Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, September 9, 2012

Msaada huu kwa watoto wenye ulemavu utawasaidia kusoma vema

wheelchairs znz Ally Sihaji and son Hilali Silaji 13 years old

Salama Zaharani (10) na wazazi wake

Sadra Hassan (9)

Viti 30 maalum kwa watoto wenye ulemavu vimetolewa kwa watoto wenye ulemavu Zanzibar leo. Viti hivyo vimeagizwana kampuni ya Uchimbaji na utafiti wa Madini ya Montero yenye makazi yake Canada na washirika wake wa Tanzania Kampuni ya madini ya Wigu Hill. Viti hivi vimetengenezwa maalum kwa ajili ya watoto walemavu na shirika lisilo la kiserikali  ‘’Wheel chairs for Kids “ huko Australia.

“Tunafurahia kuweza  kupanua wigu wa misaada yetu kwa watoto kwenye kisiwa cha Zanzibar, kama sehemu yetu ya kusaidia jamii. Hivi viti vya matairi mawili  vitaboresha maisha yao na ya wazazi na walezi wao. Siku ya leo inaweka historia ya mkakati ambao, baadae viti vya walemavu vingine 130 vitasambazwa kwa watoto wa mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro’’alisema Grant Pierce Meneja Mkuu wa Montero Tanzania.

Utoaji wa viti hivyo ulifanyika rasmi katika hospitali ya Mnazi mmoja kwa ushirikiano wa klabu ya Rotary Zanzibar ambayo ilitafuta wapokeaji na kuandaa tukio hilo.

‘’Rotary inajihusisha na mipango mbalimbali ya kijamii huku Zanzibar na ni wazi kwamba watoto wenye ulemavu wanamahitaji zaidi kulio vikundi vingine vyote katika jamii yetu. Hii ni siku ya furaha tele kwao na kwetu.”Alisema mwanachama wa RotaryStephi Said.

Viti hivi vya walemavu vimetengenezwa kwa ustadi zaidi na vinaweza kutosheleza mahitaji ya kila mtoto kulingana na ulemavu wake.

Kuhusu kampuni  ya madini ya Montero
Kampuni ya uchimbaji wana utafiti ya madini ya Montero ni kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa madini ya Rare Earth Elements (REE) na inaendesha shughuli za Mkoa wa Morogoro kupitia washirika wake wa Wigu Hill. Pia ina maeno mengine Tanzania,Afrika Kusini na Quebec Canada

Kuhusu Wheelchairs for Kids
Klabu ya Rotary huko Australia Magharibi ilianzisha mkakati wa wheelchairs for kids mwaka1998,viti hivi maalum vinatengenezwa na wafanyakazi wastaafu wanaojitolea. Mpaka sasa ina nguvukazi ya watu wapatao 100, wengi wakiwa wastaafu, wanotengeneza,wanaohakiki viwango,na kupanga na kupakia kwenye maboksi, viti hivi.Wafanyakazi wengine wa kujitolea wanatengeneza foronya na zawadi ndogo ndogo  zinazoambatanishwa na viti hivi, kwa ajili ya wapokeaji.

 
 




0 comments:

Post a Comment