Help Children
Love them
Saidia Watoto

Saturday, May 31, 2014

Bahari Rotary Club kusaidia kituo cha kulelea wasichana cha Kurasini

Mchezaji wa mchezo wa gofu kutoka Bahari Rotary Club Shakil Jaftes, akicheza gofu wakati wa uzinduzi wa michuano ya gofu kuchangia

Mchezaji wa mchezo wa gofu kutoka Bahari Rotary Club Kishan Dhebar, akicheza gofu wakati wa uzinduzi wa michuano ya gofu kuchangia fedha za kusaidia watoto wa kike wanaolelewa kwenye kituo cha Kurasini
Mbili

Group Picha

Mahojiano yakiendelea

Sister kutoka kituo cha Kurasini akizungumza na waandishi wa habari

Mchezaji wa mchezo wa gofu kutoka Bahari Rotary Club Hasnain Rahim akicheza gofu wakati wa uzinduzi wa michuano ya gofu kuchangia fedha za kusaidia watoto wa kike wanaolelewa kwenye kituo cha Kurasini

GENIUS CAP 2014 yapata washindi wake

Washindi walioingia  hatua ya tatu bora katika mashindano ya GENIUS CAP 2014, kutoka kulia ni mshindi wa kwanza John Reginald Bugeraha(13), mshindi wa pili Patrick Frank John(14) wote kutoka shule ya msingi Mount Everest, na mshindi wa tatu Samira Yahya Kishasha(12) kutoka Shule ya Msingi Anazak wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mshindi wa kwanza: Afisa Elimu Mkuu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Salum Salum akimkabidhi cheti na hundi ya Dola za Kimarekani 600 (600$)Mshindi wa kwanza wa mashindano ya GENIUS CAP 2014 John Reginald Bugeraha(13) kutoka Shule ya Msingi Mount Everest mara baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo.

Saturday, May 24, 2014

Mwanafunzi usikate tamaa kamwe

Nimependa sana namna ambavyo kijana huyu alionekana akijiamini kwa kile alichokuwa akikitafuta na hata alipokikosa anaonekana kutokata tamaa. Na Msiogoep kujaribu kamwe

Friday, May 23, 2014

Brianna asherehekea birthday party yake na watoto wenzake shuleni Jomak

Ilikuwa ni sherehe ya kutimiza miaka mitatu ya mwanafunzi wa Jomak Day Care iliyopo Bahari Beach
Briana akimlisha baba yake keki

Huyu ni ndio mhusika wa hafla hiyo anaitwa Briana iliyowashirikisha wazazi wake na wanafunzi wenzake.
Akamlisha keki mama yake pembeni ni baba yake akifuatilia

Wanafunzi wenzake



Marafiki zake

Mmoja wa wamiliki wa shule hiyo Teddy Kimario akitoa maelekezo wa wazazi wa Briana ambapo kushoto ni mama yake mzazi aitwae Caroline Nkya na baba aitwae Nkya

Alisindikizwa na mdogo wake pamoja na Dada 

Wakapiga picha ya pamoja


Sunday, May 11, 2014

Shule ya Scholasica ya Moshi yatoa wanafunzi bora msingi

Na Mwandishi  Wetu, Dodoma

SHULE ya msingi Scholastica mkoani Kilimanjaro imetoa mwanafunzi bora wa kike katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2013 aliyekuwa miongoni mwa
wanafunzi 10 bora kitaifa waliopewa tuzo juzi mjini hapa na Makamu wa Rais, Dk
Mohamed Gharib
Bilal.

Mtoto huyo,Gladness Norbert (14) ambaye sasa anasoma Kidato cha Kwanza Shule ya Marian iliyoko Bagamoyo, Pwani, pamoja na wanafunzi wengine, wamepewa fedha taslimu na cheti.

Baba mzazi wa mtoto huyo, Norbert Gwebe aliyemsindikiza mwanawe kuhudhuria hafla hiyo ya kukabidhi tuzo kwa shule, wanafunzi, halmashauri na mikoa iliyofanya vizuri,
alisema pamoja na kazi ya Mungu, wazazi wanao wajibu wa kulea watoto katika
misingi ya kupenda masomo.

Aidha alisema nidhamu ya shule inachangia kufanya mtoto afanye vizuri kwenye masomo.

Alisema pamoja na wazazi kuwa karibu na binti yao, mtoto huyo aliishi bweni ambako
pia alipata malezi bora yaliyomjengea nidhamu ya kupenda kusoma.

Akizungumzia mkakati wa wizara kutoa tuzo na zawadi kwa wanaofanya vizuri, mzazi huyo alipongeza hatua hiyo. “Hela hata kama ni ndogo, zawadi ni zawadi.

Imempa changamoto mwanangu ya kuendelea kufanya vizuri,” alisema.

Mtoto huyo, Gladness  ambaye anaamini juhudi za walimu shuleni  Scholastica pamoja na uwezo wa Mungu vimemfikisha hapa, aliahidi ataendelea kujitahidi kufanya vizuri
katika masomo yake ya sekondari.

Katikakilele cha maadhimisho ya wiki ya elimu kitaifa yaliyoambatana na utoaji tuzo,wanafunzi
10 bora waliofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2013
wakiwemo wasichana watano na wavulana, walipewa tuzo.

Pia wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika mtihani wa  taifa elimu ya sekondari mwaka jana, wakiwemo wasichana watano na wavulana, walipewa tuzo.

Aidha shule 60 zilizoonesha maendeleo mazuri  zilipata
fedha taslimu sh 3,000 kwa kila shule mahsusi kwa walimu waliochangia kuleta
maendeleo mazuri.

Makamu wa Rais, Dk Bilal aliasa wale wote waliopwa tuzo kuhakikisha wanadumu katika kufanya vizuri kwenye sekta ya elimu.