Help Children
Love them
Saidia Watoto

Saturday, December 13, 2014

Tigo yadhamini maonesho ya Tehema kwa vijana, Viwanja vya Posta

Wadau kutoka Kituo cha Utamaduni cha Ujerumani, Goethe Institute wakiwa kwenye maonesho hayo.

Ofisa kutoka mradi wa Data Huru ulio chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Daudi Fufuji akitoa maelekezo kuhusiana na namna ambavyo mradi huo unafanya kazi, maadhimisho hayo yalidhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo

 Wanafunzi wa Chuo cha A3 Institute wakionesha manjonjo yao ya upigaji wa picha katika maonesho hayo ya Tehama.
 Chombo maalum ambacho kinatumika kupigia picha kutokea angani hapo kilioneshwa namna kinavyofanya kazi.
 Ofisa kutoka mradi wa Data Huru ulio chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Daudi Fufuji akikipokea chombo maalum cha upigaji wa picha za ramani mbalimbali kutokea juu angani.
Baadhi ya mabanda ambayo wadau mbalimbali wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) walihudhuria.

Tuesday, November 25, 2014

Graduation ya Salome Magaya aliehitimu KIU pamoja na mwanae Lily Magaya aliehitimu Saut

Sunday, October 19, 2014

Bahari Rotary yawapokea waendesha pikipiki wa Mombasa wanaohamasisha elimu dhid ya Polio

Wakiwa katika picha ya pamoja waendesha pikipiki hao pamoja na maofisa wa Bahari Rotary


Mr Jp akielekeza kitu kwa waendesha pikipiki hao


Kiongozi wao akizungumza na uongozi wa Bahari Rotary



Na Evance Ng'ingo
WAENDESHA Pikipiki wametakiwa kutumia kazi yao hiyo kuielimisha jamii katika kupambana na ugonjwa wa Polio.

Wito huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa Chama Cha Waendesha Pikipiki wa Mombasa, Ally Fedha wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Fedha akiwa na waendesha pikipiki wenzake 20 wameendesha pikipiki zao wakitokea Mombasa nchini Kenya hadi Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kampeni yao katika kupambana na ugonjwa wa Polio.
Alisema kuwa waendesha pikipiki wanazunguka sehemu mbalimbali na wanakuwa wapo karibu zaidi ya wanajamii.

Alisema kuwa kwa kufanya hivyo wanaweza pia kutumia fani yao hiyo katika kuzungumza na wanajamii masuala mbalimbali kuhusiana na magonjwa na mambo mengineo ya kijamii.

"Najua uendeshaji wa pikipiki ni moja kati ya kazi za karibu zaidi na jamii, yani ni kazi ambapo mwendesha pikipiki anaweza kufika kila katika jamii inayomzunguka na kuzungumza na wanajamii husika tena kwa urahisi"alisema Fedha.

Akizungumzia harakati zao za kuhamasisha jamii dhidi ya ugonjwa wa Polio alisema kuwa wamezungumza na jamii za watu mbalimbali njiani wakiwa wanatokea Mombasa kuja Tanzania.
Alisema kuwa mbali na kufundisha na kuhamasisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo pia wanachangisha fedha kwa ajili ya kuisaidia klabu ya Mtwapa Rotary iliyopo Mombasa kupambana na ugonjwa huo.

Kwa upande wake Raisi wa Klabu ya Bahari Rotary ya hapa nchini, Ally Abdula alisema kuwa wamefurahishwa na juhudi za vijana hao kutokea Mombasa kuja hadi Tanzania kuelimisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Alisema kuwa klabu za Rotary ni klabu ambazo zipo kwa ajili ya wanajamii na zinahitaji pia kuwezeshwa ili kuihudumia jamii inayozizunguka.

"Hawa ni vijana ambao wameamua kuendesha pikipiki wakitokea Mombasa kuja hadi hapa nchini na njiani wamezungumza na watu mbalimbali na kuwaelimiesha namna bora ya kupambana na Polio sasa harakati kama hizi nzuri kwa kuwa pia wanachangisha fedha za kusaidia Klabu ya Mtwapa Rotary ya nchini kwao"alisema Abdula.

Waendesha Pikipiki hao waliwasili hapa nchini Ijumaa wakitokea Mombasa kupitia Tanga na kisha kuwasili Dar es salaam, na wanaondola leo hapa nchini.

=============== 

Bahari Rotary yawapokea waendesha pikipiki wa Mombasa wanaoelimisha masuala ya Polio

Wakiwa katika picha ya pamoja waendesha pikipiki hao pamoja na maofisa wa Bahari Rotary

Thursday, October 2, 2014

Penzi la nguruwe lamsitisha masomo

Picha ya Maktaba




UNAWEZA kudhani ni Hekaya za Kusadikika! Lakini ni  kisa  cha kweli kwamba, mama mzazi  amemshitaki polisi mwanaye wa kiume ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16 kwa kile anachodai amechoshwa na tabia ya mwanaye ya kufanya mapenzi na  nguruwe  wao  jike  mara kwa mara na hata kujikuta akiacha shule.
 
