Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, April 9, 2013

"Mkiwa field mzingatie maadili"


WANAFUNZI wa vyuo mbalimbali nchini  wametakiwa kuhakikisha wanafuata maadili, taratibu na sheria wakati wanapoenda kufanya kazi kwa vitendo (Field) katika taasisi mbalimbali.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa viwango vya Elimu na Ustawi wa Jamii Tanzania (TESWEP) Dk. Naftal Ng’ondi, ambaye pia ni Mhadhiri wa chuo cha ustawi wa jamii, katika warsha ya wahadhiri.

“Wahadhiri nyinyi ndiyo mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wanafunzi wenu huko vyuoni kuhusu sheria na maadili kwani kutokana na kukua kwa Teknohama, wanavyuo wamekua wakishindwa kufuata miiko katika jamii,” alisema Ng’ondi.

Alisema katika utafiti wa TESWEP umegundua kuwa katika makampuni mbalimbali wanavyuo wengi wanaokwenda kujifunza kwa vitendo wamekuwa wakikiuka taratibu zilizowekwa na taasisi husika na mwisho wa siku chuo husika kinalaumiwa kwa kutofundisha maadili kwa wanafunzi.

 "Hawaheshimu waajiriwa wala muda wa kufika kazini hauzingatiwi jamani hali hii inatoa taswira mbaya sana katika vyuo vyetu hivyo inabidi tuwaelimishe vya kutosha, unakuta mvulana anashusha suruali 'mlegezo' na mwanamke naye anavaa sketi fupi 'kimini' wabadilisheni|” alisema mwenyekiti huyo.

 Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo hayo Furaha Dimitrios, amesema jamii yoyote isiyokuwa na maadili ina hatari kubwa hasa katika kipindi hiki cha ulimwengu huu wa sayansi na Teknologia.

 "Sisi sote tunajua kuwa maendeleo ya jamii kwa sasa ni makubwa hivyo yatupaswa kukabiliana nayo kwa kuwa utandawazi ni mpana zaidi na wanafunzi wanatambua mambo mengi zaidi,” alisema Dimitrios
Pia aliwataka wanafunzi wanapoenda kufanya mafunzo kwa vitendo wajue kuwa ni maandalizi ya kazi wanayotarajia kwenda kufanya hivyo ni jukumu lao kuvumilia na kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo.
mwisho



0 comments:

Post a Comment