Help Children
Love them
Saidia Watoto

Friday, September 27, 2013

Elimu kupinga ugaidi ianzie ngazi ya chini

Askari akiwakoa watu waliokuwa kwenye Mall hiyo
 HIVI karibuni nchini Kenya katika jiji la Nairobi kulitokea tukio kubwa na la kusikitisha lililohusisha magaidi wa kundi la El Shabab kuvamia na kuua watu wasiokuwa na hatia waliokuwa kwenye Mall ya West gate nchini humo.

Tukio hilo la aina yake limegusa nyoyo za watu wengi duniani kote hasa ikizingatiwa kuwa wapo watu mbalimbali wakiwamo wanawake na watoto wameuwawa katika tukio hilo.


Mauaji hayo ni ya kinyama ambayo yanatakiwa kutufumbua macho wanajamii katika kuangalia namna mpya ya kukabiliana na matukio kama hayo.


Hakika njia mojawapo kubwa ya kupambana na matukio kama haya ni kwa njia ya kutoa elimu ya kutosha katika kupambana na hali hiyo.


Zipo elimu kwa njia ya filamu ambazo zimetolewa ambapo wacheza filamu wa mataifa mbalimbali wamekuwa wakielimisha vita dhidi ya tukio hilo.


Lakini pia zipo elimu kwa njia za nyimbo ambapo wasanii wamepiga vita kwa kuonesha athari za matukio kama hayo pia.


Kwa sasa harakati za kuelimisha watu kuhusiana na ubaya wa ugaidi ziingie  katika ngazi mbalimbali za elimu hasa sekondari, hapa nikiwa namaanisha katika somo kama Civics.


Hii itasaidia kwa kiasi fulani kuwaweka watu tayari katika ufahamu wa matukio kama hayo ambayo ni yameshaanza kuwa hatari kwa usalama wa mataifa ya Afrika Mashariki.

Wanafunzi wakielimishwa wanaweza kuwaelimisha watu mbalimbali katika jamii na hatimae kushiriki kikamilifu katika kupambana na hali hiyo.


Ifikie wakati hata elimu hiyo ielezee namna bora ya kupambana na ugaidi huo hasa katika kuwajibika kwa kuwafichua watu katika jamii ambao wanahisi kuwa sio wema.


Ni muda sasa kwa Tanzana kuliangalia suala hili katika umakini wa hali ya juu na kujipanga ili kuhakikisha kuwa hawa watu hawaingii hata kidogo na kufanya ubaya huku kwetu.


Elimu hii ikiendelea itasaidia wanajamii nao kutambua ubaya wa watu hawa na kamwe kutowaunga mkono.


Kwa sasa utakuta basi hasa daladala zina picha za Osama au utakuta limeandikwa jina la kundi la El Shabab sasa hio sio nzuri kwa kuwa ni kama linaongeza hamasa ya ugaidi.


Ni matumaini yangu kuwa kila mtanzania analiona tukio la ugaidi kuwa ni lake na lipo karibu yake na hivyo ana nia ya dhati katika kupambana nalo.


Blog hii inaribisha mawazo yanayohusiana na utoaji wa elimu dhidi ya ugaidi.
Mwandishi wa hili wazo ni
Evance Ng'ingo
0714 43 65 94


0 comments:

Post a Comment