Amelalamika akidai kuwa kijana huyo amenogewa `penzi’ la mnyama huyo maarufu hapa kama “kitimoto au Noah” kiasi cha kumfanya aache masomo na   kuwa mtoro sugu shuleni.

Nguruwe huyo  jike  inadaiwa  anafugwa  na  familia  ya mwanafunzi huyo anayesoma katika  shule moja  ya umma  ya sekondari, Manispaa  ya Sumbawanga.

Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Kitengo  cha Polisi Jamii  mkoani Rukwa, Sixmund Kibassa  aliyemweleza mwandishi  wa habari  hizi  jana kuwa, mama mzazi wa mtoto  ameripoti tukio hilo katika jeshi polisi. 

Kibassa amesifu uamuzi huo, akisema ni mafanikio  makubwa  yanayotokana na Mpango Shirikishi wa Kitengo  hicho  wa kurejesha  shuleni watoto  ambao ni watoro  sugu.

Anasema mwanafunzi  huyo  (jina limehifadhiwa) ni miongoni mwa watoro sugu 70 kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari katika Manispaa  ya Sumbawanga waliorejeshwa hivi karibuni kupitia mpango huo shirikishi wa kuwarejesha  watoro  shuleni  unaotekelezwa na Kitengo  cha Polisi Jamii  mkoani humo.

Kwa mujibu  wa Kibassa,  wazazi  na walezi wenyewe  wanafika katika kitengo  hicho  cha polisi  jamii  na kuripoto  kuhusu   watoto  wao  ambao  wamekatiza masomo .

Aliongeza kusema kuwa,  wazazi  na walezi hao  wanafichua ya kwamba watoto  wao hao  licha  ya kutokwenda shuleni, lakini pia nyumbani hawaonekani kwamba baadhi yao wamebainika kutumia muda wao  mwingi  kunywa pombe  vilabuni badala  ya kusoma.

“Sasa  hivi  karibuni  ni  juzi  tu  mama mmoja  alinifuata  na kuniripotia  kisa  cha mwanae wa kiume  anayesoma Kidato cha Pili  katika shule moja ya sekondari kwamba  licha ya kuwa mtoro sugu shuleni; lakini  pia  amekuwa na tabia   chafu  ya kufanya  mapenzi  na nguruwe  wao  jike   mara kwa mara …. Nilipomhoji kijana  huyo  alikiri kufanya hivyo …. basi  tulimnasihi, “ alieleza.

Kwa mujibu  wa Kibassa  baada ya kumsihi  mwanafunzi  huyo alikubali  kuendelea na masomo  ambapo  alirejeshwa shuleni kwake  na kupokelewa  na walimu  na wanafunzi wenzake  kwa furaha.

Daktari wa Tiba  ya Binadamu, Dk Paulo Maiga  akizungumzia tukio hilo alikiri  kuwa  mwanadamu  kufanya mapenzi  na mnyama kuna madhara makubwa ikiwemo  kuambukizwa  virusi  ambavyo  vikingia  mwilini mwa  binadamu  kuna uwezekano mkubwa  visiweze kutibiwa .

“Hili  ni tatizo  kubwa madhara  yake ni makubwa  huyu nguruwe anaweza kuwa  ameshambuliwa na  virusi vya ugonjwa  ambao ukiingia  na kumshambulia  mwanafunzi  huyo  upo uwezekanao  mkubwa  kusiwepo na tiba,“ alisisitiza Dk. Maiga.


Sunday, September 28, 2014

Milioni 100 zapatikana kusaidia elimu kata ya Kipawa, zimechangishwa na Diwani wa kata hiyo Bonnah Kalua

 Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund,Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Dar es Salaam,Ndg. Ramadhan Madabida akitoa hotuba yake kabla ya kuanza kuendesha harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo.
 Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa akitoa hotuba yake kwa wageni wa mbali mbali (hawapo pichani) waliohudhulia hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo.Picha zote na Othman Michuzi.
 Katibu wa Bonnah Education Trust Fund,Mary Muwasa akizungumza machache ikiwa ni pamoja kuwatambulisha wadhamini mbali mbali waliojitolea ili kufanikisha harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
  Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund,Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Dar es Salaam,Ndg. Ramadhan Madabida (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani Elfu 8 kutoka kwa Mwenyekiti wa GCUT Group Tanzania,Lucy Jeremiar Gilya.Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani Elfu 15 kutoka kwa Meneja wa Miles Networks International nchini Tanzania,Diana Paul (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Sh. Mil. 4.4 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Kampuni ya Resolution Insurance,Angela Tungaraza (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akipokea mfano wa hundi ya Sh. Mil. 9.8 kutoka kwa Meneja Uajiri wa Kampuni ya Aramex Tanzania,Jane Stella Njagi (kulia).Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa.
 Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Ndg. Ramadhan Madabida akiendelea kutoa hotuba yake.
 Meza Kuu.
 Mshehereshaji katika hafla hiyo,alikuwa si mwingine bali Mdau Ephrahim Kibonde.
Baadhi ya wageni waliohudhulia hafla ya ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund wakifatilia kwa makini harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.


Some Journalists that turned up katika event hiyo

Wadhamini mbalimbali walikabidhi michango yao


Officials from Jubilee Insuarance

Bona na Madiwani wenzake

na Marafiki zake