Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, September 30, 2012

Hongereni mliomaliza kidato cha nne

Hawa ni wahitimu wa kidato cha nne katika sekondari ya Pugu ambao wamewezeshwa na kuthibitisha kuwa wanaweza kwa hiyo ni vema kuwaendeleza wenye ulemavu ili waweze fikia malengo yao

Hekaheka za kujiandaa na mitihani ya form four

Monday, September 24, 2012

Vijana hawa wameandaliwa na kufundishwa vema na nido wanatumia elimu hiyo katika kubiridisha kwa sarakasi

 Wasanii wa Kikundi cha Shada, wakifanya onyesho la sarakasi katika ufunguzi wa tamasha la kimataifa la Sanaa Bagamoyo. Tamasha hilo limefunguuliwa rasmi Jumatatu na litaendelea kwa siku tano hadi Jumamosi ijayo

 Moja kati ya mambo yaliyokuwa kivutio kikubwa ni jinsi watoto hao walivyoonyesha umahiri katika kuruka kwenye maringi.

Wasanii wa kundi la Jeshi wakifanya onyesho la Mzingaombwe katika Tamasha la Sanaa la Bagamoyo

Sunday, September 23, 2012

Uzembe unavyoweza sababisha ajali za barabarani

Tela la Roli hili lilikutwa limepinduka katika barabara ya Tabata Relini hii inatokana na uzembe wa kutozingatia elimu ya usalama wa barabarani
                                                      Hapa ni nyuma ya tela hilo

Thursday, September 20, 2012

MCHANGO WAKO UNAHITAJIKA HMT KUSAIDIA SHULE YA MSINGI YA KIVULE

Mkoani Dar es Salaam, wilaya ya Ilala kuna shule ya Msingi iitwayo Kivule ambayo ina jumla ya wanafunzi 3,585; madarasa 11, waalimu 30, na madawati 300. (Kwa mujibu wa takwimu zake za Januari 2012). 

Kutokana na wingi wa wanafunzi wa shule hiyo kulinganisha na rasilimali zake kama madawati, waalimu na madarasa; Mwalimu mkuu wa shule hiyo Grace Ndalo alilazimika kuwagawa wanafunzi hao katika shifti mbili yaani wale wanakuja shuleni asubuhi mpaka mchana, na wanaokuja shuleni mchana hadi jioni. Hata hivyo, mwalimu mkuu huyo hakuishia hapo, alienda kuililia Wizara ya Elimu na Ufundi Stadi ambao waliahidi kuongeza madarasa 7 hapo shuleni.

Mwalimu grace hakuishia hapo, alifika katika ofisi zetu na kuomba msaada zaidi kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. Alieleza kwamba, matatizo makubwa mawili yanayoishambulia shule ya msingi Kivule ni:
1.      ukosefu wa madawati ya kutosha (asilimia kubwa ya wanafunzi wakiwa wanakaa chini)
2.      Mila potofu zinazozunguka maeneo ya shule hiyo.

Hivyo mwalimu mkuu huyo ameomba misaada ifuatayo:
1.      Madawati 895 ambapo dawati moja ni shiligi 90,000/= kwa hapa Dar es Salaam
2.     
          Kiasi cha fedha tasilimu 200,000/= kila mwezi kwa ajili ya kuwalipa waalimu ambao watajitolea muda wao kuwaelimisha wazazi wa wanafunzi hao juu ya umuhimu wa elimu; pamoja na kuwafundisha kusoma, kuandika, na kuhesabu.

Akifafanua juu ya tatizo la madawati alisema kuwa, kwa sasa dawati moja linakaliwa na wanafunzi 5-6 (ambapo kwaida dawati moja linakaliwa na wanafunzi 3) na bado wanafunzi wengine wanakaa chini.   
Akiendelea zaidi kufafanua juu ya tatizo la pili alisema kuwa, jamii inayoizunguka shule hiyo inaamini sana katika ndoa za mapema ambapo wanafunzi hususani wa kike wakilazimishwa kuolewa au kupendelea kuolewa na kuoa baada ya kutoka jandoni ama unyagoni. 

