Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, October 21, 2013

Wanafunzi waliokosa mikopo kukumbukwa


SERIKALI imejipanga kuvikopa vyuo vikuu hapa nchini kwa ajili ya ada ya wanafunzi 1107 wa masomo ya kipaumbele waliokosa mkopo kutokana na fomu za maombi kuwa na dosari.


Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema hatua hiyo ni katika kutoa nafasi kwa wanafunzi hao hasa kutokana kompyuta kuwa na matatizo na baadaye kutoa fedha hizo kwa wanafunzi wengine.


“Ni kweli kosa limefanyika na Bodi, pamoja na kuwa na haki kisheria kuhamisha fedha kwa wanafunzi wengine walitakiwa kushauliana na Wizara kabla ya uamuzi huo ili kupata maoni ya nini kifanyike, hivyo tumefikia uamuzi wa kuwapa nafasi nyingine wanafunzi wenye masomo ya vipaumbele,” alisema.


Wanafunzi hao 1107 ni miongoni mwa wanafunzi 1661 ambao walikosa mkpo katika mwaka wa masomo 2013/2014 kutokana na kuwa na dosari mbalimbali.


Mulugo alisema tayari wameiagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutafuta kiasi cha sh bilioni 2 kutoka kwenye makusanyo ya wadeni au fedha za matumizi mengine na wizara itatoa kiasi cha bilioni 1.1 ili kufikisha sh bilioni 3.1 zitakazotumiwa na wanafunzi hao.


Akitia mchaganuo huo, Mulugo alisema zaidi ya sh bilioni 1.9 zitatumika kwa ajili ya chakula na malazi, sh milioni 221.4 kwa ajili ya vitabu na viandikio, sh milioni 686.34 kwa ajili ya mafunzo ya vitendo na sh milioni 221.4 za mahitaji maalumu ya vitivo.


“ Katibu anakwenda kuviandikia vyuo kuwapokea wanafunzi hao na suala la ada liwe deni kwa serikali ambayo tutalilipa katika bajeti ijayo, tunaamini kuwa fedha hizi hazitavuruga matumizi ya vyuo kutokana na kuwa vyuo vingi vina idadi ndogo ya ya wanafunzi hawa,” alisema.


Mulugo alitaja wanafunzi watakaonufaika kuwa ni wanafunzi wa ualimu wa Hisabati(20), Sayansi(164), wanafunzi wa Sayansi na Tiba(111), uhandisi –umwagiliaji(7), ualimu (617), Sayansi ya kilimo(20), Uhandisi (70) na Sayansi (98).


“Wanafunzi ambao wanatakiwa kurekebisha dosari zao wakashindwa kufanya hivyo wakati huu, hakutakuwa na huruma tena na fedha tutawapa wahitaji wengine. Majina yao yatatolewa na bodi hivyo wazingatie hili,” alisema.


Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Asangye Bangu kutokana na bajeti iliyotengwa, wanafunzi 31,539 ambayi ni asilimia 99.6 kati ya wanafunzi 31,647 waliotarajiwa kupatiwa mikopo. Asilimia 83 ya wanafunzi hao wamedahiliwa katika kozi za kipaumbele na kayi yao asilimi 44 wamedailiwa katika kozi ya ualimu zisizo za sayansi.


Alisema asilimia 29 ya walimu waliodailiwa kwenye kozi za kipaumbele za kozi za sayansi ya tiba, ualimu wa hisabati, ualimu wa sayansi, uhandisi wa mwagiliaji, uhandisi na sayansi za wanyama wakati asilimia 17 ni wanafunzi wa kozi zingine zisizo za kipaumbele.


Bangu alisema katika mwaka wa masomo 2013/2014 Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi iliidhinisha jumla ya sh bilioni 325 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ambapo kiasi cha sh bilioni 306 zinatoka serikalini na sh bilioni 19 zinatokana na marejesho ya mikopo lengo likiwa ni kukopesha wanafunzi 94,023 ikiwa ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo.


