Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, June 23, 2013

Ikiwa bado wiki moja wanafunzi 60,000 wameomba mkopo HESLB

Na Mwandishi Wetu WAKATI ikiwa imebaki wiki moja kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu wanaohitaji mikopo kuwa wamewasilisha maombi kabla ya muda wa ukomo, wanafunzi zaidi 60,000 wamejitokeza kuomba kupatiwa mikopo.

 Bodi  ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) katika taarifa yake, imesema mchakato huo ulioanza Mei Mosi mwaka huu na mwisho wa kutuma maombi ni Juni 30. 

Imesema mchakato unaendelea vizuri na  wanafunzi wengi wamejaza fomu za maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi ya Heslb, katika wiki mbili zilizopita,   idadi ya waombaji ilifikia 66,111 miongoni mwao, 424 wakiwa ni waombaji mikopo wa mara ya kwanza waliokwishakamilisha taratibu.  

Wanafunzi 5,320 walikuwa ni waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji. Aidha wanafunzi wanaoendelea na masomo waliokwishathibitisha kuendelea kupatiwa mikopo kwa mwaka ujao wa masomo ni 60,367. 

 Taarifa hiyo ya Bodi imewataka wanafunzi kuzingatia muda uliopangwa wa kuwasilisha maombi ya mikopo ambao mwisho wake ni Juni 30 mwaka huu.

 Katika mwaka ujao wa fedha, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetenga Sh bilioni 306 kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi 98,025 wa vyuo vya Elimu ya Juu nchini.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, aliposoma bajeti ya wizara hiyo hivi karibuni, alisema Serikali kupitia Bodi  ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) itatoa mikopo kwa wanafunzi 35,649 ambao ni waombaji wapya na 62,376 wanaoendelea. 

Hata hivyo wanafunzi wanaokidhi vigezo mbalimbali vilivyowekwa na bodi, ndiyo watakaopatiwa mikopo. 

Waziri  Kawambwa katika hotuba yake, alisema mwaka unaomalizika wa 2012/13, wanafunzi 98,773 waliwasilisha maombi na kati yao, 95,594 ndiyo waliopatiwa mikopo. 

 Idadi hiyo ikilinganishwa na wanafunzi  98,025  wanaotarajiwa kupatiwa mikopo mwaka ujao wa fedha,  lipo ongezeko la takribani asili

UDSM yaanza kutoa degree ya Petroli


Na Mwandishi wa Elimu Bora

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka huu kinaanza kutoa Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Petroli, Jiolojia na Uhandisi wa Mafuta.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Kampuni ya General Electron (GE) na Chuo  hicho kusaini makubaliano ya ushirikiano  kuongeza wataalamu wa gesi na mafuta nchini.

Makubaliano hayo yalifikiwa mwishoni mwa wiki baada ya Makamu Mkuu wa UDSM  Profesa Rwekaza Mukandala kusaini mkataba huo pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya GE, John Rice ambaye alikuwa nchini kwa ziara ya kikazi.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya pande zote mbili kukubaliana  kwamba Tanzania sasa ni  mzalishaji wa  mafuta na gesi Afrika Mashariki hivyo upo muhimu wa kuboresha mafunzo ya gesi na mafuta katika vyuo vya Tanzania.

Katika makubaliano hayo, wameazimia kuanzisha mtaala wenye ufanisi katika kufundisha masomo ya gesi na mafuta na kuwavutia pamoja na kuwapa ushiriki wakufunzi  ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wakufunzi kitaalamu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Profesa Mukandala alisema Tanzania inakabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo uhaba wa rasilimali watu wenye ujuzi unaohitajika katika kushiriki kikamilifu katika sekta ya gesi na mafuta.

“Makubaliano haya ni ishara ya mwanzo ya dhamira ya ushirikiano wa muda mrefu na wa faida kati ya taasisi zetu hizi mbili katika kutoa mafunzo ya wahandisi wenye ujuzi kwa ajili ya  sekta ya mafuta na gesi nchini,” alisema.

