Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, January 7, 2013

Tamasha la kuonja embe lilivyofana, limemalizika jana

Mwakilishi wa Kampuni ya Bakhresa Fransis Wambugu (kulia) akimkabidhi boksi la juisi mgeni rasmi ambae ni Mkurugenzi wa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Beatus Malema  (kushoto) zawadi hiyo ilikuwa ni inshara ya kuonesha bidhaa zitokanazo na  embe katikati mwenyekiti wa Amagro Burton Nsape .

Muda wa kuonja embe ulikuwa ni kama hivi


Hawa ni wadau wa shamba la Kilodede lililopo Mkuranga nao walikuwapo kuonesha bishaa zao za embe kama zinavyoonekana hapa chini

Hili ni shamba la mwenyekitti bwana Burton Nsape

Wadau wa shamba la Vikawe lililopo mkoa wa Pwani waliwaonjesha watu maembe yao hapohapo

Pi amiche mbalimbali ya miembe ya kisasa ilikuwapo ikiuzwa mahala hapo

waoneshaji walikuwapo wengi wa kutosha siku hiyo

Vikawe wakitoa maelezo kwa wananchi walioenda kufahamu ukulima wao wa embe

Na Mwandishi Wetu wa Elimuboratanzania aliokuwapo mahala hapo.



Embe ni moja kati ya mazao mengi ya  biashara ambayo yanaweza kuongeza pato la nchi iwapo likitiliwa mkazo katika kuandaliwa na kutafutiwa soko nje ya nchi.

Katika maonesho ya siku tatu yaliyoshirikisha wadau kadhaa wanaohusika na embe yaliyofanyika katika uwanja wa Mnazi Mmoja kuanzia jumamosi iliyopita hadi juzi kulikuwa na mengi ya kujifunza kuhusiana na embe.

Katika maonesho hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Wakulima wa Embe nchini (Amagro) yalihusisha wanachama zaidi ya 30  wa chama hicho ambapo walionesha aina mbalimbali za embe ambazo zinaweza kulimwa na kutumiwa kibiashara.

Mwenyekiti wa Amagro Burton Nsape akizungumza kuhusiana na namna ambavyo chama chake kinawasaidia wakulima wa embe kujipatia kipato kupitia zao hilo anasema kuwa Amagro hutoa elimu kwa wanachama wake.

Nsape anasema kuwa wakulima mbalimbali walikuwa wakilima na kuuza hadi nje ya nchi embe kw amuda mrefu ambapo anafafanua kuwa ni biashara nzuri na yenye faida kubwa.

Anasema kuwa Amagro inaendeleza harakati za kuwapatia wanachama wake elimu ya maarifa mbalimbal kuhusiana na ukulima wa zao hilo kama vile namna ya kudhibiti wadudu waharibifu, namna ya kufunga na kuhifadhi embe ikiwa pamoja na matumizi ya madawa na mbolea.

Anasema kuwa changamoto kubwa inayowakabili wakulima wa embe ni ukosefu wa usafirishaji wa kitaalamu kutoka mashambani hadi kuelekea kwenye soko kwa kuwa ili kuweza kuliweka embe katika ubora wake kuna mengi zaidi ya kuyafuata.

0 comments:

Post a Comment