Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, July 29, 2014

Mzazi amlamba bakora mwalimu, hii ni mbaya sana

Walimu wawili wa shule ya Msingi Nzogimlole wilayani Nzega Mkoani Tabora wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kupigwa na kujeruhiwa vibaya na mzazi mmoja aliyetambulika kwa jina la Selemani Juma baada ya walimu hao kumurudisha shule mwanafunzi Shaabani Mziku kutokana na kuchanika kwa sare yake ya shule (bukta). Mwandishi wa habari hii alifika katika shule hiyo ya Msingi Nzogimlole na kuzungumza na mwlimu mkuu msaidizi Emmanuel Josephat alisema kuwa mwanafunzi huyo Shaaban Maziku aneyesoma Darasa la pili aliambiwa na mwalimu Richard Zakari aliyekuwa akifundisha katika Darasa hilo kum rudisha nyumbani kutokana na sare yake Bukta kuchani hadi kupelekea sehem zake za siri kuonekana. Akizungumza kwa simanzi na majonzi mwalimu huyo mkuu msaidizi alisema kuwa motto huyo alifika nyumbani na kumueleza Baba yake Selemani Juma kuwa mwalimu Rchard alichana bukta hiyo na kumwambia akamwambie Baba yake aishone. Alisema kitendo hicho kilimfanya mzazi huyo kufika shuleni na kuanza kutoa lugha chafu shuleni hapo dhidi ya mwalimu na hatimaye kuanza kutoa kipigo kwa waalimu hao hali iliyopelekea wananafunzi waliokuwa madarasani kutoka na kuanza kulia kutokana na kipigo hicho ambacho walikuwa wakipigwa waalimu hao. Akitumia mawe kurushakwa walimu hao na baadae kutumia fimbo ambayo ilifahamika kwa jina fito iliyotumika kuwa chapa waalimu hao sehemu mbalimbali katika miili yao hadi kusababisha majeraha. ‘’Mwalimu hana kosa kwani mtoto kaptura yake ilikuwa imechanika vibaya sana hali iliyopelekea sehem zake za siri kuonekana sasa hatupaswi tuwaache hivi watoto alimwambia akamwambie baba yake aishone ile sare lakini mambo hayakuwa hivyo’’alisema mwalimu. Akizungumza baada ya kutoka katika Hospitali ya kijiji hicho mwalimu Richard Zkaria alisema kuwa hali yake inaendelea vizuri na kuongeza kuwa sababu ya kupigwa na mzazi huyo haijui kutokana na jukumu alilolifanya ni la kawaida Alisema kuwa alipigwa yeye na mwalimu mwenzake Elias Kafiku ambaye alikuwa akiamua ugomvi huo kwa mazazi huyo na kumtaka aingie ofisni ili suala hilo waweze kulizungumza kiofisi na kufikia muafaka hata hivyo mwalimu huyo alipigwa. Mtendaji wa kijiji hicho ………alisema kuwa tukio hilo limetokea July 25 mwaka huu katika shule hiyo ambapo waalimu wa wili walipigwa na mzazi kisha kujeruhiwa vibaya na mzazi huyo. Alisema kuwa jitihadi mbalimbali zakumkamata mzazi huyo zilifanyika baada ya migambo wa kijiji jirani kumkata kisha kupelekwa katika kituo kidogo cha polis cha bukene ili hatua mbalimbali za kisheria ziweze kushika mkondo wake. ‘’Nawaomba wazazi na walezi wabadilike wajari elimu pia matukio kama haya wafuate taratibu sahihi za kiofisi kwani kujichukulia maamuzi kuna madhara yake’’alisema mtendaji Wakizungumza kwa muda tofauti wananchi wa kijiji hicho cha Nzogimlole walisema kuwa kitendo hicho kilichofanywa na mzazi huyo sikizuri kutokana na kujichukulia sheria mkononi hali ambayo ilipelekea uzalilishaji mbele ya waalimu pamoja na kuwapatia hofu waalimu wengine wa shule hiyo. Mwalimu Elizabert Kafurila alisema tukio hilo limewatia hofu katika utendaji kazi kutokana na wazazi kuingilia majukumu ya waalimu na kuongeza kuwa wazazi wanapaswa kujirekebisha na nkufuata taratibu maalumu za Ofisi. Kamanda wa polisi mkoani wa tabora Suzani Kaganda alisema kwamba mzazi huyo nashikiliwa kwa tuhuma za kupinga na kujeruhi vibaya na hatarifikishwa mahakamani baada ya upepelezi kukamilika. Mwisho.