Rice alisema kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi nchini kwa zaidi ya 10 ikisaidia miradi mbalimbali hasa ya kuzalisha umeme na sasa inaanzisha  ofisi yake jijini  Dar es Salaam ambapo tayari  imeajiri  Meneja wake Mkuu ili kuendesha shughuli zake.

Mwisho

Fast Jet ilivyonogesha Siku ya Muziki Duniani, mengi ya kujifunza

Fast Jet's Commercial Manager Jean Uku

Wafanyakazi wa Fast Jet

Wakitoka kumpongeza msanii ambae ni mfanyakazi wa Fast Jet Nyemo




IKIWA juzi ilikuwa ni siku ya muziki duniani wasanii  mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya juzi walitoa burudani safi katika onesho la siku ya Muziki Duniani lililofanyika  katika viwanja vya Posta, Kijitonyama.

Tukio hilo lililodhaminiwa na kampuni ya ndege ya Fast Jet iliwashirikisha wasanii Elias Barnaba, Godzila, Kala Jeremiah na wasanii wengine mbalimbali wa utamaduni.

Huku lengo lake ni kuwakutanisha wadau wa muziki pamoja na wasanii ikiwa pia na lengo la kuwa na mwelekeo mpya wa sanaa na muziki.

Pia katika kuongeza hamasa mfanyakazi wa kampuni ya Fast Jet Nyemo Mwiluka aliimba wimbo wake wa Njoo Turuke na Fast Jet.

Pia aliimba nyimbo zake nyingine mbalimbali huku akisindikizwa na madansa wake pamoja na wasanii wengine.

Tamasha hilo lilidhaminiwa na Fast jet, Alliance France, Goethe Institute na Pepsi ambapo hufanyika kila mwaka Juni 22.
Akizungumzia udhamini wake wa tukio hilo Meneja Biashara wa Fast Jet Jean Uku alisema kuwa kampuni hiyo mbali na kutoa huduma usafiri pia imeamua kusaidia masuala ya sanaa kwa kuwa inatambua nafasi ya sanaa katika kukuza ajira hususan kwa vijana.
Ends

Thursday, June 20, 2013

Msanii wa filamu aibuka mteja wa laki 2 wa Fast Jet, kupewa ofa ya kupumzika yeney mafunzo ndani yake

Ilikuwa ni surprise

akielezea furaha yake

Ongeza kichwa

Ndo huyu mwanadada

Bsi wa Fast Jet akihojiwa

Akiagwa


 MSANII wa filamu Ndeshi Shoo ametunukiwa kuwa mteja wa laki mbili kutumia huduma ya ndege ya Fast Jet.

Ndeshi  aliwahi kushiriki katika filamu za Lost iliyoigizwa na msanii mahiri Yusuph Mlela na pia ameigiza kwenye filamu ya Fare Game ambayo imeandaliwa na Mzee Chilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere, Ndeshi alisema kuwa kwake imekuwa ni kama bahati kwa kuwa alikuwa na shauku ya kufanya matangazo na kampuni hiyo.

" Hii ni fursa kubwa kwa kuwa nilikuwa nikifikiria kuwa itakuwaje kama msanii pengine kuigiza filamu kwa kupitia kampuni hii"alisema Ndeshi.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Fast Jet, Tim Lee-Foster alisema kuwa msanii huyo anapatiwa ofa ya siku mbii katika hoteli ya Serena iliyopo kisiwani Zanzibar.

