Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, May 27, 2012

Jicho la blog hii liliangazia michezo weekend hii



Mwalimu wa mchezo wa gofu Mbwana Juma akiwaelekeza wachezaji wa timu ya gofu ya taifa wakati wa mazoezi yao ya kujiandaa na kombe la Afrika, kutoka kushoto ni Hawa Wanyache, Ayne Magembe, Madimna Iddi alikuwa akiwafundishia katika uwanja wa Gymkhana
 Kijana huyu alikuwa akijifunza namna ya kucheza Tennis
 Mwanadada huyu alikuwa akifundishwa kucheza Gofu
Hwa watoto nao walikutwa wakijifunza Tennis

Thursday, May 24, 2012

Mfuko wa Tushikamane kusaidia wazee na masuala ya elimu nchini

 Mbunifu wa mavazi Binti Afrika akipewa zawadi kutoka kwa Mama Bilal kutokana na mchango wake siku hiyo ya kuchangisha michango ya kuwasaidia wazee pamoja na masuala ya elimu nchini
 Watoto hawa wanafunzi wakiwa wanaonesha mavazi yao siku hiyo walikuwa kama wanamitindo
 Huyu mwanafunzi ndio mzuka ulimpanda na akashinwa kupozi akajikuta akiruka ruka jukwaani
Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee akipita mbele ya jukwaa kuonesha mavazi yake ikiwa ni sehemu ya kuburudisha wageni waalikwa.

Elimu ya soka kutolewa katika tamasha la Simba

Meneja wa ukumbi wa Dar Live Juma Mbizo akiwa na Juma Kaseja wakizungumzia kuhusiana na elimu na tamasha la sherehe za Simba litakalofanyika katika Ukumbi wa Dar live, wapenzi na wananchi kwa ujumla wameombwa kujitokeza kwenda kujifunza katika tamasha hilo.

Kutakuwa na elimu kuhusiana na soka na masuala mengine muhimu katika nyanja za soka nchini

Friday, May 18, 2012

Kipindi cha kuelimisha, kuburudisha na kuadabisha chaja EATV Alhamisi hii

 Mwendeshaji wa kipindi hicho Mboni Masimba akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
 Mboni akiwa na Meneja Uhusiano wa kipindi hicho Shamim Mwasha wa 8020blog

   Waandishi wa habari wakichukua picha na maelezo kwa ajili ya kuwajuza wananchi.

Na Mwandishi wa Elimubora
KIPINDI cha Mboni Talk Show chenye kuburudisha, kuelimisha na kufundisha  ambacho kitaanza kuoneshwa Alhamis ijayo katika kituo cha East Africa Television.

Kipindi hicho kitarushwa na  Mboni Masimba ambae alisema kuwa vipindi vya Talk Show kwa sasa vinapendwa na kutazamwa na watu wengi zaidi kutokana na uvutiaji wake na mijadala mbalimbali ambayo inazungumzwa katika vipindi hivyo.

Akizungumzia kipindi chake Mboni alisema kuwa kipindi hicho kitakuwa na sehemu tano ambazo ni Ufunguzi, wakati wa maswali kutoka kwa mtangazaji kwa wageni na kutoka kwa hadhira kwenda kwa wageni, na pia kutakuwa na kipengele cha My dreams come true ambapo kipindi chake kitatoa misaada kwa watu wenye mahitaji mbalimbali na pia kutakuwa na Tamati.

Alisema kuwa kutokana na ukubwa wa Luninga ya East Africa Tv anahakika kuwa watu kutoka nchi za Afrika Mashariki wataburudika na kufurahishwa na kipindi hicho cha kipekee huku akiwataka wadau mbalimbali kutoa maoni yao mara baada kitakapoanza kurushwa.

“ Ni kwamba Tanzania kuna watu wa aina mbalimbali na wenye vipaji mbalimbali ambao wanatakiwa kuendelezwa na hapa ndipo nguvu ya Tv Talk Show inahitajika na mimi nitahakikisha kuwa kupitia kipindi change cha Mboni Show nitawafikiwa kila wenye kuhitaji msaada wa kuendelezwa kuwa wanafanyiwa hivyo” alisema Mboni 

Mboni aliwataka wasanii kutumia vipindi vya Talk Show kwa ajili ya kutangaza kazi zao sanaa ndani na nje ya nchi ikiwa pamoja na kuitangaza nchi ya Tanzania.

