Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, December 30, 2012

Ridhwani Kikwete atoa somo la maadili kwa Taswa

Katibu Mkuu wa Taswa Amir Mhando akiwatambulisha wageni katika mkutano mkuu wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo( Taswa) ulioendana sambamba na semina kwa waandishi wa habari

Waandishi wakijitambulisha mmoja mmoja


Ikafika muda wa kupiga picha na mgeni rasmi wa mkutano huo Ridhwan

Mwandishi Mkongwe Mzee Salim akitoa mada katika mkutano huo


Mwenyekiti wa Taswa Juma Pinto akitoa elimu yake

Watoa mada wakiwa wanafuatilai kwa makini kutoka kulia ni Mwina Kaduguda aliyewahi kuwa katibu wa Simba, katikati ni Willy Chiwango na kushoto ni mzee Salim mhariri wa kwanza wa michezo wa Daily news 

Mdau wa soka Ridhwan Kikwete akitoa mchango wake katiak kuiramisha masuala ya uandishi wa habari za michezo nchini ambapo alisisitiza suala la waandishi kuepuka kuchanganya upenzi wa timu katika kuripoti michezo

Habari Kamili kuhusiana na nin kilichojili na kuzungumzwa katika mkutano huu zitawajia kesho mchana kwanza leo onjeni picha za matukio tu. 



Friday, December 28, 2012

Mama Kikwete anastahili pongezi kwa kuimarisha elimu nchini

Rais wa Zanzibar, Dk Shein akimpongeza Mkurugenzi wa Home Shoping Center kwa kusaidia chakula kwa shule ya Wama kwa miaka mingi

Shein akipanda mti kuimarisha mazingira shuleni hapo

Hii ni sehemu ya bafu ambapo watoto wasomao shuleni hapo wanatumia

Mahala pa kulala ni pasafi na pa kuridhisha

Hiki ni chumba cha kusomea masomo ya kompyuta kwa wanafunzi wa shuleni hapo

Shein alifurahia sana

Geti la kuingilia shuleni hapo ni sehemu kubwa na yenye kuvutia sana

Wanafunzi wakiimba kuwaimbia wageni waliofika shuleni hapo. Hapo ilikuwa wakati wa kuifungua shule hiyo na kwa sasa blog hii inafanya utaratibu wa kuwasilaiana na wahusika ili kuangalia uwezekano wa kuitembelea shule hiyo tena mwa ujao

Tuesday, December 25, 2012

Elimu izingatiwe katika kuboresha Tasnia ya mavazi Bongo

Wanadada na wanamama ambao kwa kiasi kikubwa wamewekeza katiak sekta ya ubunifu wa mavazi nchini (kushoto) ni Asia Idarious ambae ni mwandaaji wa onesho la Usiku wa Kanga za Kale pamoja na Lady in Red akiwa na wadau wa mavazi ya Abaya ambayo ni ya dini ya kiislamu wakiwa katika onesho la mavazi hayo ya Abaya yaliyofanyika Hyat Kempinski Hoteli 

Wageni wakiingia katika onesho hilo

Wadada ambao wanatumia tasnia hiyo ya unbunifu w amavazi kujiongezea kipato (wanamitindo) wakiwa na Asia Idariou, kumbe tasnia hii ikiboreshwa zaidi na kukawa na msisitizo katiak elimu ya ubunifu wa mavazi basi inaweza kuwa tasnia kubwa hapa nchini 

Mavazi yenyewe ndo hayooo hapo

Wiki ijayo mtfahamu profile ya Mama wa nguvu wa Windhoeck

Mama Rgemalila wa Windhoek na Climax ambao wamekuwa wakisaidia harakati za fashion nchini na pia kuongeza ajira kwa watu wengi hasa vijana

Mbunifu mahiri nchini Evelyn Rugemalila (katikati) pembeni yake ni watu ambao wamewabunia mavazi yao akiwamo mama Rgemalila kulia

Mama Rugemalila akiwa na bana ya bidhaa yake pembeni ni inatia furaha kuwa na hali kama hii ya ujasiriamali katiak kujituma na kuendeleza kazi nchini

Shear Charity Ball Party, husaidia mengi likiwamo suala la elimu

Shear wa pili kulia akisakata muziki na wadau wake kushoto ni Slyvia Lupembe Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) hapa ilikuwa katika Shear Party ya mwaka 2011

Mgeni rasmi alikuwa akitoa neno

Shear huyu wa hapa mwanzoni ambae mwaka huu inaonekana kuwa hiyo function haikuwapo tena huku wadau wakiiulizia


Fedha wazipatazo kwa njia ya michango husaidia masuala mbalimbali likiwamo suala la elimu pia

Sunday, December 23, 2012

Nimekuja Bongo kujifunza muziki---Ngeruka Faycal

Elimu kumbe sio katika masuala ambayo yamekuwa yakionekana kuwa ni rasmi peke yake lakini kumbe unaweza kujiongezea elimu hata katika tasnia nyingine kama vile muziki na nyinginezo ambazo nazo zimekuwa zikipelekea maisha kusonga mbele

huyu ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Rwanda ambae kwa sasa yupo hapa nchini kwa ziara ya kimafunzo ya muziki akishirikiana na wasanii wa hapa nchini kujifua zaidi
Akiwa na msanii Cyril wa hapa Bongo

Akiwa na Cyril, Ben Paul pamoja na yeye mwenyewe

Hawa wadau wakishajipika kimuziki na wakitoa ngoma yao basi mambo yatakuwa mazuri sana    



Pata habari kamili.


MSANII wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Rwanda aitwae Ngeruka Faycal amesema kuwa Tanzania ni sehemu ya kujifunzia masuala mengi yahusuyo muziki na sanaa nzima kiujumla.

