ball that aims to solve the issue of shortage of desks in primary and secondary schools in Ilala municipality where by currently there is a lack of 30,487 desks. The project is an initiative under the office of the mayor of Ilala Municipal Council, this project seeks to raise a sum of 4.98 Billion Tanzanian shillings with the emphasis that the society can contribute and make change to solve the challenges by calling upon organisation and individuals to contribute to this noble cause.

Sunday, November 17, 2013

Wanafunzi wa udaktari wasaidia upimaji wa kisukari Ilala

Mwanafunzi wa Udaktari katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya, Muhimbili Elizabeth Mkashabani akimpima urefu mkazi wa Dar es salaam aliejitokeza kupima afya yake

Mwanafunzi wa Chuo Cha IMTU, Yasir Kazi

Umati wa watu ukijiandaa kuingia kupima afya zao

Madaktari wakiwa kazini

Mama Asha Bilal achangisha fedha za kununulia Madawati Ilala

Akiwa na Meya wa Ilala wakiangalia picha ambazo ziliuzwa na fedha kutumika kuchangia upatikanaji wa madawati

Wakitafakari jambo

Mzungu huyu kainunua picha


Hawa wadau wa elimu nao walinunua picha


Ujunbe ulikuwa Dawati ni elimu



Minzi alionesha picha yake aliyomchora Bi Kidude

Basi baada ya kazi ya kuuza picha Mama Bilal akaondoka.   

Friday, November 15, 2013

Meya Jerry Slaa atembelea kambi ya wachoraji wa picha kuchangia elimu






Local Tanzanian artists painting to Support Dawati Ni Elimu
 The First of its kind mayoral ball aims to raise TZS 4.98 Billion towards providing desk to 30,487 primary and secondary schools in Ilala Municipality by end of financial year 2013/14. 100% of all funds shall proceeds towards realization of this project.
To assist towards the Fund raising for the Desks, The Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel has led the path by Hosting A charity art Auction Brunch, where by proceeds from this event will go towards procuring the desks

Ten Local Tanzania Artiste are being hosted by Hyatt Regency for 5 days where the artiste are creating their works of Art at the hotel premises. The art created will then later be auctioned off to the guests attending the Brunch on 16 November.
The Mayor Jerry silaa visited the artists as they were at the studio at the Hyatt regency Kilimanjaro towards the preparation of the brunch
Robert Ntilo, one of Tanzania’s leading artists, who spoke on behalf of all artists stated, “This is a very great initiative by Mayor Silaa and we are very proud to have been invited to participate towards this goal and using our creative Talent, we can make a difference”

The artistes participating in this event are
  • ROBINO NTILA
  • AGGREY MWASHA
  • SALUM KAMBI
  • CUTHBERT SEMGOJA
  • JAMES HAULE
  • HAJI CHILONGA
  • THOBIAS MINZI
  • MOSES LUHANGA
  • PONI YENGI MISS
  • VITA MALULU

This event is sponsored by Hyatt regency Kilimanjaro and 361 degrees.

 WHAT IS MAYORS BALL?
 A Charity fundraising cum advocacy event aimed at not only fundraising but advocating the need for a right of Tanzanians to various basic human needs. This Annual event shall be the Mayor of Ilala signature event where by it shall bring all leaders from various sectors in Tanzania under one roof for one purpose, serving the society
Honoring the intentions of its founders, the Ilala Mayor’s Charity Ball., a non-profit organisation, is committed to raising money to directly benefit residents of Ilala Municipality. Proceeds from the annual Mayor’s Charity Ball will be awarded to charities chosen annually.
 ABOUT DAWATI Ni ELIMU.
DAWATI Ni ELIMU is a project towards the Mayors ball that aims to solve the issue of shortage of desks in primary and secondary schools in Ilala municipality where by currently there is a lack of 30,487 desks. The project is an initiative under the office of the mayor of Ilala Municipal Council, this project seeks to raise a sum of 4.98 Billion Tanzanian shillings with the emphasis that the society can contribute and make change to solve the challenges by calling upon organisation and individuals to contribute to this noble cause.

