Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, October 13, 2013

Bonah Education Turst Fund yazinduliwa yaanza na kampeni ya kuchangisha ada

Kulikuwa na burudani safi

Meneja wa Masuala ya Kijamii wa kampuni ya Tigo, Woinde Shisael akizungumza na waandishi kuhusiana na ushiriki wa Tigo katika kampeni hiyo

Pia kulikuwa na Fashion Show

Mkurugenzi Mtendaji wa Bonah Trust Fund, Bonah Kalua

Kikundi cha Sanaa cha Safi Cultural Center



Mwanamitindo Mahiri Asia alikuwapo kusaidia kutoa burudani

Picha ya pamoja kati ya Bonah Kalua na wageni waalikwa

Mimi niliamua kuchangia pia ili kufanikisha harakati za mwanamama Bonah Kalua (kushoto) ambae ni Diwani wa Kipawa 
analenga kusomesha watoto wengi sekondari ambao wanakabiliwa na changamoto za ukosefu wa fedha
Pia kwa pamoja tunaweza kusaidia harakati hizo za Bonah pamoja na Tigo kwa kuchangia.0716 667470



Haya Habari Kamili




Kwa sasa wadau mbalimbali wanazidi kujitokeza katika kusaidia harakati za serikali za kuimarisha elimu hapa nchini.

Tumeshuhudia Tasisi ya Hassan Majar Trust Fund ambayo hivi majuzi imezindua harakati zake za kusaidia upatikanaji wa madawari nchini kwa ajili ya kusaidia wanafunzi kusoma wakiwa wanatumia madawati.

Pia wapo wadau wengine mbalimbali kama vile Mamlaka ya Elimu Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikisaidia ujenzi wa mabweni kwa kusaidiana na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini.

Hivi majuzi ilizinduliwa rasmi Taasisi inayojishughulisha na kusaidia uboreshaji wa elimu ya Bonah Education Trust Fund na ilianza kampeni ya kuchangisha fedha za kulipia ada wanafunzi.

Taasisi hiyo ilizinduliwa katika Uwanja cha Mnazi Mmoja na Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa jana ambae aliwataka wananchi kuchangia fedha kwa lengo la kuwalipia ada wanafunzi 100 wa sekondari.

Slaa alisema kuwa ili kuwa na jamii bora inatakiwa vijana wapate elimu na kuongeza kuwa elimu ya sekondari ni msingi mzuri wa utakaowawezesha watoto kuona mbali.

Alisema kuwa mbali na serikali kuwa na kampeni ya kusaidia ujenzi wa mabweni, madarasa na vyumba vya maabra ni muda wa wanajamii kuhakikisha kuwa mabweni hayo na madarasa hayo yanatumiwa na wanafunzi.

" Najua hata tukijenga madarasa na mabweni kama hakuna wanafunzi ni kazi bura kabisa kinachotakiwa ni wanafunzi kupelekwa shule na ili kufanikisha hilo ni lazima kuchangia hivyo basi chondechonde tuungane"alisema Slaa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bonah Kalua ambae pia ni Diwani wa Kata ya Kipawa, alisema kuwa kutakuwa na kampeni mbalimbali za kuwataka wanajamii kujitokeza na kuchangia.

Alisema kuwa kuna namba ya simu ambayo ni 0716 667470 ambapo walioguswa na harakati hizo wanaweza kuchangia kwa njia ya Tigo pesa

Kwa upande wake Meneja anaeshughulikia masuala ya Huduma za Kijamii wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa Tigo inaendelea na harakati za kuwarudishia wanajamii mafanikio yake kwa kusaidia masuala ya elimu na mengineo.


" Tigo ina furaha kubwa kusaidiana na Taasisi hii katika kuifikia jamii ya kitanzania na kuipatia elimu na tuna imani kuwa fedha zinazochangiwa zitasaidia  wanafunzi hao kupata elimu bora" alisema Woinde.
Mwisho

0 comments:

Post a Comment