Faycal alisema kuwa kwa sasa ameamua kujihusisha zaidi na wasanii kutoka Tanzania na hivyo amekuja kujifunza kwanza muziki unavyotakiwa kwenda.

Akiwa hapa nchini anatarajia kuachia wimbo wa Kiswahili na msanii mahiri wa nyimbo za Bongo Flava Ben Paul wa hapa Tanzania.

Msanii huyo mwenye makazi yake nchini Ubelgiji anasifika kwa uwezo wake wa kupanga sauti mbalimbali na kwa sasa tayari ameanza mazungumzo Ben Paul kupitia meneja wake wa iliyopo nchini Ubelgiji.

Aliliambia gazeti hili kuwa amekuwa akifuatilia namna ambavyo Ben Paul anaimba na amekuwa akifanya vema katika muziki huku akisisitiza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akivutiwa na vionjo vya muziki wa Jazz vilivyopo katika nyimbo za Ben Paul.


Naye Ben Paul wakati akizungumza na gazeti hili alisema kuwa mpango wake kwa sasa ni kujitanua zaidi kimuziki kwa hiyo kuimba na msani huyo wa Rwanda ni hatua moja wapo ya kutimiza ndoto zake.


“ Mimi naona kuwa kwa sasa huyu msanii ni msanii ambae anaweza kuimba kila aina ya sanaa na pia naona kuwa kwa sasa kuna uwezekano wa kufanya kazi pamoja ila ndio mazungumzo yanaendelea kati ya meneja wangu na wa Code” alisema Ben Paul.


--- -------





Mmiliki wa Hoteli ya Peacock Mfugale atoa somo kwa wafanyabiashara ndogondogo

Mfugale akimkabidhi mwakilikishi wa TBC 1 zawadi kwa kuonesha inshara ya shukrani kutokana na msaada wa Redio hiyo katika kukuza biashara zake

Mmiliki wa hoteli hiyo Mfugale akitoa neno la shukrani kwa waandishi kuwashukuru kwa msaada wao katika kusaidia kukuza biashara zake za hoteli

Mwandishi wa Chanel Ten Kibwana Dachi akitoa neno la shukrani kwa niaba ya waandishi waliohudhuria

Waandishi walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali siku hiyo kabla ya kuanza ziara ya kutembelea vyumba vya hoteli yake mpya

Hiki ni chumba chenye hadhi ya kidiplomasia

Mfugale aliongozana na waandishi hadi vyumbani ambapo alipata fursa ya kuwafafanulia masuala mbalimbali

Sehemu za ndani za vyumba hivyo

Mahala pa kunawa mikono

Hapa akiwaonesha jakuzi lililopo katika moja ya vyumba vya hoteli hiyo

Ulifika wakati wa kusakata muziki ambapo wafanyakazi na waandishi kwa pamoja walicheza

Wafanyakazi wa East Africa Television wakiwa na Mfugale

Habari Kamili


MMILIKI wa hoteli za Peacock nchini Joseph Mfugale ametoa elimu kwa wajasiriamali wanaochipukia kuepuka kukata tamaa na badala yake wajikite zaidi katika kujiendeleza kielimu na kibiashara kiujumla.

Alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya miaka 20 tangia kuanzishwa kwa hoteli yake ya Peacock iliyopo Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Akizungumzia mikakati ya maendeleo ya hoteli zake Mfugale alisema kuwa kwa sasa anampango wa kujenga hoteli ya nyota tano katika eneo la Kigamboni itakayokuwa na uwanja wa gofu humohumo.

Mfugale alisema hayo juzi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kusherehekea miaka 20 tangia kuanzishwa kwa hoteli ya Peacock iliyopo Mnazi Mmoja, Dar es salaam.

Mfugale alisema kuwa kwa sasa biashara ya hoteli inazidi kukua kwa kasi hapa nchini na kuna kila sababu kwa wawekezaji wazawa kuhakikisha kuwa wanawekeza katika sekta hiyo iliyoajili watu wengi.

Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka 20 tangia kuanzishwa kwa hoteli ya Peacock  ya Mnazi Mmoja tayari amepanua biashara za hoteli kwa kujenga jengo jipya la hoteli hiyo lililopo nyuma  ya hoteli hiyo lenye vyumba.

Alisema kuwa pia anaendelea na ujenzi wa jengo la Peacock lililopo Iringa mjini ambalo lotaisaidia kuongeza ajira kwa vijana katika mkoa huo pamoja na kuwahifashi watalii.

Waandishi wa habari walipata fursa ya kutembelea vyumba vya jengo jipya la Peacock la Mnazi Mmoja ambapo kuna vyumba vya hadhi ya raisi, wanadiplomasia pamoja na watu wa kawaida.
Mwisho.


Pata michezo mbalimbali kutoka Chuo Kikuu Cha Ardhi (ARU)



Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) Dar es salaam wakicheza kikapu katika viwanja vya chuoni hapo juzi (Picha na Evance Ng’ingo)

Timu mbalimbali zilijitokeza pia kushiriki michezo na wanafunzi hao wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) Dar es salaam wakicheza kikapu katika viwanja vya chuoni hapo juzi (Picha na Evance Ng’ingo)

Wanafunzi wanawake wa  Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) Dar es salaam wakicheza mpira wa pete juzi katika viwanja vya michezo vilivyopo chuoni  hapo juzi

Inshu kamili
Nyakati za jioni kunakuwa na wanafunzi mbalimbali ambao wanakuwa wanashiriki michezo mbalimbali chuoni hapo baada ya kumaliza masomo yao, hiyo ni hatua nzuri kwa wanafunzi kujifunza michezo pia inaongeza hamasa ya kusoma