Sunday, November 10, 2013

Mwalimu Mkuu matatani kwa ubadhilifu

Mwalimu Mkuu Shule ya Mirerani alalamikiwa kwa ubadhirifu 
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Mirerani, Wilaya ya Simanjiro mkoani
Manyara,  Magreth Galibona analalamikiwa kufuja fedha na kudaiwa kuendesha shule hiyo namna anavyotaka.

Anadaiwa kuchangisha wanafunzi wa darasa la saba fedha kwa ajili ya picha kwa miaka miwili mfululizo pasipo halali.

Hata hivyo mwalimu huyo, amejibu shutuma hizo akisema wazazi walikubali kupitia kikao halali cha mkutano wa wazazi na walezi kulipa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya maendeleo ya shule yao hivyo hakuna tatizo juu ya hayo.

“Mimi nafanya kazi yangu siangalii majungu ya walimu wanavyosema hivyo endapo kuna watu wanaendelea na majungu yao watajua wenyewe ila mimi naendelea kufanya kazi yangu wasubiri wanachotaka,” alisema Mwalimu Galibona.  

Baadhi ya waliozungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa, walidai wanafunzi zaidi ya 150 waliamriwa kulipa Sh  2,100 kila mmoja kwa mwaka jana ili wapige picha za kufanyia mtihani ili hali halmashauri ya wilaya hiyo ilishagharimia picha hizo.

Walidai Mwalimu Galibona aliwachangisha wanafunzi 1,300 Sh 1,000 kila mmoja kwa ajili ya kutengeneza sanduku la kuhifadhi mitihani wakati fedha za ruzuku zilitengwa kwa ajili ya kazi hizo.
Kwa mujibu wao, akisikia wakaguzi wanakuja kukagua shule hiyo mwalimu huyo huwa na mtindo wa kunakilisha wanafunzi wa darasa la tatu ubaoni kwa siku moja kwa tarehe tofauti na kuwaandikia majibu ubaoni ili waonekane wana akili.
“Pia anakumbatia madaraka kwani yeye ndiye mwalimu mkuu na mtunza vifaa, fedha na chakula na ukimpinga tu anaongea na wilaya unahamishwa,” alisema mmoja wa waliozungumza na gazeti hili na kutaja baadhi ya walimu waliodaiwa kuhamishwa.

Ofisa Elimu Msingi wilayani Simanjiro Silvanus Tairo alizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema atafuatilia malalamiko yote yaliyotolewa  yapatiwe ufumbuzi kwa manufaa ya kunyanyua elimu katika wilaya hiyo.
Tairo alisema ni mgeni kwenye wilaya hiyo ila atafuatilia suala la wazazi kuchangishwa fedha za mitihani kwani Serikali ilishalipa gharama za huduma za picha na sanduku la mitihani.

Tuesday, November 5, 2013

Form form four kazi kwenu

Na Mdau wa Elimu
 MTIHANI wa kidato cha nne ulianza juzi nchini na takribani majuma mawili wanafunzi watakuwa kwenye pilika za hapa na pale za kufanya mtihani huo na kuhakikisha wanafaulu vema huku Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ikiwa imetangaza viwango vipya vya ufaulu kuanzia mwaka huu.  Ingawa marekebisho hayo ya viwango vya ufaulu yamefanyika, lakini bado kilio cha muda mrefu cha wadau wa elimu nchini ni cha mitaala ya kufundishia kubaki pale pale na bado ufumbuzi haujapatikana.

