Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, April 16, 2013

Wanafunzi 1600 Urambo hawajaripoti Shuleni


WANAFUNZI  1,605 sawa na asilimia 35 ya waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka huu katika Wilaya ya Urambo, mkoani Tabora, wameshindwa kuripoti shuleni.

Ofisa Elimu Sekondari, wilayani  Urambo, Grace
Monge, alisema idadi hiyo ambayo hawajajiunga na masomo, ni sehemu ya wanafunzi 4,604 waliochaguliwa kujiunga na sekondari mwaka huu.
Alifafanua kwamba kati ya hao ambao hawajajiunga, wavulana ni 805 na waliobaki ni wasichana.

Kwa mujibu wa Ofisa Elimu, miongoni mwa sababu za wanafunzi kutoripoti ni baadhi yao kuolewa mapema,
kukosa ada na mahitaji muhimu yanayotakiwa shuleni kutokana na umasikini wa wazazi.

Sababu nyingine ni wazazi kuwatumikisha watoto wao katika
shughuli za kilimo hasa tumbaku na wengine kuwazuia ili waongeze nguvukazi katika kilimo.

0 comments:

Post a Comment