Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, February 28, 2012

Kampuni ya kijerumani ya Merck yajitosa kupambana na kipindupindu kwa wanafunzi Pemba

 
Mwanafunzi wa shule ya Ngwachani iliyopo Zanzibar Selemani Sareh   akinywa dawa ya kichocho jana kuashiria uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa huo iliyozinduliwa na naibu waziri wa afya wa Zanzibar Sira Ubwa Mwamboga (mwenye kiremba) kushoto kwake ni Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya madawa ya kijerumani iitwayo Merck Dr. Karl Ludwig Kley
 Mwalimu akihamasisha


 wakipewa mapulizo
Naibu Waziri na wadau wa kutoka Ujerumani wakicheza muziki na kikundi cha ngoma za asili cha Pemba

Tuesday, February 21, 2012

THT ambao ni watendaji wakuu wa mradi wa Zinduka waanza kutoa elimu ya Maralia kanda ya Ziwa


Ziara hiyo imedhaminiwa na Africa Barrick Gold


 Wakitumia sanaa za maonesho kutoa ujumbe wa Malaria
Waelimishaji wakiwauliza maswali watoto hao


Na Evance Ng’ingo
KUNDI la Tanzania House of Talent (THT) limeanza ziara ya siku 60 kwa mikoa ya kanda ya Ziwa ambapo wanatumia sanaa ya maonesho kuelimisha kuhusu ugonjwa wa Malaria.

Ziara hiyo inahusisha mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera na  Shinyanga ambapo wasanii hao wanafika mpaka wilaya za vijijini kuelimisha wanafunzi na wanajamii juu ya ugonjwa huo.

Akizungumzia ziara hiyo meneja wa mradi wa Zinduka unaoratibu zoezi hilo, Sadaka Gandi alisema wasanii wanane wapo katika msafara huo.

Alisema kuwa wasanii hao watatumia snaaa ya maigizo, nyimbo pamoja na muziki wa asili katika kufikisha ujumbe.

Alisema kuwa kwa kutumia sanaa THT imeweza kuifikia idadi kubwa ya wanajamii na kufanikiwa kuwaelimisha juu ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria na namna ya kujikinga nao.

Alisema kuwa ziara hiyo inatarajiwa kumalizika machi 22 mwaka huu baada ya kuzungukia mikoa yote na kutoa elimu husika ya malaria.

“ Kupitia mradi huu wa utoaji wa elimu ya Malaria kwa njia ya sanaa wasanii wameweza kulifanikisha zoezi hili kwa hali ya juu kwa kuongeza hamasa ya wananchi katika kushiriki vita dhidi ya ugonjwa huu” alisema Sadaka.

Zaiara ya wasanii hao imeanzia na mkoani  Mara ambapo wametembelea shule mbalimbali za sekondari na kuanzisha klabu za wanafunzi zenye majukumu ya  kupambana na ugonjwa wa Malaria.


Wasanii wa THT waliopo katika ziara hiyo ni wale wanaojishughulisha na uchezaji wa aina mbalimbali za ngoma na kuimba.
Mwisho



Kajifunzeni lugha Alliance Francais


Monday, February 20, 2012

Mzingira bora ya kuchezea watoto ni muhimu kwa afya zao pia

 Kukosekana kwa viwanja vya michezo kunawafanya watoto kubuni hata magoli yao wenyewe kama yanavyoonekana haya magoli
Watot hawa wakisakata kabumbu huku wakiwa wamevalia yeboyebo zao

Mange wa U -turn blog aendeleza love kwa wanafunzi na watoto wa mitaani

 Ilikuwa ni katika kituo cha watoto  Mikocheni, mwanadada huyu anatumi ablog yake hiyo kuwasaidia watoto wenye mazingira magumu kwa kuwapatia misaada

Sehemu ya darasa hilo ambapo watoto hao husoma na kulelewa hapo

Kamati ya vazi la taifa yatoa somo kwa wadau wa vazi hilo


KAMATI inayoshughulikia vazi la taifa imeeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya mchakato wa kutafuta vazi hilo.