Upangaji huo wa Viwango vya Alama katika mitihani ya kuhitimu kidato cha nne na cha sita pamoja na matumizi ya alama za tathmini endelevu ya mwanafunzi kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi huenda yakawa yamewapa faraja kubwa wanafunzi wetu, ambao hivi sasa wapo katika vyumba vya mtihani kutimiza wajibu wao. Faraja ambayo wanafunzi wameipata na hata katika pitapita zangu mtaani na katika mabasi ya jumuiya niliyopanda kwa siku hizi mbili ni kutokana na hayo marekebisho yaliyotangazwa na Wizara na hata wao wanasikika katika majadiliano yao kuwa sasa angalau ‘watapeta’ kutokana na marekebisho hayo

 Pia walichekelea sana kuambiwa hakutakuwa tena na daraja ‘O’ ambalo lilikuwa likiwaaibisha sana wahitimu hao na mwaka jana baadhi yao walipoteza maisha kutokana na kupata daraja hilo na badala yake sasa kutakuwa na daraja la tano.

Lakini wakati wakishangilia hilo la kuwapo daraja la tano, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alikana Serikali kufuta daraja la sifuri akisema kulitokea mkanganyiko hivyo madaraja ya ufaulu kubaki I, II, III, IV na O, Hakuna Division V.

 Lakini mimi nataka kusema kuwa kuwepo kwa daraja ziro au kutokuwepo hakutawasaidia wanafunzi wetu kwa lolote na badala yake wahakikishe wanafaulu vizuri na hilo daraja ambalo wanalichekelea lisipate mtu na wote waishie katika madaraja ya I-III au IV ikibidi.

Hata hivyo, hapo awali tulishuhudia alama za ufaulu za daraja la pili zikianzia 18-21 lakini sasa alama hizo zimeongezwa hadi 24, hii ni kuwa wale ambao walipata alama 22, 23 na 24 wakapata daraja la tatu sasa watapata la pili, hii ni kubebwa na katu hapa tunapunguza tu waliofeli lakini tusishangae kuona hata hizo wasizipate.
Pia alama 22-25 awali zilikuwa ni za daraja la tatu lakini sasa wanapanda hadi aliyekuwa akipata daraja la nne hapo awali kwa kupata 26-33 hivi sasa analetwa hadi daraja la tatu, mbeleko ya hali ya juu hii kutoka wizarani hakika wanafunzi wana haki ya kushangilia.

Wizara na wadau wake wa elimu wameona kuwa kuwapa watoto daraja la tano badala ya daraja sifuri kutapunguza machungu na huenda ikawa faraja kwao na kweli imekuwa maana wameshangilia na huenda mazombi wasichorwe mwaka huu, lakini alama 48-49 haikuwapo iliishia 35 tu. 

 Bila shaka wanafunzi mwaka huu hawatafanya vituko na vioja tulivyozoea kwa miaka ya hivi karibuni ya kuandika mistari ya mashairi, kuchora picha za Zombi hajavaa viatu na matusi na badala yake wataonesha ujuzi wao kwa kupata madaraja ambayo yamefanyiwa ukarabati isipokuwa wale wa daraja la kwanza tu. 

Nimwaka wa Matokeo Makubwa Sasa ambayo ndio kaulimbiu ya Serikali baada ya ile ya Kilimo Kwanza kuanza kushika kutu kwa kasi ya ajabu bila mafanikio.   Walimu nao hawana budi kuendelea kusisitiza na kusimamia vema mitihani ambayo sasa itakuwa myepesi kwa wanafunzi wao, laikini pia tujiepushe na udanganyifu na wizi wa mitihani hiyo kama tulivyozoea.

Wizi wa mitihani ya kidato cha nne nchini imekithiri na baadhi ya watu hawa wanaofaulu kwa kubebwa na mbeleko za hali ya juu wafikapo madarasa ya mbele hushika mkia darasani.  Mwito kwa wanafunzi wote ni kufanya bidii katika kile ambacho wamejifunza kwa takribani miaka minne waliyokuwa shuleni, wengine wakisoma kwa raha huku wakipata huduma zote muhimu za shule na wengine wakisoma kwa jasho.