Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, March 28, 2012

Millen Magese amaliza kuwafundisha wanamitindo wake na sasa tayari kusafiri nao.

 "Ili muweze kuwa wanamitindo bora ndani na nje ya nchi inatakiwa kwanza mjiamini, mnasikia? na pia kuzingatia yale niliyowafundisha"
 Mkiwa mbele ya watazamaji katika shoo mnapomaliza kutembea mnatakiwa kupozi hivi sawa?
Sikia mdogo wangu huwa hizi nyusi zinatengenezwa hivi sawa?

Na Mwandishi wa Elimu Bora Tanzania.
WABUNIFU watatu wa mavazi nchini watawakilisha Tanzania katika maonesho makubwa ya mavazi ya Afrika Kusini yatakayoshirikisha wabunifu kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Wabunifu hao wamechaguliwa kutoka katika mpango wa kuendeleza wanamitindo na wabunifu wa mavazi ulioanzishwa na mwanamitindo mtanzania anayefanya shughuli zake nchini Afrika Kusini Millen Magese kupitia kampuni yake ya Millen Magese Group company Limited.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Millen alisema kuwa mpango huo umeanza kuwa wa mafanikio kwa kuwa ameweza kuwapata wabunifu wazuri pamoja na wanamitindo wenye mvuto.
Aliwataja wabunifu hao kuwa ni Doreen Noni anayetumia Lebo ya eskado bird, Jamila Vera Swai na Evelyne Rugemalira ambao watapanda jukwaani April Mosi ambapo watawakilisha katika kipengele cha Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX).
Alisema kuwa kabla ya kuwachagua alipata fursa ya kutembelea wabunifu hao na kujionea jinsi walivyokuwa wabunifu katika fani hiyo na kuhamasika kuwachukua na kushiriki katika maonyesho hayo maarufu ya mitindo katika bara la Afrika.
Alisema kuwa amevutiwa sana na jinsi walivyokuwa wabunifu na hivyo kuhamasika kuwapa nafasi hiyo ya kujitangaza kimataifa kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kupitia mradi huu anbao pia dhumuni lake kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kimataifa.
Alifafanua kuwa mpango huu pia una lengo la kuitangaza Tanzania kupitia fani ya mitindo dunia nzima kama New York fashion week, London Fashion Week, Lagos Fashion week na Milan Fashion week.
Kwa upande wa wanamitindo waliochaguliwa ni  Anastazia Gura (21) huku wengine waeili wakiwa ni  mapacha,Victoria Casmir (20) na Victor Casmir ambao wao walichaguliwa kutoka katika zoezi la kuwachagua wanamitindo lililofanyika Jumapili iliyopita.
Katika kuonesha nia ya kweli ya kusaidia mitindo hapa nchini Millen pia ameingia mkataba wa kufanya kazi na mwanamitindo wa kiume, Benard Chizi ambaye atakuwa akisaidiana naye katika kazi zake.
Mwisho.



0 comments:

Post a Comment