Akizungumza katika mkutano na wadau wa sanaa ya ubunifu Mwenyekiti wa kamati ya vazi la taifa Ndesamburo Merinyo alisema kuwa wadau wengi wamejitokeza kufanikisha upatikanaji wa vazi hilo.

Merinyo alisema kuwa wadau hao ni pamoja na wachoraji wa michoro ya mavazi  na pamoja wa wadau wengine.

Alisema kuwa kwa sasa wamepata michoro mingi kutoka kwa wachoraji mbalimbali ambao wamekuwa wakielezea namna amabcho kitambaa cha vazi la taifa kinatakiwa kuwa.

Alisema kuwa kabla ya kupatikana kwa vazi la taifa kwanza kunakuwa na kitambaa cha vazi hilo ambacho ndio kitatumika kupata vazi lenyewe.

 Alisema kuwa tayari kamati yake imeendesha midahalo mbalimbali ikiwashirikisha wadau wa ubunifu, mavazi na sanaa kiujumla na tayari imekusanya mawazo yao kuhusiana na vazi hilo.

“ Ni kwamba kwa sisi kama kamati tunaona kuwa zoezi hili litakuwa ni lenye mafanikio makubwa kwa kuwa mwamko kutoka kwa watanzania ni mkubwa na safari hii kazi takamilika kama ilivyopangwa” alisema Merinyo.

Kamati ya vazi la taifa iliundwa mapema mwaka huu na waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Emanuel Nchimbi kwa lengo la kutafuta vazi la taifa litakalotambulisha taifa la Tanzania.

Katika mdahalo huo wa basata wadau mbalimbali walitoa mawazo yao kuhusiana na wanavyotaka kitambaa hicho kuwa
Mwisho

Eti Ndalichako atakiwa kujiuzulu

(Tuma mawazo yako baada ya kusoma)

BAADHI ya wazazi ambao watoto wao wamefutiwa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne visiwani Zanzibar wanakusudia kulifikisha mahakamni Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa kutoa adhabu hiyo kinyume cha sheria.

Wazazi hao walitoa kusudia hilo mjini hapa jana katika wakati wa mjadala uliowashirikisha wadau mbali mbali wa sekta ya elimu na wanaharakati kujadili uamuzi wa Necta wa kuwafutia matokeo wanafunzi 3,303 kutoka Tanzania bara na Zanzibar na kuwazuia kufanya mitihani kwa muda wa miaka mitatu.
Ameir Hassan Ameir alisema pamoja na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya baraza hilo , kuna haja kwa wananchi visiwani humo kuitisha maandamano makubwa kupinga kufutwa kwa matokeo hayo na kushinikiza kuondolewa kwa dhabu dhidi ya wanafunzi.
Akipinga taarifa ya Necta kwamba mitihani hiyo imefutwa kwa sababu ya udanganyifu uliofanywa na wanafunzi, Ameir alisema baraza limeshindwa kuthibitisha udanganyifu huo na hivyo haliwezi kujiondoa katika kashfa ya kuvuja mtihani.
Alisema kushindwa kwa Katibu Mtendaji wa Necta, Joyce Ndalichako kutoa maelezo juu ya idadi na majina ya wananfunzi waliofutiwa mitihani kutoka kila upande wa Muungano, kumeibua hisia kwamba Tanzania bara imeandaa njama za kuua elimu elimu Zanzibar .

“Necta wanayo majina ya shule na namba za shule zote za Zanzibar , hivyo si kweli kwamba hawajui majina ya wanafunzi waliofutiwa mitihani,” alisema Ameir huku akihoji uwepo finyu wa ushiriki wa Zanzibar katika muundo wa Bodi ya Wakurugenzi wa Necta.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana wakati wa mjadala huo, bodi ya Necta ina wajumbe 14 na kati ya hao sita wanatoka upande wa Zanzibar .
“Sisi tuna uchungu na Zanzibar yetu, kuvuja kwa mitihani na watoto kufutiwa mitihani ni matokeo ya kero za Muungano. Adhabu ya miaka mitatu itawapotezea watoto wetu muda wa kusoma, Wazanzibari tuungane tulishtaki Necta,” alisema.
Ali Hassan, Mkuu wa zamani wa Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja alisema ingawa Necta imeshindwa kutoa idadi ya wanafunzi waliathirika na uamuzi wa kufutwa matokeo, anaamini asilimia kubwa wanatoka upande wa visiwani wa Muungano.
Alisema maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Necta mbele ya mkutano na waandishi wa habari Februari 14 mjini hapa yanapaswa kusikilizwa tu na mtu asiyejua chochote na kuongeza kuwa kwa hatua hiyo: “ Mama Ndalinacho amefeli astep down.” Akiwa na maana aachie ngazi.

