Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, December 5, 2012

Wanafunzi wa darasa la kwanza watozwa michango

Watoto darasa la 1 watozwa Watoto darasa la 1 watozwa michango michango
WAKATI uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa ajili ya mwaka wa masomo 2013 ukiendelea, baadhi ya shule za msingi za jijini Dar es Salaam, zimeweka utaratibu wa kuwatoza michango wazazi wanaofika shuleni kuwaandikisha watoto wao.
Gazeti hili limebaini baadhi ya shule ambazo wazazi na walezi waliokwenda kuandikisha watoto wao, wakatakiwa kulipa kuanzia kati ya Sh 26,000 hadi 28,200, jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu uliowekwa na Serikali inayosisitiza elimu ya bure katika shule za msingi.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika shule za msingi Tumaini na Kimanga zilizopo katika Manispaa ya Ilala, umebaini kuwapo kwa hali hiyo na kigezo cha uchangiaji wa michango mbalimbali kikitumika kama sababu ya utozaji wa fedha hizo.
Suala hilo ambalo limelalamikiwa na wazazi waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wiki iliyopita na wiki hii, pia limedaiwa kufanyika katika shule hizo bila taarifa zozote kwa uongozi wa Serikali ya Mtaa na kusababisha mgongano baina ya wazazi na uongozi wa mtaa.
Gazeti hili lilifika katika shule hizo kwa nyakati tofauti na kukutana na hali hiyo huku wahusika waliokuwa wakiandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza wakisisitiza kutompokea mwanafunzi yeyote ambaye hatakuwa na kiasi hicho cha fedha kilichopangwa.
Katika Shule ya Msingi Kimanga, mzazi alitakiwa kumlipia mwanawe Sh 10,000 ya choo, Sh 10,000 ya madawati, Sh 6,000 ya fulana, Sh 1,200 ya nembo katika shati pamoja na fedha ya mlinzi Sh 1,000.
Katika Shule ya Msingi Tumaini, wazazi na walezi wamekuwa wakitozwa Sh 15,000 ya madawati, Sh 7,000 ya fulana, Sh 2,000 ya lebo, Sh 2,000 ya gharama ya mlinzi pamoja na Sh 2,000 ya picha ambayo anatakiwa kwenda nayo siku anayoanza shule.
“Hatumpokei mtoto yeyote ambaye mzazi wake hatakuja na fedha za uandikishaji, huo ndio utaratibu tuliouweka,” alisema Mwalimu anayeshughulikia uandikishaji wa wanafunzi hao katika Shule ya Msingi Tumaini ambaye hata hivyo hakuwa tayari kutaja jina lake.
Mwalimu mwenye jukumu kama hilo katika Shule ya Msingi Kimanga aliyejitambulisha kwa jina la Mwalimu Mhina, alisema kama mzazi hatakuwa na fedha hizo, mwanafunzi atapokewa, lakini mzazi ataendelea kudaiwa.
Walimu wakuu wa shule hizo hawakupatikana kwa madai ya kuwa nje ya maeneo ya shule kwa shughuli zingine za kiofisi. Lakini uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Tabata Kimanga, ulikiri kupokea taarifa hizo huku ukisisitiza kutopokea malalamiko kutoka kwa mwananchi yeyote kuhusu suala hilo.
“Taarifa hizo tumezisikia, isipokuwa hatujajua kama suala hilo lipo kweli, utaratibu uliowekwa na Manispaa kama kungekuwa na uchangiaji wowote, lazima wangetuandikia barua ili tuwajulishe wananchi wetu wafahamu,” alisema Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Mataa wa Kimanga, Flora Musiange.
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime alipoulizwa, alisisitiza kuwa uandikishaji wa wanafunzi hao ni bure huku akiahidi kumtuma haraka Ofisa Elimu kufuatilia suala hilo katika shule hizo.
“Hakuna shule yoyote inayopaswa kutoza gharama za uandikishaji, nilipata malalamiko hayo katika Shule ya Ukonga nikamtuma Ofisa Elimu kufuatilia, nipe saa mbili ofisa wangu atakuwa ameshafika katika shule hizo,” alisema Fuime alipozungumza na gazeti hili jana mchana.
Mulugo afunga shule
Wakati wazazi wakitozwa fedha za kuandikisha wanafunzi wao, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amezifunga shule mbili kwa kukiuka utaratibu wa ujenzi wa majengo ya shule.
Moja ya shule hizo inamilikiwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Kaumo ambaye amefungiwa kwa kujenga fremu za maduka 10 mbele ya shule kinyume cha sheria.
Aidha, Waziri ameahidi kufuatilia usajili wa shule hiyo kwani inaonekana kusajiliwa Juni mwaka huu wakati maduka hayo hayapo wakati Septemba Mulugo alibaini maduka katika shule hizo.
Shule hiyo ya Awali na Msingi ya Heroes iliyoko Chanika wilayani Ilala imefungiwa hadi itakapobomoa maduka hayo au kuihamishia sehemu nyingine.
Akiwa katika ziara ya kutembelea shule, Mulugo alifika shuleni hapo na kufunga shule hiyo na kumtaka mmiliki ifikapo Januari asipokee wanafunzi mpaka warudishe majengo kama ilivyosajiliwa.
Kaumo alikubali kufanya makosa ya kujenga maduka na kuahidi kufanya marekebisho kwa kubomoa maduka wiki ijayo na kurudisha kama ilivyokuwa mfumo wa zamani.
Alisema lengo lilikuwa kuwa na biashara zinazoendana na mahitaji ya wanafunzi shuleni hapo na alipopata taarifa ya Naibu Waziri kupita na kukemea maduka shuleni aliyafunga yote.
Katika Shule ya Deli iliyopo Pugu, Mulugo alibaini shule hiyo haijasajiliwa, lakini imeendelea kutangazwa kutoa elimu ya kitaifa ya shule ya awali na uangalizi maalumu wa watoto.
Alipofika shuleni hapo alikuta tangazo linaloonesha ni shule ya kimataifa ya awali na kuwaamrisha kulifuta kwa kuwa haijasajiliwa kutokana na eneo lake kuwa dogo na limezungukwa na maduka.
Aliyekuwa Mwalimu wa Taaluma shuleni hapo, Talile Hussein alikiri kutosajiliwa na kwamba awali ilikuwa sekondari, lakini baada ya kupata matatizo ya kidato cha pili mwaka jana, waliwaomba wazazi kuhamisha wanafunzi wote na kubaki kituo cha tuisheni.
Alisema sasa wako katika mpango wa kuanzisha shule ya kimataifa ya awali na wameanza kutangaza bila kusajili. Alikiri pia waliwahi kukataliwa kusajiliwa kwa kuwa eneo lao
habariLeo
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo

0 comments:

Post a Comment