Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, December 23, 2012

Nimekuja Bongo kujifunza muziki---Ngeruka Faycal

Elimu kumbe sio katika masuala ambayo yamekuwa yakionekana kuwa ni rasmi peke yake lakini kumbe unaweza kujiongezea elimu hata katika tasnia nyingine kama vile muziki na nyinginezo ambazo nazo zimekuwa zikipelekea maisha kusonga mbele

huyu ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Rwanda ambae kwa sasa yupo hapa nchini kwa ziara ya kimafunzo ya muziki akishirikiana na wasanii wa hapa nchini kujifua zaidi
Akiwa na msanii Cyril wa hapa Bongo

Akiwa na Cyril, Ben Paul pamoja na yeye mwenyewe

Hawa wadau wakishajipika kimuziki na wakitoa ngoma yao basi mambo yatakuwa mazuri sana    



Pata habari kamili.


MSANII wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Rwanda aitwae Ngeruka Faycal amesema kuwa Tanzania ni sehemu ya kujifunzia masuala mengi yahusuyo muziki na sanaa nzima kiujumla.

Faycal alisema kuwa kwa sasa ameamua kujihusisha zaidi na wasanii kutoka Tanzania na hivyo amekuja kujifunza kwanza muziki unavyotakiwa kwenda.

Akiwa hapa nchini anatarajia kuachia wimbo wa Kiswahili na msanii mahiri wa nyimbo za Bongo Flava Ben Paul wa hapa Tanzania.

Msanii huyo mwenye makazi yake nchini Ubelgiji anasifika kwa uwezo wake wa kupanga sauti mbalimbali na kwa sasa tayari ameanza mazungumzo Ben Paul kupitia meneja wake wa iliyopo nchini Ubelgiji.

Aliliambia gazeti hili kuwa amekuwa akifuatilia namna ambavyo Ben Paul anaimba na amekuwa akifanya vema katika muziki huku akisisitiza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akivutiwa na vionjo vya muziki wa Jazz vilivyopo katika nyimbo za Ben Paul.


Naye Ben Paul wakati akizungumza na gazeti hili alisema kuwa mpango wake kwa sasa ni kujitanua zaidi kimuziki kwa hiyo kuimba na msani huyo wa Rwanda ni hatua moja wapo ya kutimiza ndoto zake.


“ Mimi naona kuwa kwa sasa huyu msanii ni msanii ambae anaweza kuimba kila aina ya sanaa na pia naona kuwa kwa sasa kuna uwezekano wa kufanya kazi pamoja ila ndio mazungumzo yanaendelea kati ya meneja wangu na wa Code” alisema Ben Paul.


--- -------





0 comments:

Post a Comment