Faisal Mohamed, ambaye pamoja na Ali walisema ni miongoni mwa waathirika wa watoto wao kufutiwa mtihani alisema alivishambulia vyombo vya habari na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa alichoeleza kuwa kushindwa kuandika kwa kina habari za kashfa ya mitihani na kupokea kutoka Necta na kusaini taarifa bila kudadisi maelezo ya baraza hilo juu ya utata wa matokeo na hatua zilizochukuliwa dhidi ya wanafunzi.

Hata hivyo walalamikaji wote hawakueleza kusudio la kulishtaki baraza litatekelzwa kwa sheria, lakini walisema chini ya makosa ya jinai ni kinyume cha sheria kutoa hukumu ya jumla kwa kosa ambalo ni la mtu mmoja mmoja

Rais Kikwete akisalimiana na Mwanafunzi Godlisten Ole

"
"Nikiwa mkubwa natarajia kuwa kama wewe" ndio anavyoonekana kusema mtoto huyu kwa Kikwete mara baada ya kusalimiana walipokutana Longido wakati Kikwete alipoenda kufungua mradi wa uwezeshaji wa mifugo

Sunday, February 19, 2012

Msanii Mosp aendeleza elimu ya muziki maofisini


Msanii wa muziki wa asili na kizazi kipya, Amos Pauson akiwaimbia wafanyakazi wa gazeti la Habarileo juzi wakati alipotembelea gazeti hilo (Picha na Evance Ng’ingo)

Friday, February 17, 2012

Alice Foundation yatoa mafunzo ya katiba kwa wakazi wa Ubungo

 Bi Alice akiwa katika harakati zakuandaa notes kwa ajili ya wakazi hao ambayo iliandaliwa na Taasisi ya Alice kwa ushirikiano na Wizara ya Fedha ambapo elimu ya Mkukuta ilitolewa kwa watendaji na mwenyekiti serikali za mitaa zote katika kata ya Ubungo wilaya ya kinondoni Dar- es-salaam. wajasiriamali katika kata ya Ubungo pia walikuwepo.
 Alice akiwa na mtoa mada kutoka wizara ya Fedha
 Mtoa mada akiwafundisha wakazi hao masuala yahusuyo Mkukuta
 Wakazi wa Ubungo wakijadili masuala mbalimbali yahusuyo Mkukuta
Bi Alice akitoa neno la shukrani kwa wakazi waliohudhuria mafunzo hayo. Taasisi hiyo pia inajsihughulisha na masuala mbalimbali yahusuyo mazingira, kuwasaidia wanawake, Mkukuta na masuala mengine yanayoihusu jamii

Umuhimu wa kuwa na vitabu vya kutosha kwa kila mwanafunzi7tisha



Thursday, February 16, 2012

Watoto wa Tanzania Mitindo House wapewa fedha za kusoma


Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Benki ya Stanbic, Abdallah Singano (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Waathirika na VVU cha Tanzania Mitindo House (TMH), Bi Khadija Mwanamboka (kushoto) ikiwa ni msaada kwa kituo hicho kwa ajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali wakati maofisa wa benki hiyo walipotembelea kituo hicho Magomeni, Dar es Salaam jana. Wakishuhudia ni baadhi ya watoto wa TMH.

Wednesday, February 15, 2012

Ujamaa Arts Gallery yashirikiana na UNHCR yatoa mafunzo ya kuibua vipaji vya uchoraji kwa watoto waliopo katika kambi za wakimbizi nchini

 Mkurugenzi wa Ujamaa Arts Gallery Lorna Mashiba akihutubia katika ufunguzi wa maonesho yao yanayoendelea katika Gallery hiyo iliyopo katika eneo la Mbuyuni njia ya kuelekea Mwenge, wadau wanaombwa kuhudhuria na kununua picha hizo ili kuwezesha zoezi la kuwasaidia watoto hao kujifunza zaidi uchoraji wa picha
 Mkurugenzi Mkazi wa UNHCR nchini Oluseyi Bajulaiye akihutubia katika ufunguzi wa maonesho hayo ambayo yanaendelea katika Gallery ya Ujamaa
 Lorna Mashiba akiwaonesha wageni rasmi picha zilizochorwa na watoto hao ambazo zinauzwa
 Hizi ni baadhi ya picha zilizochorwa na watoto hao
Mdau wa masuala la sanaa ya uchoraji ambae pia ni Public Diplomacy Specialist wa Ubalozi wa Marekani nchini Finike Gogomoka akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa UNHCR Oluseyi Bajulaiye wakati wa hafla hiyo

Watu wengi walihudhuria kuona picha za watoto hao

 Wachina hawa nao walifika kushuhudia
 Hawa wadada ni wadau wakubwa wa Ujamaa Arts Gallery
 Mkurugenzi wa Ujamaa Arts Gallery Lorna Mashiba (kulia) akizungumza na Public Diplomacy Specialist wa Ubalozi wa Marekani Finike Gogomoka
 Zoezi la uchoraji wa picha live lilifanyika
 Wageni wakiangalia na kununua picha
Lorna akimshukuru mgeni rasmi ambae alikuwa ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa nchini Herman Mwansoko (kushoto)

Mzee Small atoa somo kwa wasanii


Msanii gwiji wa maigizo nchini Mzee Small akiwafundisha wasanii Richie (kulia) na JB (katikati) namna ya kuboresha kazi zao wakiwa katika kazi zao za sanaa

Uhaba wa vitabu shuleni nini chanzo


WADAU wa elimu wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali zinazopelekea wanafunzi kushindwa kufanya vema katika masomo pamoja na mitihani yao ya mwisho.

Ukosefu wa vitabu ni moja kati ya sababu za msingi ambazo zinasababisha wanafunzi kushindwa kufanya vema katika masomo yao.

nhjghjg.jpgLicha ya serikali kupitia wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kutoa ruzuku kwa shule mbalimbali za serikali kuanzia za msingi mpaka sekondari lakini bado hali sio shwari katika upatikanaji wa vitabu hivyo.

Ukosekanaji wa vitabu hivyo unasababaishwa na sababu mbalimbali moja wapo ikiwa ni mazingira tata ya upatikanaji wa tenda za kununulia vitabu hivyo.

Kuna tetesi kuwa wakuu wa shule ndio hutoa fedha za kununulia vitabu hivyo na hivyo kuwa katika mazingira ya kuwapatia tenda watu wao wa karibu na pengine wasiokidhi vigezo vya kupewa tenda hizo.


Matokeo yake watu hao huishia kununua vitabu pungufu na pengine kununua vitabu ambavyo haviendani na muda au mahitaji husika.


Mmiliki wa maktaba ya uuzaji wa vitabu ya Salamanda Clarence Mponda anasema kuwa awali wakati zabuni zikitolewa na Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi mfumo wa upatikanaji wa zabuni ulikuwa upo wazi na wa kuridhisha.

bnm.jpgAnasema kuwa ilikuwa ni rahisi kwa wazabuni wadogo pia kupata nafasi za kusambaza vitabu kwa kuwa walikuwa wakishindana.
Anasema kuwa kwa sasa suala la manunuzi ya vitabu lipo chini ya Tamisemi na kuongeza kuwa walimu wakuu wanakuwa na nguvu zaidi katika kununua vitavbu hivyo.

Anasema kuwa hali hiyo inaleta utata kwa kuwa mfumo wa upatikanaji wa zabuni sio wa wazi tena na inawawia vigumu wao kama wanunuzi wa vitabu kupata tenda za kununua vitabu hivyo.

