Help Children
Love them
Saidia Watoto

Wednesday, December 19, 2012

Tumekuja kufundishana mpira- Zambia

Mchezaji bora Afrika Katongo akitoa maelezo kuhusiana na mchezo wao dhidi ya Taifa Stars

Huyu ndo Katongo mchezjai bora Afrika 2012

Hapa wakitoka katiak uwanja wa ndege kuelekea hotelini kwao




Na Mwandishi wa Elimuboratanzania

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Zambia Herve Renard amesema kuwa mchezo wao wa keshokutwa dhidi ya timu ya Taifa Stars una umuhimu mkubwa kwao katika kujiandaa na michuano ya Afrika.

Alisema kuwa alipopewa taarifa na shirikisho la Soka la Zambia kuhusiana na mechi hiyo ya kirafiki alifurahia kwa kuwa alijua anakuja kucheza na timu yenye uwezo.

Alisema kuwa anatambua anatambua uwezo wa wachezaji wa Tanzania kwa kuwa wanauthubutu wa kujaribu kufika mbali.

Alisema kuwa wachezaji na timu nxima kiujumla ni nzuri na kuongeza kuwa ni fursa nzuri katika kuwapima wachezaji wake wa sasa.

“ Changamoto kubwa tuliyonayo ni kulinda ushindi wetu huu na kuhakikisha kuwa haututoki n ahivyo mechi kama hizi ni nzuri kwetu katika kujipima” alisema kocha Renard.
Mwisho 

0 comments:

Post a Comment