Help Children
Love them
Saidia Watoto

Thursday, January 17, 2013

Kauli ya kuwa wasanii hawana elimu iliyotolewa na Bodi ya Filamu ilivyowakasirisha wasanii leo hapo Vijana Social Hall

Steve Nyerere akataka kuhakikisha kuwa wasanii wanaandamana kama ambavyo wanavyofanya Chadema kwa kuwa kwa kufanya hivyo ndio heshima itakuja kwao

Aisee kauli hiyo ilimkasirisha sana Mboto mpaka akataka kuhakikisha kuwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu kujiuzulu na kutaka awakome kabisa wasanii nchini




Ahaa!! Yani huyu mwanamama ndio anatuchanganya sisi yani hata Kikwete mwenyewe anatusadia lakini huyu anatukatisha tamaa yani sisi eti hatujasoma
Huyu alitaka kujua uwezo wa kazi wa bodi hiyo na iweje iwachanganye hivyo




Wasanii wa tasnia ya filamu na Maigizo nchini leo wameonesha kukerwa kwao na kauli iliyokuwa ikitolewa mara kwa mara na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Joycee Fisoo kuwa hawana elimu ya kutosha.

Wasanii hao kwa pamoja wameamua kuendesha maandamano ya kutaka mama huyo aachie ngazi ili kupisha mtu anayejua sanaa na kuwatetea maslahi yao .


Wakati huohuo wasanii hao wamepinga viwango vya malipo ambavyo vimewekwa na bodi ya filamu nchini vinavyotakiwa kulipwa na wasanii wa tasnia hiyo.

Wasanii hao waliokutuna juzi na jana katika ukumbi wa Vijana  Social Hall kwa pamoja walionekana kupinga viwango hivyo huku wengine wakisisitiza kuwa bodi hiyo imewasariti baada ya kuwasaidia.


Akisoma viwango mbalimbali kama vile ada ya ukaguzi wa mwongozo wa filamu (script) ambapo alisema kuwa kwa saa moja ni shilingi elfu 60 na kuongeza kuwa  iwapo zoezi hilo likichukua zaidi ya saa moja itawaumiza wasanii.

Alisema kuwa iwapo msanii atakuwa akitaka script yake hiyo isomwe haraka haraka basi itatakiwa alipie laki moja.

Alisema kuwa pia iwpao mwandaaji wa filamu akitaka kutumia wasanii kutoka  nchi za Afrika Mashariki atatakiwa kulipia 120,000/= huku wasanii wa kigeni wan je ya Afrika Mashariki watatakiwa kulipiwa dola 500.

Pia alisema kuwa kibali cha kutengeneza filamu imekuwa ni laki 5 huku kama mtayarishaji akiwa anataka kupewa kibali kwa haraka itabidi alipie milioni moja huku kama mtayarishaji ni mgeni kutoka nje ya nchi basi atatakiwa kulipia dola 3000.

Wakati Sangu akisoma maelezo hayo wasanii walikuwa wakizomea huku wengine wakitoa maneno ya kulalam akuwa viwango hivyo ni vikubwa.

Sangu aliendelea kuwasomea wasanii hao viwango hivyo ambapo aliwataarifu kuwa kubandika barabarani tangazo la kutangaza ni shilingi 5000 kwa tangazo moja.

Alisema kuwa adhabu zitakazotolewa kwa watu watakaokiuka taratibu hizo watatozwa faini za hapohapo ya milioni moja ikiwa pamoja na amri ya kusitisha utengenezaji wa filamu hiyo.

“ Mimi naona kuwa hii bodi inataka watu turudie hali zetu za wizi, kuzurura na tushindwe kupata hiki kidogo tunachokipata kwa sasa, na hii ni kinyume na Rais Kikwete atakavyo” alisema Sangu.

“ Yani kama ukipewa kibali cha kuitengeneza filamu kwa miezi mitatu ni shilingi laki tano lakini sasa iwpao miezi mitatu ikiisha na haujamaliza filamu yako basi itabidi ulipie tena laki 5 nyingine sasa hii ni adhabu na itapelekea watu kutengeneza filamu mbovu zisizokuwa na umuhimu” alisema Sangu.

Mbali na hayo lakini pia Sangu aliendelea kuishutumu bodi hiyo huku akiendelea kutupa lawama za wasanii hao kwa Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Joyce Fisoo kuwa amekuwa akiwakejeli wasanii kuwa hawana elimu.

Kufuatia kauli hiyo wasanii walipandwa na jazba huku wengine wakianza kutoa lawama zao kwa katibu mtendaji huyo kuwa anatakiwa kujiudhulu.


Wasanii waliotoa mawazo yao ambao ni Cloud, Mpoto na wengineo walisikika kwa pamoja wakisisitizia kuwa katibu huyo ajiudhulu haraka iwezekanavyo na kusisitiza kuwa wataandamana kusisitiza jambo hilo.

Tunaendela na juhudi za kumtafuta mama Fisoo na tutawajaurisha muda si mrefu 




0 comments:

Post a Comment