Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, March 10, 2013

Modesta Mahiga atoa somo siku ya wanawake duniani

 

Picha ya juu kabisa ni mfanyakazi wa Benki hiyo ya Ecobank akicheza muziki katika maadhimisho hayo,  picha ya katikati ni mwanadada mhamasishaji wa masuala ya haki za vijana, wanawake na masuala ya elimu Modesta Mahiga


Ikafuata muziki kutoka kwa wafanyakazi wa benki hiyo na wageni waalikwa
 Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Temeke ndio alikuwa mgeni rasmi siku hiyo

    Wafanyakazi wa benki ya Ecobank wakifuatilia somo lililokuwa lilitolewa na Modesta Mahiga


Bi Abellalulu Sultan ndio alipewa zawadi kuwa ni mfanyakazi mwenye umri mdogo zaidi katika benki hiyo
                                                        Happy Workers

                                             CEO wa Ecobank Enoch Osei-Safo akitosi na wageni


                                            Zawadi kibao zikiendelea kutolewa.

Habari Kamili.


Mwanaharakati Mjasiriamali hapa nchini Modesta Mahiga amewataka wanawake wenye mafanikio na wanaoshikilia nafasi za uongozi katika ofisi mbalimbali kuwaendeleza walio chini yao.

Modesta alisema hayo juzi wakati alipokuwa akizungumza kuhusiana na namna ambavyo wanawake wanaweza kujiimarisha katika ngazi za uongozi.

Alisema kuwa wanawake wenye madaraka wanatakiwa kutambua kuwa kwa kuwaendeleza wafanyakazi wa chini yao ndio wanakuwa wamejiimarisha zaidi katika nafasi zao hizo.

Alisema kuwa kwa kuwaendeleza na kuwasaidia wanawake wa chini yao wanakuwa wana uhakika kwa kupata watu wa kuwasaidia kazi iwapo wao wanakuwa hawapo kazini kwa dharura au likizo.

" Mimi najitolea mfano mimi mwenyewe kuwa kwa kipindi ambapo nakuwa sipo ofisini naweza kukuta kuwa kumbe wale niliowaacha nimewajengea misingi ya kujiamini na kufanya shughuli kama inavyotakiwa, sasa kama nisingekuwa nimefanya hivyo si ndio ningekuta kila kitu kimeharibika"alisema Modesta.

Katika hafla hiyo iliyoandaliwa na benki ya Ecobank pia wafanyakazi walipewa zawadi mbalimbali ambapo mwanadada Abellalulu Sultan pamoja na Catherine Uliwa walipewa zawadi kuwa wafanyakazi wadogo zaidi katika benki hiyo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa  benki ya Ecobank Enoch Osei-Safo alisema kuwa benki hiyo itaendelea kuwasaidia wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi katika benkiu hiyo.

Alisema kuwa kwa sasa asilimia 40 ya wafanyakazi ni wanawake na kuongeza kuwa bado kuna mikakati mingi ya kuwasaidia wanawake hao.

0 comments:

Post a Comment