Help Children
Love them
Saidia Watoto

Tuesday, April 16, 2013

"Rudisheni shule za wasichana za Mtwara na Masasi" Wananchi




WABUNGE wanaotoka mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara wametakiwa kutetea haki za watoto ikiwemo kuishauri Serikali kurudisha shule za wasichana za Mtwara na Masasi  zitoe elimu kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne badala ya kidato cha tano na sita.

Hayo yalisemwa juzi na  mmoja wa washiriki kutoka Kanda ya Kusini, Bibiana
Mmoro wakati wa kongamano la Kitaifa la Wanawake, lililoandaliwa na Muungano wa Mashirika ya kutetea masuala ya jinsia lililomalizika jana mjini Dodoma.

Mmoro alisema kuwa, shule hizo mbili zilikuwa zikisaidia kwa
kiasi kikubwa kupokea watoto wa Kusini  lakini baada  ya kubadilishwa kuwa
kidato cha tano na sita wengi wanaochaguliwa wanatoka nje ya Kanda ya
Kusini.

Pia, alitaka wabunge kutetea haki za watoto kwa kuhakikisha kila wilaya
inakuwa na shule moja ya bweni ili kuwapa fursa wanafunzi wengi wa kike
kupata elimu bora.

Mbunge wa Viti Maalumu Agnes Hokororo (CCM) alisema masuala ya siasa
yamekuwa yakirudisha nyuma maendeleo kwa wananchi kupiga vita baadhi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

0 comments:

Post a Comment