Wednesday, July 16, 2014

Isome taarifa ya matokeo kidato cha sita hapa,

   
BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA), imetangaza matokeo ya Kidato cha Sita uliofanyika kati ya Mei 5 hadi 21, 2014 ufaulu umeongezeka kwa asilimia 8.13 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.

Kwa mwaka huu, wanafunzi 38,905 kati watahiniwa 40,695 ikiwa ni asilimia 95.98. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu walikuwa ni 44,366 sawa na asilimia 87.85.

Kaimu Katibu Mkuu wa NECTA, Dk Charles Msonde alisema wanafunzi waliofaulu wasichana ni 12,080 sawa na asilimia 97.66 wakati wavulana ni 26,825 sawa na asilimia 95.25.

Alisema watahiniwa wa shule walioaulu ni wanafunzi 34,645 sawa na asilimia 98.26 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa ni 10,900 ambayo ni asilimia 99.2 na wavulana 23,45 sawa na asilimia 97.84. Mwaka 2013 watahiniwa 40,242 sawa a asilimia 93.92 ya watahiniwa wa shule waliauu mtihani huo.

" Mtahiniwa atahesabiwa kuwa amefaulu somo endapo atakuwa amepata angalau gredi D (alama 30) katika somo husika. Hivyo, kiwango cha juu cha ufaulu katika somo ni Gredi A ambapo kiwango cha chini cha ufaulu (pass) katika somo ni Gredi D. Ufaulu katika gredi A, B+, B na C utakuwa ni ‘Principal Pass’"

" Daraja la Kwanza limepangwa kwa poiti 3-7, la Pili 8-9, TAtu 10-13 na Daraja la Nne mtahiniwa watakuwa wamaaulu kwa kuwa na angalau D mbili au principal pass moja na aliyepata DAraja Siuri ni yule aliyepata ufaulu chini ya D mbili." alisema. Uzito wa alama katika Gredi; A=1, B+= 2, B=3, C=4, D=5, E=6 na F=7.

Alisema watahiniwa wa Kujitegemea waliofaulu ni 4,260 sawa na asilimia 80.73.  ya watahiniwa 5,27 waliofanya mtihani. Mwaka 2013 Watahiniwa wa Kujitegemea 4,124 sawa na asilimia 53.87 walifaulu mtihani huo.

Msonde alisema Baraza limezuia matokeo ya watahiniwa 150 wa shule   ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa, watahiniwa tisa waliopata matatizo ya kiafya.

"Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya mtihani kwa masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa katika Mtihani wa Kidato cha Sita Mei, 2015.

Alisema watahiniwa 29 wa shule  ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote. Watahiniwa husika  wamepewa fursa ya  kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita Mei, 2015.

Msonde alisema Baraza limefuta matokeo yote ya watahiniwa wawili waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani.

Ubora wa ufaulu
Msonde alisema ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata Watahiniwa wa Shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 30,225 sawa na asilimia 85.73 wamefaulu katika madaraja I - III wakiwemo wasichana 9,954 sawa na asilimia 90.59 na wavulana 20,271 sawa na asilimia 83.53.
Daraja kwa Kwanza ni wanafunzi 3,773, wavulana 2,232 na wasichana 1,541, Daraja la Pili ni wanafunzi 9,631ikiwa wavulana ni 6,179 na wasichana 3,452.

 Daraja la Tatu ni wanafunzi 16,821 ikiwa wavuana ni 11,860 na wasichana 4,961, Daraja la IV: wanafunzi 4,420 ikiwa ni wavulana 3,474 na wachana 946 na Daraja 0: wanafunzi 612, wavulana wakiwa ni 524 na wasichana 88.

Ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule
Msonde alisema ufaulu wa watahiniwa wa shule katika masomo  yote (14) ya msingi umepanda ikilinganishwa na mwaka 2013. Ufaulu wa juu kabisa ni ule wa somo la Kiswahili ambao ni asilimia 99.88 ya watahiniwa wote wa Shule waliofanya somo hilo  wamefaulu.

Alisema ufaulu katika masomo ya Sayansi (Physics, Chemistry, Biology na Advanced Mathematics) umeendelea  kuimarika kwa kulinganisha na ufaulu wa masomo hayo mwaka 2013.

Shule zilizfanya vizuri
Msonde alisema  wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha Wastani wa Pointi (Grade Point Average – GPA) na mchanganuo wa upangaji wa shule zilizofanya vizuri umezingatia shule zenye idadi ya watahiniwa wasiopungua 30.

Alitaja shule hizo kuwa ni Igowole(Iringa), Feza Boys(Dar), Kisimiri (Arusha), Iwawa (Njombe), Kibaha(Pwani), Marian Girls(Pwani) Nangwa(Manyara), Utawa(Mbeya), Kibondo(Kigoma) na Kawawa (Iringa).

Shule kumi za mwisho 
Msonde alizitaja shule hizo kuwa ni Ben Bella( Unguja), Fidel Castro(Pemba), Tambaza(Dar), Muheza High School(Tanga), Mazizini(Unguja), Mtwara Technical(Mtwara), Iyunga Technical(Mbeya), AL-Falaah Muslim(Unguja), Kaliua (Tabora) na Osward Mang'ombe( Mara).
Watahiniwa walioanya vizuri

Msonde alisema watahiniwa waliofanya vizuri zaidi wamepatikana kwa kuangalia wastani wa Pointi (GPA) kwenye masomo ya tahasusi pamoja na wastani wa alama za jumla walizopata.

Alitaja majina ya wanafunzi hao ni Isaack Shayo (St. Joseph Cathedral), Doris Atieno Noah(Marian Girls), Innocent Sabbas Yusufu(Feza Boys'), Placid Ezekiel Pius(Moshi), Benni Shayo(Ilboru), Abubakar Juma(Mzumbe), Mwaminimungu Christopher(Tabora Boys), Chigulu Japhaly(Mzumbe), Hussein Parpia (AL-Muntazir Islamic Seminary) na Ramadhani Ally Msangi(Feza Boys).

Watahiniwa kumi bora kwa masomo ya biashara ni Jovina Leonidas(Nganza), Nestory Makendi (Kibaha), Imma Anyandwile(Umbwe), Thersia Marwa na Grace Chelele(Loyola), Betria Rugila(Baobab), Jaqueline Kalinga(Weruweru), Tajiel Kitojo( Arusha), Shiriya Ramaiya(Shaaban Robert) na Mwanaid Mwazema(Weruweru)

Watahiniwa kumi bora wa masomo ya Lugha na Sanaa ni Lisa Mimbi(St. Mary Goreti), Rosalyna Tandau( Marian Girls), Joseph Ngobya(St. Joseph Cathedral), Aneth Mtenga na Idda Lawenja( Marian Girls), Edna Mwankenja( Kisimiri), Catherine Kiiza( St. Mary Mazinde Juu), Nancy Adonswai(Mwika), Mohamed Salmin(Mwanza) na Idrisa Hamisi( Mwembetogwa).

Sunday, July 6, 2014

Angalia video ya wanafunzi hawa wa Tusiime wakiimba

Shule hiyo iliyopo Tabata Ilala, Dar es salaam sio nzuri tu kimasomo bali hata katika kuinua vipaji vya wanafunzi pia

Tuesday, July 1, 2014

Sekondari ya Mtakuja yapewa vitabu kutoka Bahari Rotary

Mkuu wa Sekondari ya Mtakuja, Beatrice Mhina Ramadhan akiwa na Kamusi zake (Dictionary) ofisini kwake baada ya kukabidhiwana Bahari Rotary
Mkuu wa Sekondari ya Mtakuja, Beatrice Mhina Ramadhan(kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Wilnfred Haule katikati pamoja na mmoja kati ya walimu wa shule hiyo baada ya kupewa msaada wa vitabu kutoka Bahari Rotary.