Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, March 23, 2016

Tigo yatoa madawati 50 kwa shule 10 za Kinondoni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akihutubia wananchi na wanafunzi katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda(kulia) na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (wa pili kulia),wakiwa wameketi kwenye moja ya madawati 500 yalikabidhiwa na kampuni ya Tigo kwa shule za msingi 10 jijini Dar es Salaam jana. Wengine katika picha  ni Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani , Goodluck Charles (wa tatu kulia)na Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Dkt. Aziz Msuya(kushoto). Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.

Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.
 Mwanafunzi Saidat Proches akishukuru mara baada ya makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akiongea na walimu na wananchi mara baada  makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam

Sherehe ya makabidhiano ilifanyika leo shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga


Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez akiteta jambo na  Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani , Goodluck Charles katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam

Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga
 Wanafunzi wa shule ya msingi kawawa wakishuhudia makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga




Machi 22 2016 Dar es Salaam: Kampuni ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi nchini.

Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo katika kata ya Mabibo katika manispaa ya Kinondoni, Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo nchini.

“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari, wahandisi na wengineo, "amesema Gutierrez.

Gutierrez amesema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya Iringa na Morogoro na kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini siku za zijazo.

Makabidhiano yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye alisema madawati hayo 500 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Dar es Salaam na kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.

“Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa Dar es Salaam. Ni dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 500 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao katika mazingira bora zaidi,” alisema Makonda.

Tigo yatenga Milioni 300 kuwasomesha wanafunzi

Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa wa jumla ya shilingi million 300 mapema leo  jijini Dar Es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula na kushoto ni Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael.

Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) katikati ni Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez,na kushoto ni Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael. wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa wa jumla ya shilingi million 300 mapema leo  jijini Dar Es Salaam.

Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez  akipeana mkono na Mmoja wa wanafunzi waliopata udhamini wa tigo  Carolyne Paul, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Udsm shahada ya uhandisi wa kompyuta na teknolojia ya habari   wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa wa jumla ya shilingi million 300 mapema leo  jijini Dar Es Salaam.

Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez(katikati),Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula(kulia) na Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael(kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaochukua mafunzo ya Tehama mara baada ya kampuni ya Tigo kutangaza udhamini wa jumla ya shilingi million 300 kwa wanachuo hao   mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Tigo Kijitonyama jijini Dar Es Salaam.
Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez(katikati) akipata "SELFIE"  na ,Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula  na Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael pamoja na wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaochukua mafunzo ya Tehama mara baada ya kampuni ya Tigo kutangaza udhamini wa jumla ya shilingi million 300 kwa wanachuo hao   mapema leo katika ofisi za makao makuu ya Tigo Kijitonyama jijini Dar Es Salaam   .



Dar es Salaam Machi 23, 2016 Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) leo wametangaza kudhamini wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa kwa jumla ya shilingi million 310.
Akitangaza udhamini huo jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema fedha hizo zitagharamia ada ya chuo, gharama za kufanya utafiti, malazi na chakula kwa kipindi cha miaka minne cha masomo ya Tehama kwa kila mwanafunzi.
Gutierrez amesema udhamini huo unaowalenga kuwasiadia vijana wenye vipaji katika taaluma ya Tehama kutimiza ndoto zao za kimaisha ni sehemu ya sera ya kampuni hiyo ya mawasiliano ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kukuza sekta ya tehama na kuleta maendeleo nchini.

“Tunaamini kupitia udhamini huu kampuni yetu,  kwa kushirikiana na DTBi, inatoa mchango wake katika kujenga kizazi kijacho cha mabingwa katika sekta ya Tehama ambao watakuwa nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa nchi hii,”Gutierrez amesema akiongeza kwamba tayari kuna makubaliano kati ya Tigo na DTBi unaowapa wanafunzi kutoka DTBi fursa ya kubuni bidhaa mbalimbali vya Tehama ambavyo hutumiwa na Tigo kibiashara na mapato kugawanywa kwa wadau wote.  

 Wanafunzi tisa waliobahatika kupata udhamini wa Tigo ni Erickson Muyungi (UDSM), Fatma Moshi (UDSM), Caroline Paul (UDSM), Michael Lunyungu (UDOM), Robert Charles (UDOM), Isack Kipako (UDOM), Jacqueline Dismas (UDSM), Jumanne R. Mtambalike (IFM) na Joel Mtebe (UDSM).

Akizingumzia zaidi kuhusu mkataba huo kati ya Tigo na DTBi, Mkurugenzi huyo wa Tigo amesema: “mbali na udhamini tunaoutoa kwa wanafunzi wa Tehama tuna mradi wa pamoja uitwao ‘Project Digitize’ ambao umewawezesha wanaTehama chipukizi kuanzisha kampuni zao kuipitia ubunifu wao na ambao wanapata msaada kutoka Tigo katika kuendeleza miradi yao. Hadi leo kuna wanatehama watatu wanaosaidiwa na Tigo kupitia mpango na ambao bidhaa pindi bidhaa zao zitakapoanza kutumika kibiashara, watafaidika kutokana na mgawanyo wa mapato..”
 Naye Mkurugenzi Mtendaji wa DTBi Mhandisi George Mulamula kwa upande wake amesema üshirikiano na Tigo umetoa fursa na njia za kibunifu kwa wanafunzi wa DTBi kupata elimu, kujenga uwezo wao wa Tehama ambavyo vitawasaidia kuonyesha vipaji vyao katika fani hii ndani na nje ya nchi.

Mulamula aliongeza kusema kwamba: “DTBi’s ina malengo ya kuwahamasisha vijana wakiwemo wanawake kujenga tabia za kuwa wajasiriamali Tehama ili kusaidia kukuza sekta binafsi na kuongeza makusanyo ya kodi nchini. Katika kutekeleza azma hii, Tigo imetoa mchango mkubwa kwa kuwawezesha wajasiriamali wetu kufikia ndoto zao za uzalishaji mali, kusaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii, kuleta nafasi mpya za ajira yote haya yakiwa ni vielelezo vya jinsi ambavyo tehama inaweza kusaidia kukuza pato la taifa.”