Vilevile, jamii hiyo hawatambui juu ya uzazi wa mpango, kupelekea mwanamume mmoja kuwa na hadi watoto 30 na wanawake tofauti (hili linachangia uongezekaji wa wanafunzi shuleni hapo wakati rasilimali ni chache). Pamoja na hayo yote, wazazi wa wanafunzi hao hawaipi Elimu kipaumbele, hivyo msaada unahitajika kuwakomboa wazazi hao pia katika fikra potofu ili waanze kusisitizia watoto wao umuhimu wa elimu kwani ndio ufunguo wa maisha
.   
 Hasaan Majaar Trust ingependa kushirikiana na wewe katika kuisaidia shule ya msingi Kivule. Kitakachopatikana kitapelekwa shuleni hapo na wewe kama mfadhili wa namna moja hadi nyingine utakuwa pamoja nasi kukabidhi rasilimali hizo.
Wasiliana nasi kupitia
·         simu namba:  +255 767 699932 / +255 718528009 / +255 685 353566 / +255 22 2775116
·         baruapepe:       info@hassanmaajartrust.org


wanafunzi wa darasa la saba na mitihani





Wanafunzi wa darsa la saba wamemaliza mitihani yao hii leo huku wengine wakiwa wamefanya mtihani huo wakiwa katika hali mbaya ya kimsaada kwa kuwa wlaikuwa hawana hata penseli au peni za kufanyia mtihani huo.
 

Tuesday, September 18, 2012

Mengi atoa somo la biashara kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini


 
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo Vya Habari Nchini            (MOAT) Regnard Mengi akipokea hati ya usajili ya Chama Cha Kuweka na Kukopa cha Wahariri, Wahariri Development Saccos kutoka kwa mwenyekiti  wa saccos hiyo Gogfrey Shogolo anayeshuhudia katikati ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absolom Kibanda na kushoto ni ofisa wa  wa Ushirika kutoka Manispaa ya Ilala Stanslaus Mwansao (Picha na Evance Ng’ingo)




WAHARIRI pamoja na Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kutambua kuwa ni jukumu lao kuinua kipato chao na hakuna mtu mwingine mwenye jukumu hilo.

Wito huo ulitolewa juzi na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT)  Reginard Mengi katika viwanja vya Karimjee wakati akizindua Chama cha Kuweka na Kukopa cha Wahariri, Wahariri Development Saccos.

Mengi alisema kuwa iwpao wahariri wakijiendeleza kimaisha wanaweza kuwa huru katika kufanya maamuzi yao wenyewe kulingana na maadili ya kazi zao bila kurubuniwa na watu wengine. 

Alisema kuwa Saccos ni njia mojawapo ya kuinua kipato chao hivyo aliwataka kuitumia vema kwa kuchukua mikopo yenye malengo ya kibiashara na ambayo wanaweza kuirudisha kwa muda unaotakiwa.

Pia aliwataka kuepuka migogoro ambayo inaweza kujitokeza kutokana na saccos hiyo huku akiwataka waitumie  kama chombo cha ukombozi wa maisha yao kwa kuimarisha wazo lao la biashara kabla ya kuchukua mkopo.

“ Kwanza ningependa muelewe kuwa pesa haina sura, hapa nikiwa na maana kuwa katika kuitafuta hakuna kuwa na mzaha nayo hakuna suala la aibu wala suala la kuogopa kuisaka” alisema Mengi.

“Natambua kuwa mtu huwezi kuwa mhariri mzuri huku ukikabiliwa na na shida mbalimbali,  sasa basi msikubali kuishia kupewa tu sifa kuwa nyinyi ni wahariri wazuri huku mkiwa mnakabiliwa na shida mbalimbali” aliongeza Mengi.

Aliahidi kuisaidia Saccos hiyo kwa kila hali ili iweze kutimiza ndoto yake na aliwaomba wahariri kukutana nae punde watakapokuwa wanahitaji msaada wake.

