Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, November 21, 2018

Diamond akabidhi rasmi kadi za bima ya Resolution kwa wakazi wa Tandale

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Resolution Insurance, Maryann Mugo akikabidhi kadi za bima ya afya kwa wakazi wa Tandale kwa dada wa msanii Diamond Platinum, Diamond aliahidi kuwapatia wakazi 1000 huduma hiyo ya bima (Na Mpigapicha Wetu) 

Na Mwandishi Wetu
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nasib Abdul, Diamond Platinum ameshakamilisha ahadi yake ya kuwapatia kadi ya huduma ya bima ya afya wananchi wa Tandale.

Diamond aliwahi kutoa ahadi hiyo wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa ya kuwa angewapatia kadi hizo wananchi 1000 wa eneo hilo ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwao.

Wakazi hao wamepewa msaada huo wa bima ya afya kupitia kampuni ya bima ya Resolution Insurance ambapo Mkurugenzi Mtendaji wake Maryann Mugo alibainisha kuwa huduma hiyo ni kwa ajili ya watu wanne kwenye familia.

Alisema,”sisi tunapenda kuwahudumia wananchi kujipatia huduma nzuri za afya na kwa kile alichokifanya msanii Diamond kuwasaidia wakazi hawa huduma ya bima basi ni fahari kubwa kwetu”.

Alisema, wananchi mzitumie vema kadi hizi kwa kuwa ni mkombozi halisi katika maisha yenu na kama mnavyojua kuwa mkikosa bima ya afya ni hatari kwa maisha yenu.

Kwa upande wake msanii Diamond aliyewakilishwa na dada yake Esma kwenye makabidhiano hayo aliwataka wananchi wa Tandale kutumia vema huduma za bima hiyo na kujiwekea akiba ya fedha ili mwisho wa siku huduma hiyo ya mwaka mmoja ikiisha waweze kujihudumia kama kawaida.

Alisema,”Diamond ameniagiza niwashukuru kwa kumwombea nay eye amewakumbuka kwa kuwaletea huduma bora ya afya kwa njia ya kampuni hii ya bima ya Resolution