Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, March 11, 2012

Tigo yamwaga Compyuta Chuo Kikuu cha Dodoma



  Mratibu wa promosheni ya tigo katikaElimu Edward Shila akikabidhi msaada wa Kompyuta kwa Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Profesa Shaaban Mlacha juzi. Jumla ya Kopyuta 48 zenye thamani ya zaidi ya Sh 37 Milioni zilikabidhiwa na kampuni hiyo kwa ajili ya Kitivo cha sayansi ya tiba kwa jamii. (Picha na Kwa hisani ya Tigo)


Na Mwandishi wa elimu bora kutoka Dodoma.
Tigo imetoa msaada wa kompyuta 48 kwa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kama sehemu ya kuboresha sekta ya elimu na kusaidia matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tecknohama).

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyiaka leo katika chuo kikuu cha Dodoma. Kompyuta zilikabidhiwa kwa niaba ya Tigo na mratibu wa Promosheni na Matukio Bwana Edward Shila. Akizipokea kwa niaba ya chuo,kaimu makamu mkuu mipango, fedha na utawala, Prof. S.A.K.Mlacha ameshukuru Tigo kwa msaada huo na kusema kuwa kompyuta hizo zitasaidia kuboresha mahitaji ya Tecknohama chuoni hapo.

“Ili tuweze kukabiliana na ushindani duniani,wanafunzi wanahitaji kuwa na uelewa juu ya kompyuta na tecknohama,” alisema Prof. Mlacha. “Msaada huu utawaunganisha na taarifa na tecknolojia kama njia ya kusoma na kupata taarifa ya yale yanayoendelea katika masomo yao,” alisema.

Bw. Shila alisema, “Teknolojia imekuwa ni sehemu kubwa ya maisha yetu, elimu na kazi. Tigo imefurahia kutoa komputa na vifaa vingine kwa viongozi wetu wajao.”

Msaada huu ni muendelezo wa msaada wa vitabu, vilitolewa katika fani ya uhandisi,udaktari na fani nyinginezo,ambavyo vilikabidhiwa katika chuo kikuu cha Dodoma Desemba mwaka jana  na kuhifadhiwa katika maktaba tano za chuo hicho

0 comments:

Post a Comment