Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, March 12, 2012

Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Mkwawa chakumbwa na dhahama ya moto

 Kitanda hiki kiliteketea kabisa
 Kikosi cha Zima moto kiliwasili kuzima moto huo lakini hata hivyo walifika wamechelewa na kukuta moto umeisha
Polis akichukua maelezo kutoka kwa mwanafunzi huyu kuhusiana na tukio hilo.

Na Mdau wa Elimu Bora, Iringa.

Moto mkubwa ambao chanzo chake bado kufahamika umeteketeza vyumba viwili vya bweni la wasichana maarufu kama Hall 6 vyumba Block W katika chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE) Iringa .

Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa chanzo cha moto huo bado hakifahamiki .

Walisema kuwa moto huo ulianza kuwaka katika chumba kimoja wapo chumba Block W muda wa saa 6 mchana na kuwa wakati huo baadhi ya wanafunzi walikuwa wamejipumzisha katika vyumba hivyo .

Hivyo walisema kuwa waliona moto huo ukianza kuwaka katika chumba kimoja wapo na kuanza jitihada za kujaribu kuzima moto huo bila mafanikio hadi kikosi cha zimatomo kutoka Manispaa ya Iringa na jeshi la polisi walipofika kuzima moto huo.

Mkuu wa chuo hicho cha Mkwawa Prof. Philimon Mushi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la moto japo amesema kwa sasa ni mapema sana kuelezea kwa kina suala hilo na kuwa taarifa zaidi ataitoa baada ya uchunguzi wa tukio hilo kufahamika ikiwa ni pamoja na kujua madhara yaliyojitokeza na chanzo cha moto huo.

0 comments:

Post a Comment