Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, June 19, 2013

Zantel kuelimisha wakulima kupitia SMS

Mkurugenzi wa Kilimo wa wizara, Daktari Mshindo Msola, alielezea kufurahishwa kwake na huduma hiyo





Mtaaalamu wa Bidhaa wa simu kampuni ya simu ya Zantel Cecil Mhina akifafanua namna ya upatikanaji wa taarifa za kilimo kupitia mtandao huo, pembeni yake ni Afisa Rasirimali Watu Mkuu wa Zantel Francis Kiaga na Mkurugenzi wa Kilimo katika Wizara ya Kilimo na Ushirika Mshindo Msola na  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Sibesonke inayoratibu taarifa hizo, Uwe Schwarz,. ( Picha na Mpiga Picha Wetu)


Na Mdau wa Elimuboratanzania
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, kwa kushirikiana na wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na kampuni ya Sibesonke leo wamezindua huduma mpya ya kutoa taarifa kuhusu kilimo kupitia simu za mikononi.
Huduma hiyo mpya inayofahamika kama,Z-KILIMO,itawawezesha wakulima nchini Tanzania kupata taarifa za papo kwa pao na uhakika kuhusu njia za kuendesha kilimo cha kisasa kwenye simu zao za mikononi.
Kupitia huduma hii ya Z-KILIMO, wakulima nchini, hata wale walio vijijini wataweza kupata taarifa muhimu za namna ya kuendesha kilimo cha kisasa na hivyo kuongeza uzalishaji na kukuza sekta nzima ya kilimo.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Rasirimali watu cha Zantel, Francis Kiaga, amesema kwa kupitia huduma hii wakulima nchini watapata fursa ya kipekee kupata taarifa kuhusu kilimo moja kwa moja kupitia simu zao.
“Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wetu, na kinachangia sana kwenye kukuza na kuchangia uchumi wa nchi yetu, na huduma hii imekuja wakati muafaka katika kuendeleza juhudi hizo, lakini pia kuwapa wakulima umuhimu wa huduma ya simu katika namna wanayoihitaji zaidi’ alisema Kiaga.
Akielezea zaidi huduma hiyo Kiaga alisema itawasaidia zaidi wakulima katika kuokoa muda ambao zamani waliupoteza katika kupata taarifa kuhusu kilimo, na pia kuwaongezea uzalishaji wa mazao yao.
Huduma ya Z-KILIMO pia itawapa wakulima taarifa kuhusu maandilizi ya ardhi, aina za mbolea, aina za mazao, aina za mifugo, aina ya magonjwa yanayoshambulia mazao, upaliliaji, taarifa za usafiri, hali ya hewa pamoja na sehemu ya majadiliano baina ya wakulima.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kilimo wa wizara, Daktari Mshindo Msola, alielezea kufurahishwa kwake na huduma akisema itasaidia kufungua fursa zaidi kwa wakulima nchini.
‘Kupitia huduma hii, wakulima sasa wataweza kuboresha mbinu zao za kilimo katika hatua zote za kilimo na hivyo kuongeza uzalishaji’ alisema Dkt Msola.

Nao kampuni ya Sibesonke, ambao wameingia ushirikiano wa kiteknolojia na wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika pamoja na wizara ya maenedeleo ya Mifugo na Uvuvi, ukiwa na lengo la uwafikia watanzania wakulima kuwapa taarifa muhimu za kilimo kwenye simu zao.

“Sibesonke ina furaha kwa kuwezesha watanzania kufaidika na teknolojia hii kupitia mtandao wa Zantel’ alisema Daktari Uwe Schwarz, Mkurugenzi Mkuu wa Sibesonke. “Kampuni ya Zantel imeonyesha dhamira ya dhati katika kuhakikisha teknoljia hii inawafaidisha watanzania wote kwa mtandao wake ulioenea nchi nzima’ alisiistiza Daktari Schwarz.

Wakulima wanaweza kujiunga na huduma hii kwa kubonyeza *149*50#, ambapo wataweza kupata maelekezo ya kutumia huduma hii.





0 comments:

Post a Comment