Sunday, May 13, 2012

Kanisa la Redeemed Gospel Church latoa somo kwa Alice Foundation

Mwenyekiti wa Alice Foundation akipokea chakula kutoka kwa Mch. Mkenda na wazee wa baraza kanisa la Redeemed wakimkabidhi msaada Alice James Dosi kwa ajili kuwasaidia watoto walio na matatizo mbalimbali. Kanisa hilo lilitoa somo la upendo na moyo wa kusaidia kwa Taasisi hiyo

Friday, May 11, 2012

BSS NA BASATA WAPEANA SOMO

 Msanii wa muziki wa asili Chemundu Gwao akiwa na wasanii waliofanya vema katika BSS mwaka jana Haji Ramadhan na Wazzi
 Chemundu Gwao akichangia mada
Mmiliki wa Bernchmark Production ambae ndio mmiliki wa program ya BSS Ritha Paulsen  akisistiza jambo kwa mratibu wa BSS katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Vicky Temu.


Na Evance Ng’ingo
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii waliotoka katika mradi wa Bongo Star Search kuwa na mikakati ya kujiendeleza wenyewe badala ya kutegemea kusaidiwa na mradi huo pindi shindano linapokwisha.

Wito huo ulitolewa jana na mratibu wa BSS katika Basata Vicky Temu wakati akichangia mada katika mkutano uliowashirikisha BSS na wadau wa sanaa na kufanyika Basata.

Vicky alisema kuwa wasanii hao wanatakiwa kutambua kuwa uhusiano kati ya BSS na wasanii hao unamalizika mara baada ya shindano hivyo wanatakiwa kutumia vema elimu ya muziki waliyoipata wakiwa ndani ya shindano hilo kujiendeleza zaidi.

Hata hivyo alimtaka mwandaaji wa shindano hilo Ritha Paulsen kuwaendeleza wasanii hao ikiwa pamoja na kuingia mkataba na studio za kurekodia muziki kwa lengo la kuwaendeleza zaidi watakaofanya vema pindi shindano linapomalizika.


Wakati huo huo mwandaaji wa shindano hilo Rita, aliwataka waandishi pamoja na watangazaji wa redio na luninga kuwasaidia wasanii watokao katika BSS badala ya kuwakatisha tama.

Alisema kuwa kuna wadau mbalimbali katika vyombo vya habari na sanaa kiujumla ambapo wanawakatisha tamaa wasanii watokanao na mradi wa BSS kwa kutotaka kuwasaidia kuwatangaza.

Katika hatua nyingine gazeti hili lilishuhudia hali ya mtafaruku katika ya Rita na BSS katika suala la upatikanaji wa kibali cha mwaka huu na suala la upangaji wa majaji.

Rita alilalamikia kitendo cha Basata kutaka kumpatia kibali cha muda cha kuandaa shindano hilo kwa mwaka huu mpaka pale atakapomweka bayana mdhamini wake wa mwaka huu huku Rita akisisitiza kuwa apewe kibali kamili ili mdhamini wake aweze kusaini mkataba kwa kuwandio atakuwa na imani kuwa shindano lipo.

“ Sasa mkinipa kibali kamili si ndio mdhamini atatoa huo udhamini na kutuhakikishia kuwa anatudhamini kwa mwaka huu au? Mkinipa kibali cha kawaida ntashindwa kupata udhamini kwa nini kwanza msinipe kibali cha mwaka mzima” alihoji Rita.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Kitengo cha Matukio cha Basata, Malimu Mashili alisema kuwa baraza hilo haliwezi kutoa kibali kamili kabla halijapata mwelekeo wa shindano la mwaka huu ili kwa kuwa chochote kikiharibika ni baraza ndio litahusika.

Kikao kilimalizika huku Basata ikiwa imemtaka Rita kuwasilisha bajeti inayotaja zawadi, na gharama nyinginezo licha ya kuwa Rita aliwataka wampatie kibali kamili ili aweze kusaini mkataba na mdhamini wake lakini hata hivyo alisema kuwa suala la kutaja zawadi ni mapema mno kwa kuwa wadhamini wengine hujitokeza shindano likiwa limenza.

