Help Children
Love them
Saidia Watoto

Saturday, April 20, 2013

Mwanafunzi aliyepua watu huko Boston Marekani aliyekuwa hajakamatwa sasa kashakamatwa

                                                        Huyu ndo alikuwa amebakia

HATIMAYE MTUHUMIWA WA PILI WA MIRIPUKO YA BOSTON ATIWA MBARONI


Mshukiwa wa mwisho katika utegaji wa mabomu yaliyowauwa watu 3 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 180 katika mbio za Marathon za Boston amekamatwa akiwa ndani ya boti. Polisi imesema kuwa amepelekwa hospitali akiwa mahututi.

Kukamatwa kwa mtu huyo Dzhokhar Tsarnaev, mwenye umri wa miaka 19 kumehitimisha operesheni kubwa ya siku nne, na kumekuja siku moja baada ya shirika la upelelezi la Marekani FBI kuchapisha picha za washukiwa hao.

Mshukiwa mwingine, Tamerlan Tsarnaev mwenye umri wa miaka 26 na ambaye ni kaka wa Dzhokhar, aliuawa jana Ijumaa katika majibizano ya risasi na polisi.

Kaka waripuaji: Tamerlan Tsarnaev (Kushoto) na mdogo wake Dzhokhar
Tamerlan Tsarnaev (Kushoto) na mdogo wake Dzhokhar

Umati wa watu katika mji wa Boston ulishangilia kwa shangwe baada ya kuibuka kwa ripoti ya kukamatwa kwa mshukiwa huyo. Shughuli zote katika mji huo zilikuwa zimesimamishwa wakati operesheni ya kuwasaka vijana hao ilipokuwa ikiendelea.

Bado yapo maswali yasio na majibu
Akizungumza muda mfupi baada ya kukamatwa kwa Dzhokhar Tsarnaev, rais wa Marekani Barack Obama alisema kukamatwa kwa mshukiwa huyo ilikuwa hatua muhimu katika mkasa unaohusu miripuko ya Boston.

Hata hivyo, Obama alisema kuwa bado yanabakia maswali yasio na majibu, ambayo ni pamoja na sababu iliyowafanya vijana hao kufanya mashambulizi, na ikiwa walikuwa na msaada katika uhalifu wao.

''Tutatathmini kilichotokea, na tutachunguza kama magaidi hawa walikuwa na washirika, na tutafanya chochote kinachohitajika kuhakikisha usalama wa watu'', alisema rais Obama.

Mripuko kwenye mbio za Marathon za Boston iliuwa watu 3 na kujeruhi zaidi ya 180

Polisi mjini Boston wamesema kuwa watu wengine watatu wamekamatwa na wanahojiwa kwenye nyumba aliyoishi Dzhokhar Tsarnaev karibu na chuo kikuu cha Massachusetts.

This image obtained April 19, 2013 courtesy CBS News shows Dzhokhar Tsarnaev, a suspect in the Boston Marathon bombing who was captured Friday night, April 19, 2013 after he was found hiding in a boat in a Boston suburb
Polisi wamesema walikuwa wakianza kukata tamaa katika operesheni yao, hadi pale walipopigiwa simu na raia ambaye ameiona damu kwenye boti yake, na kumkuta mshukiwa ndani ya boti hiyo akiwa ametokwa na damu nyingi.

Hisia kali dhidi ya Marekani
Watuhumiwa hao wametambuliwa kuwa ni jamii ya Chechen kutoka kusini mwa Urusi, ambao inaaminiwa wamekuwa wakiishi Marekani kwa muda wa miaka 10. Jimbo la Chechnya limeshuhudia vita viwili vikubwa tangu mwaka 1994, baina ya Urusi na wapiganaji wanaotaka kujitenga kwa jimbo hilo.

Kaka mkubwa Tamerlan anasemakana alikuwa na maoni makali dhidi ya Marekani, akiishutumu nchi hiyo kutumia Biblia kama kisingizio kuzivamia nchi nyingine.

Kabla ya kukamatwa kwa mdogo wake mji wa Boston ulikuwa umepooza, baada ya utawala kufunga barabara zote na kuwashauri wenye biashara kuzifunga. Hali kadhalika wakazi milioni moja wa mji huo na vitongoji vyake walikuwa wameombwa kubakia ndani ya nyumba zao, na kufungua mlango tu kwa maafisa wa polisi waliovali

0 comments:

Post a Comment