Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, April 29, 2012

Tigo yanogesha siku ya Taaluma kwa Vyuo Vikuu



Mwenyekiti wa Bodi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Charles Nyoni (katikati) akikata utepe wakazi wa ziara ya kuzungukia vibanda vya maonyesho wakati wa maadhimisho ya siku ya Taaluma kwa Vyuo vikuu liliyofanyika Makumbusho ya Taifa kwa udhamini wa Tigo.Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha IFM, Profesa Mjema na Mwanafunzi wa Chuo hicho, Dorthea Msofe.

Tigo Yadhamini Siku ya Taaluma kwa Vyuo Vikuu

Tigo Yadhamini Siku ya Taaluma kwa Vyuo Vikuu
Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali na vyuo watapata fursa ya  kujumuika pamoja katika siku ya Taaluma iliyodhaminiwa na Tigo, na kupata fursa ya kukutana na waajiri wa makampuni mbalimbali kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa nane mchana katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa.
Vyuo vitakavyohudhuria ni pamoja na Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo cha Ardhi, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na vinginevyo. Wanafunzi watakuwa na nafasi ya kufahamiana, kupata taarifa za taalum na kupata taarifa moja kwa moja kutoka kwa waajiri ambao watakaokuwepo katika siku ya maendeleo ya taaluma.
 “Katika uchumi wa leo kuna changamoto nyingi, makampuni lazima yavute watu wenye vipaji bora ili kuendeleza ushindani. “Tukio hili linawasaidia waajiri kuangalia watu wenye vipaji zaidi,” alisema Alice Maro ambaye ni Afisa Uhusiano wa Tigo. ‘’Vijana wenye taaluma na motisha mbalimbali na wanafunzi wapya wanaweza wakajaribu taaluma wanazozipata darasani katika mazingira halisi ya kazi (Kwa vitendo) kwani wanaweza kuwa sehemu za hizo kampuni siku za karibuni’’ alisema.
Burudani ya moja kwa moja kutoka bendi za muziki wa hapa nyumbani itatolewa na Mapacha Watatu na wasanii mbalimbali kutoka Chuo cha IFM wakati wote wa tukio na baada ya hapo wanafunzi watajumuika pamoja katika ukumbi wa Cine Club.




Saturday, April 28, 2012

Kuna mengi ya kujifunza katika maonesho ya picha za Mama BAHAME katika Ujmaa Arts Gallery iliyopo Mbuyuni njia ya Mwenge

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nyayo Za Mama inayojishugulisha na sanaa ya  uchoraji na kunakshi picha ya Nyayo Za Mama, Candida Bahame (kulia) akimuonesha mdau wa picha Jese Mnguto picha anazoziuza katika Gallery ya Ujamaa (Picha na Mpigapicha Wetu)
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nyayo Za Mama inayojishugulisha na sanaa ya  uchoraji na kunakshi picha ya Nyayo Za Mama, Candida Bahame (kushoto) akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa
Ujamaa Art Gallery Lona Mashiba wakati wa ufunguzi wa maonesho ya mauzo ya kazi z sanaa za Mama Bahame yanayoendelea katika Gallery hiyo iliyopo Mbuyuni njia ya Mwenge (Picha na Evance Ng’ingo)
 Sehemu y apicha hizo zebnye ujumbe mbalimbali wa kuelimisha
Mkurugenzi wa Ujamaa Art Gallery Lona Mashiba akizungumza na wageni waliojitokeza wakati wa maonesho ya picha za Candida Bahame yanaoendelea katika Ujamaa Art Gallery iliyopo eneo la Mbuyuni njia ya kuelekea Mwenge

Mkurugenzi Mtendaji wa Ujamaa Art Gallery Lona Mashiba (wa kwanza) akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) Chansa Kapaya wakiangaliwa picha zilizochorwa na mchoraji Candida Bahame.

Habari Kamili 
Na Mwandishi Wetu
WANAJAMII wametakiwa kutumia kazi za sanaa za mikono za wasanii wa hapa nchini katika kupamba nyumba zao ili kuongeza hamasa na maendeleo ya tasnia hiyo hapa nchini.

Wito huo ulitolewa juzi na Mdau wa sanaa za uchoraji Candida Bahame ambae ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nyayo Za Mama wakati akizindua maoenesho ya wiki mbili ya kazi zake za sanaa.

Candida alisema kuwa wasanii wa hapa nchini wanao uwezo wa kuchora na kutengeneza picha kwa kutumia viashiria mbalimbali vya kisanii ambavyo zinapendezesha nyumba.

Alisema kuwa wanajamii wakiwa na utamaduni wa kununua kazi zao za sanaa na kuzipamba majumbani kwao watakuwa kwa kiasi kikubwa wamesaidia kukua kwa sanaakiwa kama mdau wa kazi za sanaa ya uchoraji hapa  nchini.

“ Mimi naona kuwa muda umefika kwa hoteli zetu, ofisi na hata nyumba zetu watu kutumia picha za wasanii wa hapa nchini katika kupamba nyumba zao ili kuonesha kuwa wanathamini na kutambua sanaa zetu hapa nchini” alisema Candida.

Akizungumzia sanaa yake hiyo ambayo alisema kuwa alianza tangia miaka ya 1980, Candida alisema kuwa gharama ya picha zake anazipanga kulingana na muda aliotumia kuzichora pamoja na umaridadi wa picha hizo.

Alisema kuwa anatumia kipaji chake kufikisha ujumbe kwa njia ya maneno ambapo anatumia shanga kushona maneno yenye ujumbe na pia anatumia shanga kutengenezea picha.Maonesho hayo ya wiki mbili yanaendelea katika Ujamaa Art Gallery.
Mwisho