 Naye Mwenyekiti wa saccos hiyo Godfrey Shogolo alisema kuwa saccos hiyo ambayo ni kwa ajili ya wahariri inalenga kuinua maisha ya wahariri hao na kuongeza kuwa mchango wa kujiunga nayo ni shilingi 400,000/=
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Sunday, September 16, 2012

Mazingira ambayo yahitaji na pia yanaihathiri elimu nchini

 Pasipokuwa na elimu ya kutosha kwa waendesha bodaboda hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa usalama wao kwa kuwa wengi wao watazidi kufa siku hadi siku.
Hapa unaweza kujiuliza kuwa mahala ambapo kuna shida kubwa ya maji kama hii je wanafunzi wanaweza kuwahi kwenda shule kuendelea na masomo yao, picha hii inatoa habari kuwa mahala penye shida ya maji basi hata maendeleo yao ya elimu nayo pia yanaweza kuwa ya shida pia

Ay afanya ziara ya kimafunzo katika ofisi za magazeti ya serikali ya Habari leo na Daily news

Akisalimiana na mmoja kati ya waandishi waandamizi wa gazeti la habari leo

 Akipeana hai na mwandishi wa habari wa Daily News online wakati alipotembelea ofisi ya magazeti ya serikali
Hapa akisalimiana na wasanifu kurasa wa gazeti la habarileo alipotembelea banda lao

Saturday, September 15, 2012

Zantel kuwaendeleza kielimu wachezaji wa African Lyon

Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel imetangaza nia ya kusaidia timu ya soka ya African Lyon ikiwa pamoja na kusaidia kuendeleza elimu kwa vijana waliopo katika Academy ya timu hiyo kijana huyu pichani atasaidiwa kwenda kusoma nchini Marekani

Mmoja kati ya maofisa wa Zantel, Natasha, akitoa zawadi kwa washiriki waliohudhuria hafla hiyo

Wednesday, September 12, 2012

Wakufunzi wa makocha wapewa somo

Wakufunzi wa makocha waliopo hapa jijini kwa semina ya siku nne wakipewa somo na mwalimu wao katika viwanja vya Karume jana

Mamis kinondoni wazidi kujifua, wapewa elimu ya kujiamini

Mwandaaji wa Miss Kinondoni Vivian Sirikwa akiwafunda washiriki wa shindano hilo ambalo litafanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa Kasa uliopo Mikocheni

Monday, September 10, 2012

Rais Kikwete azindua chuo cha kijeshi nchini kilichopo Kunduchi Dar es salaam

Rais Jakay Kikwete akipena mkono nma Meja Jenrali Charles Makalala mara baada ya kumkabidhi funguo ikiwa ni inshara ya ufunguzi wa chuo hicho kilichopom Kunduchi, Dar es salaam

Rais Kikwete akiwa na wakuu mbalimbali wa chuo hicho mara baada ya kukizindua leo

Hapa akikizindua rasmi chuo hicho jana ambapo alittoa wito kuwa kinatakiwa kuendeleza elimu ya kijeshi na kuwa mfano wa kuigwa ndani na nje ya bara la Afrika

Sunday, September 9, 2012

Msaada huu kwa watoto wenye ulemavu utawasaidia kusoma vema

wheelchairs znz Ally Sihaji and son Hilali Silaji 13 years old

Salama Zaharani (10) na wazazi wake

Sadra Hassan (9)

Viti 30 maalum kwa watoto wenye ulemavu vimetolewa kwa watoto wenye ulemavu Zanzibar leo. Viti hivyo vimeagizwana kampuni ya Uchimbaji na utafiti wa Madini ya Montero yenye makazi yake Canada na washirika wake wa Tanzania Kampuni ya madini ya Wigu Hill. Viti hivi vimetengenezwa maalum kwa ajili ya watoto walemavu na shirika lisilo la kiserikali  ‘’Wheel chairs for Kids “ huko Australia.