“ Ni kwamba yani kwa sasa huu utaratibu ni kama vile sio mzuri kwa kuwa zamani ilikuwa rahisi mno sisi tulikuwa tunaenda moja kwa moja kugombania tenda katika Halmashauri za wilayani na mambo yalikuwa yanaenda vema sana” alisema Mponda.

Hata hivyo ofisa elimu wa wilaya ya Kinondoni Lucy Gurtu anapingana na hoja hiyo kwa kufafanua kuwa kwa kawaida walimu wakuu hawana idhini ya kununua vitabu moja kwa moja.

Anasema kuwa fedha za ruzuku za vitabu zinapotoka Tamisemi hufika kwanza katika ofisi ya wilaya na kisha kupangiwa matumizi kulingana na mahitaji ya shule husika.

Anasema kuwa kupitia wakaguzi wa elimu wa wilaya ofisi yake hugundua shule yenye uhaba wa vitabu na kuchanganua ni vitabu vya aina gani vinahitajika kwa muda huo.

Anasema kuwa pia walimu wenyewe hupeleka maombi kwa ofisa elimu wa wilaya kuelezea mahitaji halisi ya vitabu vinavyotakiwa.

Anasema kuwa kutokana na hilo kunakuwa hakuna mianya ya rushwa kwa kuwa walimu wakuu wanajengea hoja ya hitaji husika na kuliombea fedha.

Anasema kuwa wakuu wa shule huandika idadi ya vitabu inavyohitaji kwa kuchanganua ni vya aina gani na pia hata kama wakihitaji vifaa vya mahabara pia hutoa mapendekezo ya aina ya vifaa.

Anasema kuwa baada ya kutoa mchanganuo ofisi yake huwapatia fedha za kununulia vitabu husika na hivyo walimu hununua vitabu kulingana na mahitaji waliyohidhinisha.

Anasema kuwa iwapo walimu ikibainika kuwa hawakununua vitabu kulingana na makubaliano husika wakaguzi wa elimu wanalo jukumu la kuwachukulia hatua.


Anasema kuwa wakaguzi wa elimu kwa kushirikiana na wakaguzi wa ndani wa Manispaa huendesha zoezi la ukaguzi na kutoa ripoti kuhusiana na manunuzi ya vitabu husika.

“ Ni kwamba najua yani kunakuwa na changamoto mbalimbali ambazo kwa pamoja inatakiwa kushirikiana katika kuzitatua, mfano suala la kuwa na wakaguzi wa kutosha wa kukimbia huku na huko kukagua masuala muhimu ya elimu katika wilaya na mengineo” anasema Lucy.


Kutokana na hakli hiyo ya wakuu wa mikoa kupewa fedha za kununulia vitabu kulingana na mahitaji yao huenda ndilo linalopelekea mazingira ya rushwa katika kutoa zabuni hizo.


Naibu Katibu Mkuu wa ofisi ya waziri mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Jumanne Sajni anafafanua zaidi kuwa ofisi yake hupeleka fedha kwa ofisi za elimu za wilaya ambazo ndio huwa na jukumu la kununua vitabu.

hil.jpgAnasema kuwa walimu huwa na jukumu la kuidhinisha aina ya vitabu vya kununuliwa na kisha kupelekea maombi sehemu husika na pia ufuatiliaji wake hufanyika kiundani ili kuhakikisha kuwa vitabu vimenunuliwa.

“ Mimi ninchoweza kusema kuwa kama kuna walimu ambao wanachakachua ununuzi wa vitabu basi ni jukumu la kamati ya shule kuhakikisha kuwa linashughulikia suala hilo” alisema Sajni.

Alisema kuwa Mkuu wa shule husika anajadiliana na kamati ya shule katika kuamua aina ya vitabu vya kununua na
kisha kuanza kwa pamoja mchakato wa kununua vitabu hivyo.

Lakini hata hivyo alikiri kuwa huenda kukawepo kwa dalili za mazingira hayo ya rushwa na hivyo alitoa wito kwa maofisa wa elimu wa wilaya kushirikiana na maofisa ugavi na wakaguzi wa elimu kufuatilia manunuzi ya vitabu.
Mwisho