Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, December 5, 2012

Tanzania Mitindo House ilvyochangisha fedha za kusaidia elimu ya watoto waishio mazingira magumu

Add caption

Wanamitindo waliwakilisha pia katika kuchangisha fedha hizo







Habari Kamili


Na Evance Ng’ingo
ONESHO la mavazi kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watoto waishio katika mazingira hatarishi juzi lilikusanya shilingi milioni 72  kwa njia ya mauzo ya nguo na vitu vya thamani.

Onesho hili liitwalo Red Ribon liliandaliwa na mbunifu wa mavazi Khadija Mwanamboka kwa kushirikiana na Flaviana Matata Foundation ambapo ilihudhuriwa na watu wengi.


Vitu vilivyouzwa ni pamoja na vinyago, nguo za kisasa, nguoz zilizobuniwa na wabunifu wa ndani, vitabu na bidhaa nyinginezo muhimu.


Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana kutokana na michango itokanayo na  onesho hilo la mavazi kwa miaka mitano Kadija alisema kuwa wanawahudumia watoto katika vituo vya Magomeni na Kigamboni ambapo wanatoa misaada kwa watoto mbalimbali.

Alisema kuwa kupitia mauzo ya kazi mbalimbali za wabunifu wa mavazi wameweza kupata fedha kwa njia ya mauzo ya nguo na watu wengi wametoa misaada yao.

Katika mauzo ya jana Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe alichangia kwa kununua kitabu kwa shilingi milioni 3 ambapo pia alichangamsha hafla hiyo baada ya kuimba wimbo wa leta tutigite akiwa na msanii Linex.
Watu wengine mbalimbali walichangia fedha jana kwa njia mbalimbali ambapo Mkurugenzi wa Benchmark Production Ritha Paulsen alinunua gauni lililotolewa na mbunifu wa mavazi Evelyn Rugemalila wa Eve Collection kwa shilingi milioni 2
Mwisho



0 comments:

Post a Comment