Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, June 9, 2013

Taasisi ya Hassan Maajar yakabidhi madawati 321 mkoani Rukwa

Furaha ilioje

Shafi Majaar akitoa hotuba yake

Wakaimba nyimbo za shukrani



Manyanya akizindua madawati kwa kuandika

Zena Majaar Tenga ambae ni Mkurugenzi wa HMT akisoma risala yake

Picha ya pamoja

Wanafunzi wakifurahia msaada huo

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitoa shukrani zake


 Sharif Maajar akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stela Manyanya uthibitisho wa utoaji wa madawati hayo (asante Hamza Temba wa ofisi ya RC Rukwa). 

Habari kwa hisani ya HMT 
Taasisi ya Hassan Maajar Trust imetoa msaada wa madawati 321 katika shule nane (8) katika Halmashauri nne (4) za mkoa wa Rukwa yatakayokalisha wanafunzi 963. 

Madawati hayo yalikabidhiwa katika hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi ya Kansense, iliyoko Wilaya ya Sumbawanga. Bi Zena M Tenga pamoja Bwana Shariff Maajar, kwa niaba ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust walikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Engineer Stella Manyanya. 


Shule ziliopokea madawati hayo ni: Sopa na Mkowe (Halmashauri ya Kalambo), Korogwe na Wampembe (Halmashauri ya Nkasi), Maleza na Mleche (Halsmashauri Sumbawanga) na  shule Chipu na Kasense (Manispaa Sumbawanga). 


“"Elimu ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu kwa hiyo sisi tunafurahia msaada kama huu," alisema Mh. Mhandisi Stella Manyanya, Mkuu wa mkoa Rukwa. "Watoto wetu wanakabiliwa na changamoto nyingi na hili la ukosefu wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kweli lina athiri maendeleo yao. Kwa hivyo natoa shukurni nyingi kwa Taasisi ya Hassan Maajar Trust na kazi yao hii ya kijamii ni ya kupongezwa ”, aliongeza. 


Huu ni msaada wa nne chini wa mradi wa Hassan Maajar Trust wa “Dawati Kwa Kila Mtoto”, (A Desk For Every Child) na mkoa wa Rukwa ni mkoa wa nne kati ya mitano itakayonufaika kwa msaada inyatolewa na Hassan Maajar Trust kwa kutumia fedha zilizopatikana na michango iliyotolewa kufuatia kampeni iliyoanzishwa Desemba 2011.

 Hadi sasa Hassan Maajar Trust imekabidhi jumla ya madawati 1,515 kati ya madawati 1,764; Njombe (680), Singida (264), Mwanza (250) na sasa Rukwa (321). Mkoa utaofwatia ni Lindi (250). Garama za madawati haya ya mkoa wa Rukwa ni jumla ya Tsh 22,500,000. 

Hassan Maajar Trust pia imeshirikiana na African Barrick Gold (ABG) kupitia Mfuko wao wa Maendeleo  kutoa madawati 2,360 kwa shule 15 katika Wilaya ya Kahama, Shinyanga yenye thamani ya dola 300,000 (takribani shilingi milioni 480)


"Sisi kama Hassan Maajar Trust tuna malengo ya kuboresha mazingira ya kujifunza katika shule nchini Tanzania. Kwa kupitia kampeni yetu ya 'Dawati Kwa Kila Mtoto' tunatarajia kufikia shule nyingi iwezekanavyo, "alisema Zena M Tenga Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust," Na pia tunaamini kwamba mtu yeyote anaweza kuchangia katika hii  kampeni yetu na kuchangia maendeleo ya shule zetu kwa njia ya mchango wowote mkubwa au ndogo ", aliongeza.

1 comments: