Help Children
Love them
Saidia Watoto

Thursday, October 3, 2013

Coke Studio, a platform for learning music

Famous Comedian in town who was the  Master of Ceremony, Evance Bukuku (left) Coca - Cola Brand Manager  Maurice Njowoka, Lady Jaydee and Evance from this blog

Njowoka insists something to Jide

Madee

The B Band

Diamond the Coca Cola's ambossodor


Country Director for Coca-Cola Tanzania, Yebeltal Getachew (left ) Diamond and Coca Cola brand Manager in Tanzania Maurice Njowoka

Some hugs

Ongeza kichwa




Na Evance Ng'ingo

KWA sasa katika medani ya muziki hapa nchini na duniani kote kumekuwa  harakati zinazofanywa na wadau mbalimbali wa muziki ambapo wameamua kuwekeza katika fani hiyo.



Uwekezaji huo katika muziki upo kwa aina mbalimbali ambapo wapo ambao wanawekeza kwa kuwasaidia wasanii kujiinua kimuziki na pia wao ambao wanajipanga kuwekeza kwa kufungua miradi kadhaa ya kukuza muziki.



Miradi hiyo ni kama vile ile ya kuwekeza studio au vifaa vingine vya muziki ambapo wasanii wanaendelezwa kisanaa.



Miradi kama vile Tusker Project Fame, Epiq Bongo Star Search au ile iliyokuwa CocoCola Pop Idol ni moja kati ya miradi ambayo makampuni makubwa yamewekeza au kudhamini kwa lengo la kusaidia sanaa.



Miradi mingine inalenga kuinua asili ya muziki kwa kuanzisha nyimbo zenye vionjo vya muziki wa asili.

Mradi wa Coke Studio ni moja kati ya miradi ya kuendeleza muziki hapa nchini wenye lengo la kuendeleza muziki wa kisasa wenye asili ya Afrika.



Coke Studio ni kipindi muziki ambacho kitakuwa kikirushwa kwenye runinga na kwa hapa nchini kwa kuanzisha kitahusisha wasanii kama vile Nasib Abdul, Diamond na Judith Wambura, Lady Jaydee.



Hicho ni kipindi ambacho kitahusisha wasanii wenye miondoko tofautitofauti ya kisasa kitakuwa kikiitwa Coke Studio Afrika.



Kipindi hicho kinahusisha wasanii kutoka Afrika Mashariki na wengine wa kutokea Afrika Magharibi na Kusini.



Wasanii kutoka kona nyingine ya Afrika ni pamoja na Seif Keita kutoka nchini Mali, King Sunny Ade, Mi, Waje, Jimmy Jat and Bez froma Nigeria.



Kwa upande wa  Afrika Mashariki wengine ni pamoja na Octopizzo, Miss Karun and Just a Band wakiwa wanatokea nchini Kenya na pia kuna Hip Hop Panstula pia kuna na Lilian Mbabazi  wa Uganda pia.



Pia wapo akina Boddhi Satva pamoja na Tumi wa Afrika Kusini pamoja na kundi la Culture Music la kisiwani Zanzibar.



Kitaanza kurushwa kesho kuanzia saa tatu usiki katika luning ya ITV ambapo kitaanza kuoneshwa kwa miezi miwili.



Wasanii hao akina Diamond na Lady Jaydee ni wasanii ambao walienda nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki katika kurekodi kipindi hicho.



Baada ya kumalizika kwa season one ndio itaanza rekodi ya season 2 ambapo wasanii wengine watachaguliwa pia.



Umoja wa wasanii mbalimbali kama hao wakishiriki kwenye kipindi hicho watasaidia harakati za kupata muziki wa kisasa wenye asili ya Afrika.



Pia kutakuwa na wasanii walioshirikishwa katika kipindi hicho ambapo  kutakuwa na wasanii kama vile Bamboo wa Kenya, Sega na Dela pamoja na Kassongo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na pia Temi Dollface kutoka Nigeria.



Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka anafafanua kuwa Coke Studio itakuwa ikioneshwa Kenya, Uganda, Tanzania na Nigeria.



Anaongeza kuwa itaenda hewani kwa vipindi vinane vya dakika 45 kila kimoja huku kukiwa na saa mbili za vipindi maalum kwa mwaka mpya.



Aliongeza kuwa katika kila kipindi kutakuwa na masuala mbalimbali muhimu katika sanaa ambapo anatolea mfano wa ujengaji wa sauti za kipekee kutoka kwa wasanii.



" Pia kutakuwa na fursa ya watazamaji kuona kile kitakachokuwa kikijili nyuma ya pazia ambapo wataona namna kipindi kinavyotengezwa na mengine" alisema Njowoka.



" Kwa ni fursa kubwa sana kwa Tanzania kushirikishwa kwenye kipindi kama hiki kwa kuwa kuna nchi nyingi Tanzania ambazo zingependa kuwa na miradi kama hii lakini kwa sasa ni Tanzania ipo na wasanii  wetu pia wamo." alisema Njowoka.



Anaongeza kuwa hiyo ni fursa kubwa  kwa wasanii wa hapa nchini kutangaza kazi zao za sanaa pamoja na kuonesha vipaji vyao katika nchi nyingine nyingi za Afrika.



Anatolea mfano kwa nchi kama Pakistani ambao kipindi hicho kimekuwa na mafanikio makubwa huku kikikadiriwa kuwa na watazamajimilioni 77 kwenye You Tube peke yake.



Akizungumzia ushiriki wake katika kipindi hicho msanii Lady Jaydee anasema kuwa amekuwa akiimba na kujitangaza sehemu mbalimbali za ndani na nje ya Tanzania.



Anasema kuwa anaona kuwa kipindi hicho kitasaidia kuinua harakati zake za kujitangaza zaidi nje ya nchi.



"Kupitia kipindi hiki sisi kama wasanii mbali na kukuza vipaji vyetu, kukutana na kufanya kazi pamoja na wasani wengine lakini pia ni wakati muafaka  kusema kwa ile ndoto yangu ya kujitangaza kimataifa zaidi inaenda  kukamilika" alisema Lady Jaydee.





Kwa upande wake msanii Diamond Platnumz anasema kuwa akiwa kama balozi wa Coca Cola hiyo kwake ni muendelezo wa fursa ambazo amekuwa akizipata kupitia kampuni hiyo.



Kipindi hicho asili yake ni nchini Brazil ambapo kimekuwa kikiitwa Estudio Coca - Cola ambacho kilirushwa kwa mara ya kwanza machi 2007.



Kikiwa kinaoneshwa hapa nchini washabiki watakuwa na fursa ya kuona na pia kupakua (downloading) vitu mbalimbali kama Video huku pia wakiwa katika nafasi ya kushinda vitu mbalimbali.


0 comments:

Post a Comment