Wizara ya elimu na uongozi wa HESLB walikutana na Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kufuatia wanafunzi wapatao 36 kwenda kuonana na kamati hiyo kuasilisha kilio chao cha kukosa mkopo.
(mwisho)

Sunday, October 13, 2013

Bonah Education Turst Fund yazinduliwa yaanza na kampeni ya kuchangisha ada

Kulikuwa na burudani safi

Meneja wa Masuala ya Kijamii wa kampuni ya Tigo, Woinde Shisael akizungumza na waandishi kuhusiana na ushiriki wa Tigo katika kampeni hiyo

Pia kulikuwa na Fashion Show

Mkurugenzi Mtendaji wa Bonah Trust Fund, Bonah Kalua

Kikundi cha Sanaa cha Safi Cultural Center



Mwanamitindo Mahiri Asia alikuwapo kusaidia kutoa burudani

Picha ya pamoja kati ya Bonah Kalua na wageni waalikwa

Mimi niliamua kuchangia pia ili kufanikisha harakati za mwanamama Bonah Kalua (kushoto) ambae ni Diwani wa Kipawa 
analenga kusomesha watoto wengi sekondari ambao wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa fedha
Pia kwa pamoja tunaweza kusaidia harakati hizo za Bonah pamoja na Tigo kwa kuchangia.0716 667470



Haya Habari Kamili




Kwa sasa wadau mbalimbali wanazidi kujitokeza katika kusaidia harakati za serikali za kuimarisha elimu hapa nchini.

Tumeshuhudia Tasisi ya Hassan Majar Trust Fund ambayo hivi majuzi imezindua harakati zake za kusaidia upatikanaji wa madawari nchini kwa ajili ya kusaidia wanafunzi kusoma wakiwa wanatumia madawati.

Pia wapo wadau wengine mbalimbali kama vile Mamlaka ya Elimu Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikisaidia ujenzi wa mabweni kwa kusaidiana na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini.

Hivi majuzi ilizinduliwa rasmi Taasisi inayojishughulisha na kusaidia uboreshaji wa elimu ya Bonah Education Trust Fund na ilianza kampeni ya kuchangisha fedha za kulipia ada wanafunzi.

Taasisi hiyo ilizinduliwa katika Uwanja cha Mnazi Mmoja na Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa jana ambae aliwataka wananchi kuchangia fedha kwa lengo la kuwalipia ada wanafunzi 100 wa sekondari.

Slaa alisema kuwa ili kuwa na jamii bora inatakiwa vijana wapate elimu na kuongeza kuwa elimu ya sekondari ni msingi mzuri wa utakaowawezesha watoto kuona mbali.

Alisema kuwa mbali na serikali kuwa na kampeni ya kusaidia ujenzi wa mabweni, madarasa na vyumba vya maabra ni muda wa wanajamii kuhakikisha kuwa mabweni hayo na madarasa hayo yanatumiwa na wanafunzi.

" Najua hata tukijenga madarasa na mabweni kama hakuna wanafunzi ni kazi bura kabisa kinachotakiwa ni wanafunzi kupelekwa shule na ili kufanikisha hilo ni lazima kuchangia hivyo basi chondechonde tuungane"alisema Slaa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bonah Kalua ambae pia ni Diwani wa Kata ya Kipawa, alisema kuwa kutakuwa na kampeni mbalimbali za kuwataka wanajamii kujitokeza na kuchangia.

Alisema kuwa kuna namba ya simu ambayo ni 0716 667470 ambapo walioguswa na harakati hizo wanaweza kuchangia kwa njia ya Tigo pesa

Kwa upande wake Meneja anaeshughulikia masuala ya Huduma za Kijamii wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa Tigo inaendelea na harakati za kuwarudishia wanajamii mafanikio yake kwa kusaidia masuala ya elimu na mengineo.


" Tigo ina furaha kubwa kusaidiana na Taasisi hii katika kuifikia jamii ya kitanzania na kuipatia elimu na tuna imani kuwa fedha zinazochangiwa zitasaidia  wanafunzi hao kupata elimu bora" alisema Woinde.
Mwisho

Shirika lisilo la kiserikali la Hope 4 Young Gilrs latoa zawadi kwa washindi wa Insha

Watoto kutoka shule mbalimbali wakipatiwa ujumbe kwanza

Ongeza kichwa

Mgeni rasmi akitoa risala yake

Wanafunzi wakipewa vyeti







Wanafunzi walioshinda ndo hawa hapa


Habari Kamili.


TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya Hope For Young Girls imeendesha shindano la uandishi wa insha kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Tukio hilo lilifanyika jumamosi iliyopita katika hoteli ya Giraffe na kuwashirikisha wazazi wa wanafunzi hao walioshinda.

