Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, September 4, 2012

Madam Ritha atoa somo la kupambana na ukahaba uwanja wa fisi


 Madam hakusita kudondosha chozi wakati wa uzindizi huo ambao ulimgusa vilivyo
Hapa akicheza kwenda kwenye jukwaa la kuzindulia albamu hiyo ya aina yake iliandaliwa na mshindi wa bss 2009 Paschal Cassian.
Umati mkubwa wa watu ulijitokeza Uwanja wa Fisi kuhudhuria uzinduzi huo wa aina yake

MSHINDI wa shindano la bss 2009 Paschal Cassin amepania kukusanya shilingi milioni 30 kwa ajili ya kupambana na biashara ya uuzaji wa miili inayofanywa na machangudoa wa uwanja wa Fisi.
Cassian alisema hayo wakati akizindua albamu yake ya nyimbo za injili iitwayo  Yasamehe Bure  yenye nyimbo nane.
Nyimbo hizo ni  Chuki ya Nini, Nikumbuke na Mimi, Jina la Yesu, Mafuriko, Pesa, Baba na Usilie.
Kama ilivyo kawaida katika uzinduzi wa nyimbo za injili huwa kunakuwa na wakati wa kuchangisha fedha za kununulia albamu husika ambapo katika tukio hilo MC alianza kwa kuelezea uuhimu wa kuchangia albamu hiyo.
Mbali na kufafanua kwa inalenga kuwasaidia akinadada wanaojiuza lakini pia alisisitiza kuwa akinadada hao watapatiwa njia mbadala ya kuondokana na sakata hilo.
Naye Jaji Mkuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) Ritha Paulsen aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo alipopanda jukwaani alianza kwa kumkosoa MC kwa kusisitiza kuwa inatakiwa hata hao wanunuaji kwa maana ya wanaume kuacha kununua mara moja.
Alisema kuwa ili kupambana na biashara hiyo haramau inatakiwa kwanza wanaume kuepuka kwenda kununua madada hao kwa kuwa wanunuzi wasipokuwepo basi hata wauzaji hawatakuwepo.
Pia alichangia albamu hiyo kwa kuinunua kwa milioni 10 ili kufanikisha kampeni hiyo muhimu.

Naye Cassian alichangia kwa kusema kuwa akiwa kama kijana mbali na kumtumikia Mungu kwa kila jambo pia ameona kuwa ni wakati muafaka wa kuwatumikia wanadamu ambao ameanzia kwa wanadada hao wa Uwanja wa Fisi.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na maelfu ya watu waliojitokeza katika eneo hilo huku wengine wakiwa wanaimba nae na kucheza nae pamoja.

Akizungumzia zaidi albamu hiyo alisema kuwa ina lenga kuwarudisha waliopotea kwa Mungu kwa kuwapatia ujumbe wa neno la Mungu kwa njia ya nyimbo.   
Mwisho



0 comments:

Post a Comment