Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, April 14, 2013

Yaliyojili UDSM katika mjadala wa elimu

Mjadala uliomalizika sasa hivi katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kuhusiana na masuala ya elimu ambapo kulikuwa na mjadala unaojadilia mstakabali wa elimu yetu hapa Tanzania kuhusiana na namna ya kuuboresha.

Mtandao huu ulikuwapo eneo hilo ambapo unakuletea yale yaliyojili.

Kulikuwa na hoja ambayo ilikuwa ikitaka matumizi ya kiswahili yatumike kufundishia kuanzia elimu ya msingi hadi vyuo vikuu ambapo mjadala huu ulipingwa na wengine waliuunga mkono.

Pia kulikuwa na watu ambao walisema kuwa eti kuna wanafunzi wa vyuo vikuu wanahitimu kwa kupewa Degree za chupi ambapo wanafunzi wa kiume wanawatumia wanafunzi wa kike kujipatia degree za chupi kutoka kwa wakufunzi.

Professor  Azaveli Lweitama alilalamikia matumizi ya lugha ya kiswahili ambapo alisema kuwa kuna dalili za utaaila kutokana na kusisitizia matumizi ya lugha ya kiingereza shuleni.

Kesho tutawaletea mengine zaidi

0 comments:

Post a Comment