Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, April 16, 2013

Mwalimu akutwa kafa



MWALIMU wa Shule ya Atlas,Elizabeth Mbaga (22) mkazi wa Kimara Baruti amekutwa amekufa chumbani kwake na mwili wake ukiwa hauna jeraha lolote.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema mwili ulikutwa juzi saa 11:30 jioni. 

Ingawa Polisi imesema chanzo cha kifo hakijafahamika, taarifa kutoka kwa jamaa na majirani, kabla ya kubainika amekufa chumbani, jana yake usiku alitoka na rafiki yake wa kiume na haikufahamika walikokwenda. 

 “Juzi (Jumapili) usiku waliondoka hapa na mpenzi wake mwenye asili ya Kiasia. Lakini muda mfupi kabla ya kuondoka kulikuwa na kutoelewana,” alisema mmoja wa majirani ambaye hakutaka jina lake litajwe. 

Aliendelae kusema, “Hatukumuona mpaka walimu wenzake walipokuja jana hapa nyumbani na kukuta mwili wake kitandani huku mlango ukiwa umeegeshwa,” alisema mmoja wa majirani ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
  
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Shule ya Atlas, Zana Rugambwa, baada ya mwalimu huyo kutoonekana shuleni Jumatatu huku simu yake ikiwa haipatikana, walimu wenzake waliamua kumfuata nyumbani kwake na kukuta amefariki dunia. 

Mwili wa mwalimu huyo ambao umehifadhiwa hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi, unatarajiwa kuagwa leo katika shule ya Atlas Madale kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Arusha.

0 comments:

Post a Comment