Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, March 18, 2012

Ujumbe kutoka Alice Foundation.



Katika kata ya Ubungo iliyopo Ubungo mkoani Dar es Salaam kuna mahitaji mbalimbali kwa wanajamii waishio katika kata hiyo ambapo  kuna wanafunzi ambao wamejiunga na masomo ya Sekondari.

Kati ya wanafunzi hao wapo ambao wanahitaji misaada mbalimbali kuhusiana na elimu yakiwamo mabegi, kalamu na mengineo muhimu.

Yanahitajika madaftari 1000 ambayo yatasaidia wanafunzi zaidi ya 100 walio katika mazingira hatarishi katika kata hii ya Ubungo.

Zoezi hili linaratibiwa na Alice Foundation ambapo wana ratibu masuala mbalimbali katika kata hii yakiwamo masuala yahusuyo haki za wanawake, masuala ya afya, mazingira na vijana kiujumla.

Wasiliana Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo kwa mchango wako wowote ule.

Alice Dosi Mwamsojo
0713 022558

0 comments:

Post a Comment