Help Children
Love them
Saidia Watoto

Thursday, November 15, 2012

Barnaba aungana na mabalozi wa elimu katika kufanikisha ujenzi wa hosteli 30 za wasichana

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba akikaribishwa na Nancy Sumari

Mabalozi wa elimu nchini Nancy Sumari (kushoto) Faraja Kota (kulia) na Rebeka Giuni (katikati) wakijadiliana jambo

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba akiwa na mabalozi wenzake mara baada ya kujiunga nao

Mratibu wa blog  hii ya elimuboratanzania ambayo pia ni moja kati ya blog zinazodhamini Evance Ng'ingo akiwa na Barnaba

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa akisalimiana na na Barnaba

Waziri Kawambwa akifafanua jambo kuhusiana na matembezi ya hisani lakini pia alimkaribisha Barnaba katika kampeni hiyo

Ofisa wa TEA akimpatia kipeperushi Barnaba



Na Mwandishi wa elimuboratanzaniablog

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Barnaba ameungana na mabalozi wengine katika kuhamasisha ujenzi wa hosteli za wanafunzi wasichana.

Barnaba anaunga na Nancy Sumari, Faraja Kota na Rebeka Giuni katika kampeni hiyo inayolenga kukusanya bilioni 2.3 na kujenga hosteli 30 ambapo Barnaba atashiriki matembezi hayo.

Habari kamili 
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imeandaa matembezi ya hisani ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni 30 ya wanafunzi wa kike.

Matembezi hayo yataanzia katika eneo la Mlimani City kesho kuanzia saa moja hadi saa tano asubihi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mary Nagu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa alisema kuwa matembezi hayo ni moja kati ya harakati ya kuchangisha bilioni 2.3 kwa ajaili ya ujenzi wa mabweni hayo yatakayohudumia wanafunzi wa kike 1,504.

Alisema kuwa mikoa ambayo inahitaji mabweni hayo kwa wingi ni Mara, Kigoma, Rukwa, Tanga, Dodoma,Manyara, Lindi na Magu .

Alisema kuwa ni vema wananchi wakajitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za ujenzi wa mabweni hayo kwa kununua fomu za ushiriki ambapo alisema kuwa fomu zinauzwa kwa shilingi 20000/= katika ofisi za TEA.
“ Mimi naona kuwa hizi ni juhudi nzuri ambazo zinafanywa na hawa watu wa TEA kwa kushirikiana na mabalozi wetu mbalimbali  na kuna jukumu la kila mmoja wetu katika kuhakikisha kuwa wanafunzi hawa wanasaidiwa uhakika wao wa mahala pa kulala kwa kuwajengea hizi hosteli” alisema Waziri Kawambwa.

Lengo la serikali ni kujenga mabweni 100 kwa lengo la kuhudumia wanafunzi wa kike 4,800 nchini ili kuwanusuru na hatari ya kupata ujauzito wakiwa shuleni.
Mwisho

0 comments:

Post a Comment