Katika shindano hilo wanafunzi walioibuka na ushindi ni pamoja na Nicole Othman wa sekondariya Kenton.

Shahista Amini wa shule ya msingi  Mlimani pamoja na Conish Tayari wa shule ya msingi Mwenge.

Katikahafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Naja Mammen Nielsen ambae ni mwakilishi kutoka Global Platform ya Upanga.

Katika hafla hiyo wanafunzi mbalimbali walipewa vyeti  vya kutambua ushiriki wao katika shindano hilo.

Wanafunzi hao ni Najima, Doreen,Grace,Agnes,Amie,Conish,Steve,Ashura,Janeth na Jane.
Mwisho  

Thursday, October 10, 2013

Fedha za mikopo kwishnei


KITENDO cha wanafunzi kukosa mikopo kwa muhula wa mwaka 2013 na 2014 inatokana na kuisha na hivyo kuwa chanzo cha baadhi ya wanafunzi kukosa mikopo kwa muhula wa masomo wa mwaka 2013/14.
 

Jana baadhi ya wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma Chuo Kikuu wa Iringa, Chuo cha Kiislamu cha Morogoro walikusanyika karibu na Ukumbi wa habari maelezo baada ya juhudi za kwenda Ikulu kugonga mwamba.





Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitenga sh bilioni 306 kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya juu nchini, ikiwa ni pamoja na waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo.


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa alisema jana wanafunzi waliopata ni kutokana na fedha walizokuwa wametengewa kwa kazi hiyo.


“ Wengine wamekosa kwasababu fedha zimekwisha, tumekopesha mpaka senti ya mwisho ilipoishia ndio ukawa mwisho.Na hili ni kamaida kwa watu kukosa kutokana na uhaba wa fedha,” alisema na kuongeza kuwa kama kunabaadhi ya watu wanaandamana kwa hilo itakuwa ni unaharakati wao.



Akizungumza kwa niaba ya wenzao, Athuman Mohamed amelalamikia hatua ya kukosa mikopo na kudai kuwa wengi waliokosa ni yatima na wasi na uwezo wa kujisomesha.

Sunday, October 6, 2013

"Wakuu wa shule jitaidini kutatua kero zenu" Mchome

SERIKALI imetaka wakuu shule kuwa mstari wa mbele kutatua baadhi ya changamoto zinazokabili shula na walimu wakati serikali ikiwa inashughulikia matatizo yao.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Consolata Mgimba alipokuwa akitoa salamu za Katibu Mkuu, Profesa Sifuni Mchome wakati wa kufunga kitaifa mafunzo ya wakuu wa shule za sekondari Tanzania bara kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES II).


Alisema serikali inatambua changamoto zinazokabili ikiwa ni pamoja na madeni, uhaba wa nyumba za walimu na kuwataka wakuu wa shule kuwa mstari wa mbele katika kutatua baadhi ya changamoto badala ya kuwa sehemu ya kuvunja moyo walimu.


Alisema ni imani yake kuwa wakuu wa shule watakuwa mstari wa mbele katika kutekeleza mkakati wa serikali wa Matokeo Makubwa ya haraka sasa (BRN) ili kuweza kuboresha ufaulu wa wanafunzi na kuinua kiwango cha elimu hapa nchini.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM), Dk Sisten Masanja alisema mafunzo hayo yamefanyika baada ya kubainika kuwapo upungufu  kwa baadhi ya wakuu wa shule katika uongozi na utawala, usimamizi na uandishi wa ripoti za matumizi ya fedha na ufuatiliaji na tathimini.


Madarasa yanayovuja Kunduchi yapatiwa msaada


Na Mdau wa Elimu
MADARASA matatu ya shule ya msingi Kunduchi iliyopo jijini Dar es Salaam yanavuja kiasi ambacho yamefungwa na kushindwa kuendelea kutoa huduma ya elimu kwa wanafunzi wa shuleni hapo.


Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Pelagia Mdimi aliyasema hayo kayika maadhimisho ya miaka 25 ya benki ya Eco Tanzania ambayo imetoa misaada mbalimbali kwa shule hiyo ambayo imegharimu Sh milioni 48.


Katika maadhimisho hayo benki ya ECo imetoa madawati 50, daftari 3000, viti na meza za walimu 50, penseli 2000 pamoja na kukarabai na kupaka rangi darasa la saba.


Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwalimu Pelagia alisema madarasa yanayovuja ni matatu na kwamba yalijengwa kwa msaada wa serikali ya Japan mwaka 2002 ambapo kwa sasa hayatumiki kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa .


"Shule hii ina wanafunzi takribani 2099 na walimu 51 ambapo tatizo la ukosefu wa madarasa ni jambo ambalo limekuwa likitukwaza katika kutoa elimu iliyo bora kwa wanafunzi wetu" alisema Pelagia na kuongeza kuwa hata walimu hawana ofisi ya kufanyia kazi jambo ambalo limesababisha kuchukua darasa moja n akulifanya ofisi.


Alisema kutokana na kukabiliwa na ukosefu wa madarasa pamoja na hayo yanayovuja, wanatoa wito kwa wananchi kujitokeza kuchangia ili waweze kuendeleza juhudi za kutoa elimu iliyo bora kwa wanafunzi wa shule hiyo.


Kwa upande wake Ofisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Isaac Chahe alisema katika kuadhimisha miaka hiyo benki hiyo imeazimia kuboresha elimu kwa kiwango chao huku wakilenga shule za msingi ili kuwajengea wanafunzi mazingira mazuri ya kupata elimu.


"Tunaamini  kuwa mchango wetu katika kutoa vifaa hivi utasaidia kwa kiasi kikubwa  kuboresha uelewa na hatimaye matokeo ya mtihani wa wanafunzi kwa mwaka ujao" alisema Chahe.


Hata hivyo aliahidi benki hiyo kuongeza jitihada ili kuleta maendeleo zaidi katika sekta ya elimu na hasa shule za msingi nchini kwani wanalo azimio la kuboresha uchumi na maendeleo katika nchi kupitia nyanja ya mbalimbali.
MWISHO.


Thursday, October 3, 2013

Coke Studio, a platform for learning music

Famous Comedian in town who was the  Master of Ceremony, Evance Bukuku (left) Coca - Cola Brand Manager  Maurice Njowoka, Lady Jaydee and Evance from this blog

Njowoka insists something to Jide

Madee

The B Band

Diamond the Coca Cola's ambossodor


Country Director for Coca-Cola Tanzania, Yebeltal Getachew (left ) Diamond and Coca Cola brand Manager in Tanzania Maurice Njowoka

Some hugs

Ongeza kichwa




Na Evance Ng'ingo

KWA sasa katika medani ya muziki hapa nchini na duniani kote kumekuwa  harakati zinazofanywa na wadau mbalimbali wa muziki ambapo wameamua kuwekeza katika fani hiyo.



Uwekezaji huo katika muziki upo kwa aina mbalimbali ambapo wapo ambao wanawekeza kwa kuwasaidia wasanii kujiinua kimuziki na pia wao ambao wanajipanga kuwekeza kwa kufungua miradi kadhaa ya kukuza muziki.



Miradi hiyo ni kama vile ile ya kuwekeza studio au vifaa vingine vya muziki ambapo wasanii wanaendelezwa kisanaa.



Miradi kama vile Tusker Project Fame, Epiq Bongo Star Search au ile iliyokuwa CocoCola Pop Idol ni moja kati ya miradi ambayo makampuni makubwa yamewekeza au kudhamini kwa lengo la kusaidia sanaa.



Miradi mingine inalenga kuinua asili ya muziki kwa kuanzisha nyimbo zenye vionjo vya muziki wa asili.

Mradi wa Coke Studio ni moja kati ya miradi ya kuendeleza muziki hapa nchini wenye lengo la kuendeleza muziki wa kisasa wenye asili ya Afrika.



Coke Studio ni kipindi muziki ambacho kitakuwa kikirushwa kwenye runinga na kwa hapa nchini kwa kuanzisha kitahusisha wasanii kama vile Nasib Abdul, Diamond na Judith Wambura, Lady Jaydee.



Hicho ni kipindi ambacho kitahusisha wasanii wenye miondoko tofautitofauti ya kisasa kitakuwa kikiitwa Coke Studio Afrika.



Kipindi hicho kinahusisha wasanii kutoka Afrika Mashariki na wengine wa kutokea Afrika Magharibi na Kusini.



