Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, March 6, 2012

TAASISI ya kifedha ya Bayport imetoa msaada kwa Sekondari ya Mpindimbi





TAASISI ya kifedha ya Bayport hapa nchini, imeendelea kutoa msaada wa vitabu kwa shule ya Sekondari Mpindimbi ili viwasaidie kukuza kiwango cha elimu nchini.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika viwanja vya shule hiyo na kupokelewa na Ofisa Elimu wa Wilaya ya Masasi kwa shule za sekondari, Generosa Nyoni.

Akizungumza katika makabidhiano hayo mjini hapa jana, Meneja wa Kanda ya Kusisni, Aidan Kessy, alisema msaada huo ni endelevu kwa shule 20 na kwa wilaya zisizopungua 20 kwa mikoa ya Tanzania Bara.

Alisema wanaamini kwa kutoa msaada huo wa vitabu kwa shule hiyo ya Mpindimbi, walimu na wanafunzi wataweza kuvitumia vizuri kwa ajili ya maendeleo ya elimu nchini.

“Huu ni mkakati endelevu uliobuniwa maalum kwa ajili ya kuwapatia wanafuunzi urahisi kwenye shughuli zao.

“Naamini mambo utakuwa ni mpango mzuri na wenye tija kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata dhana za kujifundishia ili waelimike zaidi,” alisema.

Naye Ofisa Elimu wa Wilaya kwa shule za sekondari mjini Masasi, Generosa Nyoni, akiwashukuru Bayport kwa kuwasaidia vitabu kwenye eneo lao.

“Tunashukuru na wengine waige mwendo huu maana ndio utakaowawezesha wanafunzi wamudu masomo vizuri, “ alisema.
Tayari shule mbalimbali zimenufaika kwa mpango huo wa kutoa msaada wa vitabu ulioanzishwa mwaka jana.


0 comments:

Post a Comment