“Tunafurahia kuweza  kupanua wigu wa misaada yetu kwa watoto kwenye kisiwa cha Zanzibar, kama sehemu yetu ya kusaidia jamii. Hivi viti vya matairi mawili  vitaboresha maisha yao na ya wazazi na walezi wao. Siku ya leo inaweka historia ya mkakati ambao, baadae viti vya walemavu vingine 130 vitasambazwa kwa watoto wa mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro’’alisema Grant Pierce Meneja Mkuu wa Montero Tanzania.

Utoaji wa viti hivyo ulifanyika rasmi katika hospitali ya Mnazi mmoja kwa ushirikiano wa klabu ya Rotary Zanzibar ambayo ilitafuta wapokeaji na kuandaa tukio hilo.

‘’Rotary inajihusisha na mipango mbalimbali ya kijamii huku Zanzibar na ni wazi kwamba watoto wenye ulemavu wanamahitaji zaidi kulio vikundi vingine vyote katika jamii yetu. Hii ni siku ya furaha tele kwao na kwetu.”Alisema mwanachama wa RotaryStephi Said.

Viti hivi vya walemavu vimetengenezwa kwa ustadi zaidi na vinaweza kutosheleza mahitaji ya kila mtoto kulingana na ulemavu wake.

Kuhusu kampuni  ya madini ya Montero
Kampuni ya uchimbaji wana utafiti ya madini ya Montero ni kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa madini ya Rare Earth Elements (REE) na inaendesha shughuli za Mkoa wa Morogoro kupitia washirika wake wa Wigu Hill. Pia ina maeno mengine Tanzania,Afrika Kusini na Quebec Canada

Kuhusu Wheelchairs for Kids
Klabu ya Rotary huko Australia Magharibi ilianzisha mkakati wa wheelchairs for kids mwaka1998,viti hivi maalum vinatengenezwa na wafanyakazi wastaafu wanaojitolea. Mpaka sasa ina nguvukazi ya watu wapatao 100, wengi wakiwa wastaafu, wanotengeneza,wanaohakiki viwango,na kupanga na kupakia kwenye maboksi, viti hivi.Wafanyakazi wengine wa kujitolea wanatengeneza foronya na zawadi ndogo ndogo  zinazoambatanishwa na viti hivi, kwa ajili ya wapokeaji.

 
 




Saturday, September 8, 2012

Wanafunzi washiriki mashindano ya riadha ya taifa

Wawakilshi wa Umiseta wakiwawakilishi wanafunzi katika mashindano ya taifa ya raidha yanayoendelea katiak uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ambapo kwa mwaka huu mashindano hayo yametoa nafasi kwa wanafunzi kuwakilishwa na wenzao hao katika mashindano hayo ya taifa

Friday, September 7, 2012

Elimu ya michezo ikitolewa mapema inasaidia kujenga na kuinua vipaji

Watoto hawa walikutwa wakijifunza kucheza mchezo wa Tennis, mafunzo kama haya yanapotolewa mapema yanasaidia kuwajengea uwezo na kujua vipaji vyao mapema.

Ni vema wazazi wakawa wanawapeleka watoto wao katika viwanja kama hivi kujifunza michezo mbalimbali

Namna ya kujifunza kucheza gofu

Wasichana hawa walikutwa na mpiga picha blog hii wakijifunza namna ya kupiga vizuri mpira wa gofu

Tuesday, September 4, 2012

Mengi ya kujifunza katika maonesho ya siku ya wakandarasi Mlimani City

Joan Kayamba aliyekaa akijadiliana jambo na mwenzake wakati wa maonesho ya siku ya wakandarasi yaliyofanyika jana katiak ukumbi wa Karimjee

Joana Kayamba na mwenzake wakitoa mafunzo ya matumizi ya marumaru zao katika maonesho hayo

Polis wazingatie mafunzo yao kuhusiana na masuala ya haki za binadamu




Huyu askari alimwelekezea mtutu tumboni na kumsambaratisha marehemu. Ni wazi watu wa Iringa wanamfahamu askari huyu.