Mtafaruku mwingine uliibuka katika suala la upatikanaji wa majaji wa shindano hilo ambapo Basata ilimtaka Rita kuwapelekea majina ya watu watano ili iweze kuwachagua watatu kati yao huku ikisisitiza kuwa huo ni utaratibu wa kawaida.

Akionesha kushangazwa na utaratibu huo Rita alisema kuwa anapenda kuwatumia majaji wake wale wale kwa kuwa ndio ameshawajengea hisiza nzuri kwa washabiki wa BSS na huvuti kipindi hivyo kuwabadilisha sio haki.

Mkutano huo ulivuta hisia za wadau  mbalimbali wa sanaa waliokuwa katika mkutano huo uliodumu kwa saa tatu kwa lengo la kutathmini maendeleo ya BSS, lakini hata hivyo Basata ilimpongeza kwa kuendesha shindano hilo kwa miaka sita bila ya kusimama.
Mwisho 

Wanafunzi jitokezeni kEsho katika Ukumbi wa Nkurumah UDSM


 Meneja Masoko wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Omari Mbura akitoa maelezo kwa waandishi kuhusiana na tukio hilo la kesho katika ukumbi wa Nkuruma, pembeni yake ni Mustapha Hasanali
Mtaalamu kutoka nchini India ambae ni mmoja kati ya waratibu wa shughuli hiyo ya kesho.


Na Mwandishi wa Elimubora
WASANII wa muziki wa kizazi kipya Dully Sykes na Chidi Benz watasindikiza uzinduzi shindano la wanafunzi litakalofanyika kesho katika Ukumbi wa Nkuruma uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Shindano hilo litakalozinduliwa kesho linashirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchini chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ushirikiano na mpango wa kuendeleza wajasiriamali vijana unaodhaminiwa na serikali ya India kupitia mradi wake wa IndiAfrika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Meneja Masoko wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Mbura Omari alisema kuwa hakutakuwa na kiingilio siku hiyo ya kesho ambapo shughuli itaanza tangia asubuhi.

Akizungumzia shindano hilo Mbura alisema kuna vipengele vingi ambavyo vijana wanashindanishiwa ikiwa mojawapo ni kuangalia uelewa wao katika Nyanja za biashara, mazingira, uchumi na nyinginezo nyingi.

Alisisitiza kuwa utamaduni ikiwa ni moja kati ya Nyanja muhimu wanafunzi wanatakiwa kuandika masuala muhimu ya kujadili katika Nyanja ya utamaduni.

Alisema kuwa ili kuweza kuibuka mshindi katika shindano la hapa nchini na lile la Afrika kiujumla wanafunzi wanatakiwa kuonesha umakini katika kutetea kile ambacho wanaona kuwa kinafaa katika masuala ya utamaduni.

Alisema kuwa mshindi wa jumla katika kanda ya Afrika atapata milioni kumi lakini pia kutakuwa na mshindi wa nchi ambapo atapatikana mmoja katika kila Nyanja.

“ Katika shindano hili vijana watashirikiana katika nyanja za uandishi wa insha, upigaji wa picha na ubunifu katika kuwasilisha ujumbe pia lakini pia wataandika michanganuo yao katika Nyanja mbalimbali ambapo lengo ni kuwapatia fursa ya kuonesha uwezo wao katika kufikiri” alisema Mbura.

Katika kusisitiza na kuonesha nia ya kuimarisha ushirikiano huo mbunifu wa mavazi nchini Mustapha Hasanali aliahidi kusaidia mbunifu chipukizi mmoja katika wiki ya mitindo ya Swahili ambapo ataenda kushiriki kuonesha mitindo nchini Afrika Kusini.
Mwisho

Monday, May 7, 2012

Maziko ya mwanafunzi Isabela wa shule ya Little Beaumont

 Mwanafunzi Isabela ambae pia alikuwa ana malengo makubwa katika tasnia ya Modeling aliyefariki mwezi uliopita na kuzikwa nyumbani kwa babu yake Makongo Juu, mtoto huyu alikuwa bega kwa bega na mama yake ambae ni mbunifu wa mavazi, Evelyin Rugemalila ambapo mara ya mwisho alienda nae nchini Afrika Kusini katika wiki ya mavazi ya Afrika Kusini.
Wadau wa mitindo na mavazi wakiongozwa na mwanamitindo mahiri wa kimataifa wa ndani na nje ya nchi wakitoa heshima ya mwisho, Millen alikuwa na wadau wengine wa tasnia ya ubunifu wa mavazi nchini
Evance wa elimubora akiwa na baadhi ya watu walioenda na Bella katika wiki ya mavazi Afrika Kusini wakiwa pembeni ya kaburi alipolazwa Marehemu

Shindano la Excel with Grand Malt kwa vyuo vikuu lazinduliwa

 Msanii muziki Hip Hop Joe Makini akiburudisha katika Tamasha hilo lililofanyika katika sekondari ya Central Dodoma
Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt Consolata Adam (Mama Adam) kushoto akiwa na Meneja Masoko wa Tanzania Breweries Nick Tesha wakati wa uzinduzi wa shindano la Excel with Grand Malt wakati wa Tamasha la uzinduzi wa tamasha la 

Wasanii Mabalozi wa Malari waendeleza elimu kwa wanajamii dhidi ya ugonjwa huo

 Walishikana mikono kuashiria ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo
Wasanii wa Tanzania House of Talent (THT) wakitumbuiza katika uzinduzi wa kampeni ya Night Watch inayolenga kuhamasisha matumizi ya vyandarua nyakati za usiku
Balozi wa kujitolea wa vita dhidi ya ugonjwa wa Malaria Mwasiti Almasi akimkabidhi fulana yenye ujumbe wa mapambano ya vita dhidi ya Malaria Michael Finlay wa ExxonMobil ambao ni wadau wakubwa wa mapambano dhid ya Malaria ( Na Mpigapicha Wetu)
Diamond alikuwapo kuwapa tafu.

Na Mwandishi Wetu
WASANII ambao ni mabalozi wa vita dhidi ya Malaria wametakiwa kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo ili kuinusuru jamii kubwa ya wanajamii.

Wito huo ulitolewa juzi na Meneja wa Mradi wa Kitaifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) Dk Ally Mohamed wakati akizindua kampeni mpya ya kupambana na ugonjwa wa Malaria iitwayo Night Watch inayoratibiwa na mradi wa Zinduka na kuwashirikisha mabalozi hao.

Dk Mohamed alisema kuwa wasanii wanaweza kutumia nguvu ya sanaa katika kuielimisha jamii juu ya ugonjwa wa Malaria hasa kwa kuondoa dhana potofu ambazo zinarudisha nyuma juhudi za serikali katika kupinga ugonjwa wa Malaria.

Alisema kuwa kampeni hiyo mpya ya Night Watch ambayo inawahamasisha wanajamii kutumia vyandarua nyakati za usiku ni kampeni nzuri na yenye kuleta tija katika vita dhidi ya Malaria.

Aliongeza kuwa  kuna uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa maambukizi ya malaria nyakati za usiku  na hivyo aliwataka wasanii hao kutumia nafasi zao katika jamii kuhakikisha kuwa wanaitumia vema kampeni hiyo ya Nighwatch kuwakumbusha wanajamii kutumia vyandarua na masuala mengine muhimu.

“ Mradi NMCP unatambua mchango wa wasanii katika kupambana na ugonjwa wa Malaria ambapo kupitia kamepni hizi zinazofanywa mmewezea kuongeza uelewa wa watu juu ya ugonjwa huu na namna ya kupambana nao” alisema Dk Mohamed.

Wakizungumzia kampeni hiyo wasanii Mwasiti Almasi na Fid Q alisema kuwa wakiwa kama wasanii watatumia vipaji vyao katika kuhakikisha kuwa wanawakumbusha wanajamii umuhimu wa kutumia vyandarua.

Fiq Q alisema kuwa atahakikisha kuwa katika ngazi ya kifamilia wazazi na watoto wanatumia vyandarua kila usiku ili kuweza kuepuka maambukizi dhidi ya ugonjwa huo.

Pia hafla hiyo ilihudhuriwa na Michael Finlay wa ExxonMobil ambao kwa pamoja na African Barrick Gold ni wamekuwa wakidhamini shughuli mbalimbali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.

Kampeni hiyo ya Nightwatch itaanza kutangazwa katika kituo cha redio cha TBC kuanza kesho (Jumatano) ambapo wasanii wanaoshiriki katika kampeni hiyo ni Diamond, Barnaba, Linah, Mwasiti, Bi Kidude na Professor J.
Mwisho