Wasanii kutoka kona nyingine ya Afrika ni pamoja na Seif Keita kutoka nchini Mali, King Sunny Ade, Mi, Waje, Jimmy Jat and Bez froma Nigeria.



Kwa upande wa  Afrika Mashariki wengine ni pamoja na Octopizzo, Miss Karun and Just a Band wakiwa wanatokea nchini Kenya na pia kuna Hip Hop Panstula pia kuna na Lilian Mbabazi  wa Uganda pia.



Pia wapo akina Boddhi Satva pamoja na Tumi wa Afrika Kusini pamoja na kundi la Culture Music la kisiwani Zanzibar.



Kitaanza kurushwa kesho kuanzia saa tatu usiki katika luning ya ITV ambapo kitaanza kuoneshwa kwa miezi miwili.



Wasanii hao akina Diamond na Lady Jaydee ni wasanii ambao walienda nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki katika kurekodi kipindi hicho.



Baada ya kumalizika kwa season one ndio itaanza rekodi ya season 2 ambapo wasanii wengine watachaguliwa pia.



Umoja wa wasanii mbalimbali kama hao wakishiriki kwenye kipindi hicho watasaidia harakati za kupata muziki wa kisasa wenye asili ya Afrika.



Pia kutakuwa na wasanii walioshirikishwa katika kipindi hicho ambapo  kutakuwa na wasanii kama vile Bamboo wa Kenya, Sega na Dela pamoja na Kassongo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na pia Temi Dollface kutoka Nigeria.



Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka anafafanua kuwa Coke Studio itakuwa ikioneshwa Kenya, Uganda, Tanzania na Nigeria.



Anaongeza kuwa itaenda hewani kwa vipindi vinane vya dakika 45 kila kimoja huku kukiwa na saa mbili za vipindi maalum kwa mwaka mpya.



Aliongeza kuwa katika kila kipindi kutakuwa na masuala mbalimbali muhimu katika sanaa ambapo anatolea mfano wa ujengaji wa sauti za kipekee kutoka kwa wasanii.



" Pia kutakuwa na fursa ya watazamaji kuona kile kitakachokuwa kikijili nyuma ya pazia ambapo wataona namna kipindi kinavyotengezwa na mengine" alisema Njowoka.



" Kwa ni fursa kubwa sana kwa Tanzania kushirikishwa kwenye kipindi kama hiki kwa kuwa kuna nchi nyingi Tanzania ambazo zingependa kuwa na miradi kama hii lakini kwa sasa ni Tanzania ipo na wasanii  wetu pia wamo." alisema Njowoka.



Anaongeza kuwa hiyo ni fursa kubwa  kwa wasanii wa hapa nchini kutangaza kazi zao za sanaa pamoja na kuonesha vipaji vyao katika nchi nyingine nyingi za Afrika.



Anatolea mfano kwa nchi kama Pakistani ambao kipindi hicho kimekuwa na mafanikio makubwa huku kikikadiriwa kuwa na watazamajimilioni 77 kwenye You Tube peke yake.



Akizungumzia ushiriki wake katika kipindi hicho msanii Lady Jaydee anasema kuwa amekuwa akiimba na kujitangaza sehemu mbalimbali za ndani na nje ya Tanzania.



Anasema kuwa anaona kuwa kipindi hicho kitasaidia kuinua harakati zake za kujitangaza zaidi nje ya nchi.



"Kupitia kipindi hiki sisi kama wasanii mbali na kukuza vipaji vyetu, kukutana na kufanya kazi pamoja na wasani wengine lakini pia ni wakati muafaka  kusema kwa ile ndoto yangu ya kujitangaza kimataifa zaidi inaenda  kukamilika" alisema Lady Jaydee.





Kwa upande wake msanii Diamond Platnumz anasema kuwa akiwa kama balozi wa Coca Cola hiyo kwake ni muendelezo wa fursa ambazo amekuwa akizipata kupitia kampuni hiyo.



Kipindi hicho asili yake ni nchini Brazil ambapo kimekuwa kikiitwa Estudio Coca - Cola ambacho kilirushwa kwa mara ya kwanza machi 2007.



Kikiwa kinaoneshwa hapa nchini washabiki watakuwa na fursa ya kuona na pia kupakua (downloading) vitu mbalimbali kama Video huku pia wakiwa katika nafasi ya kushinda vitu mbalimbali.