Alisema kuwa msanii huyo amekuwa ni mteja wa laki mbili kukata tiketi ya kusafiria na ndege tangia ilipoanza kutoa huduma ya usafiri hapa nchini.
Mwisho

Wednesday, June 19, 2013

Zantel kuelimisha wakulima kupitia SMS

Mkurugenzi wa Kilimo wa wizara, Daktari Mshindo Msola, alielezea kufurahishwa kwake na huduma hiyo





Mtaaalamu wa Bidhaa wa simu kampuni ya simu ya Zantel Cecil Mhina akifafanua namna ya upatikanaji wa taarifa za kilimo kupitia mtandao huo, pembeni yake ni Afisa Rasirimali Watu Mkuu wa Zantel Francis Kiaga na Mkurugenzi wa Kilimo katika Wizara ya Kilimo na Ushirika Mshindo Msola na  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Sibesonke inayoratibu taarifa hizo, Uwe Schwarz,. ( Picha na Mpiga Picha Wetu)


Na Mdau wa Elimuboratanzania
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, kwa kushirikiana na wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na kampuni ya Sibesonke leo wamezindua huduma mpya ya kutoa taarifa kuhusu kilimo kupitia simu za mikononi.
Huduma hiyo mpya inayofahamika kama,Z-KILIMO,itawawezesha wakulima nchini Tanzania kupata taarifa za papo kwa pao na uhakika kuhusu njia za kuendesha kilimo cha kisasa kwenye simu zao za mikononi.
Kupitia huduma hii ya Z-KILIMO, wakulima nchini, hata wale walio vijijini wataweza kupata taarifa muhimu za namna ya kuendesha kilimo cha kisasa na hivyo kuongeza uzalishaji na kukuza sekta nzima ya kilimo.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali watu cha Zantel, Francis Kiaga, amesema kwa kupitia huduma hii wakulima nchini watapata fursa ya kipekee kupata taarifa kuhusu kilimo moja kwa moja kupitia simu zao.
“Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu, na kinachangia sana kwenye kukuza na kuchangia uchumi wa nchi yetu, na huduma hii imekuja wakati muafaka katika kuendeleza juhudi hizo, lakini pia kuwapa wakulima umuhimu wa huduma ya simu katika namna wanayoihitaji zaidi’ alisema Kiaga.
Akielezea zaidi huduma hiyo Kiaga alisema itawasaidia zaidi wakulima katika kuokoa muda ambao zamani waliupoteza katika kupata taarifa kuhusu kilimo, na pia kuwaongezea uzalishaji wa mazao yao.
Huduma ya Z-KILIMO pia itawapa wakulima taarifa kuhusu maandilizi ya ardhi, aina za mbolea, aina za mazao, aina za mifugo, aina ya magonjwa yanayoshambulia mazao, upaliliaji, taarifa za usafiri, hali ya hewa pamoja na sehemu ya majadiliano baina ya wakulima.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kilimo wa wizara, Daktari Mshindo Msola, alielezea kufurahishwa kwake na huduma akisema itasaidia kufungua fursa zaidi kwa wakulima nchini.
‘Kupitia huduma hii, wakulima sasa wataweza kuboresha mbinu zao za kilimo katika hatua zote za kilimo na hivyo kuongeza uzalishaji’ alisema Dkt Msola.

Nao kampuni ya Sibesonke, ambao wameingia ushirikiano wa kiteknolojia na wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na wizara ya maenedeleo ya Mifugo na Uvuvi, ukiwa na lengo la uwafikia watanzania wakulima kuwapa taarifa muhimu za kilimo kwenye simu zao.

“Sibesonke ina furaha kwa kuwezesha watanzania kufaidika na teknolojia hii kupitia mtandao wa Zantel’ alisema Daktari Uwe Schwarz, Mkurugenzi Mkuu wa Sibesonke. “Kampuni ya Zantel imeonyesha dhamira ya dhati katika kuhakikisha teknoljia hii inawafaidisha watanzania wote kwa mtandao wake ulioenea nchi nzima’ alisiistiza Daktari Schwarz.

Wakulima wanaweza kujiunga na huduma hii kwa kubonyeza *149*50#, ambapo wataweza kupata maelekezo ya kutumia huduma hii.