Help Children
Love them
Saidia Watoto

Thursday, March 14, 2013

Mwanafunzi kupelekwa China na Tigo


Mratibu wa michezo ya Bahati Nasibu kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania Bakari Maggidi (kushoto) akiangalia majina ya watu waliokuwa wakishindanishwa katika bahati nasibu ya Ascend Y200 iliyochezeshwa na Tigo, katikati ni Meneja wa Bidhaa wa Tigo William Mpinga na kulia ni ofisa kutoka Tigo David Semkwao (Picha na Mpiga Picha Wetu)

 Na Mwandishi Wetu
 MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu
Kishiriki Cha Afya cha mkoani Kilimanjaro (KCMC) Fredy Mgaya ni mmoja kati ya washindi wawili walioshinda bahati nasibu ya Ascend Y200 iiliendeshwa inayoendeshwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo.

Mwingine aliyeshinda ni David Semkwao ambae ni msanifu wa majengo mkazi wa Ubungo ambapo washindi wote hao wanapata nafasi ya kuelekea nchini jijini Beijing nchini China kwa matembezi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kuchezesha bahati nasibu hiyo, Meneja wa Bidhaa wa Tigo, William Mpinga alisema kuwa washindi hao watalipiwa gharama zote kuanzia tiketi za ndege, maradhi na fedha za kujikimu wakiwa chnini humo.

Alisema kuwa wakiwa nchini China watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii kama vile ukuta wa Beijing na maeneo mengine muhimu.

Alifafanua kuwa Tigo inaendelea na kampeni yake bahati nasibu hiyo ambayo ni maalum kwa wateja watakaonunua simu aina ya Ascend Y200.

Wakizungumzia ushindi huo washindi walioshinda bahati nasibu hiyo ya jana waliwasihi watu wengine nao kujitokeza kununua simu hizo ili waweze kushinda bahati nasibu hizo.
Mwisho


0 comments:

Post a Comment