Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, October 2, 2013

Haa!!! walimu 529 kufukuzwa??


WALIMU 529 wamefukuzwa kazi katika  miaka mitatu iliyopita kutokana na utoro maeneo yao ya kazi.

Katibu Msaidizi, Idara ya Utumishi wa Walimu katika ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma, Christina Hape alisema idadi hiyo inatokana na mashauri 669 yaliyofikishwa kwenye ofisi zao kutokana na utoro wa walimu kwa zaidi ya siku tano.

Alisema mwaka 2010/2011 walipokea mashauri 260, mwaka 2011/12 mashauri 152 na mwaka 2012/13 mashauri 257.

“ Hayo ni mashauri ambayo yamefika makao makuu, na baadhi yake yalirejeshwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosewa taratibu. Lakini katika ngazi ya wilaya zote nchini mashauri 1,128 yalishughulikiwa,” alisema.

Alisema ni makosa kwa walimu kuwa nje ya kituo cha kazi bila kufuata taratibu na kuwa suala hilo linakwenda pia kwa walimu wa serikali wanaofundisha masomo ya ziada kwenye shule binafsi wakati wa muda wa kazi.

Kuhusu makosa ya walimu wenye uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi, Hape alisema walimu 84 walikutwa na kosa hilo kuanzia mwaka 2008 hadi 2012 na kukiri kuwa tatizo hilo ambalo linachangiwa na wahusika, jamii kushindwa kutoa ushahidi ili kuwatia hatiani walimu waliofuata maadili ya kazi zao.

Akizungumzia walimu walioripoti vituo vya kazi katika ajira za mwaka jana, Katibu Msaidizi  katika idara hiyo, Evelyne Omari alisema walimu 11,000 walisajiliwa baada ya kusaini mkataba na mwajili wao na kukiri kuwapo baadhi ya walimu ambao wamekuwa hawajisajili kwenye tume hiyo.

Naibu Katibu Mkuu, Edwin Mikongoti  alisema tume yake imekasimisha madaraka kwa wakuu wa shule, vyuo na walimu wakuu kushughulikia makosa ya madogomadogo ya kinidhamu na kutoa adhabu kwa walimu na wakufunzi.

0 comments:

Post a Comment