Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, March 10, 2013

Maya Azucena afundisha kutetea haki za wanawake kwa njia ya muziki

Msanii Maya Azucena akiimba sambamba na mratibu wa onesho hilo Chedi Guru Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya MegaMark Entertainment iliyoratibu ziara hiyo

                                                     
Maya akiwatambulisha wasanii wa kundi la Bendi ya Wa Kwetu waliokuwa wakimpigi avyombo vya muziki siku hiyo.
                                              Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa Ubalozi wa Marekani Dana Banks akifuatilia onesho hilo, Ubalozi wa Marekani ulidhamini ujio wa mwanamuziki huyo ambapo ziara hiyo ni ilikuwa sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Marekani Maya Azucena akiimba wakati wa onesho lake lililofanyika juzi katika ukumbi wa Trinity Masaki.


Mmoja kati ya washabiki wa muziki ambao walipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao katika onesho hilo, akiimba na kushabikiw ana wapenzi wa burudani waliojitokeza siku hiyo.

 

Habari Kamili

MSANII wa muziki ambae pia ni mwanaharakati wa haki zwanawake kutoka nchini Marekani Maya Acuzena juzi alifanya onesho la kuvutia lililobeba ujumbe wa kuhamasisha haki za wanawake.

Maya ambae yupo hapa nchini kwa uratibu wa kampuni ya Matangazo bna Burudani ya MegaMark ambayo imemleta msanii huyo hapa nchini kwa mara ya pili.

Onesho hilo la Maya lilifanyika katika ukumbi wa Trinity ambapo alikuwa akiimba muziki wa moja kwa moja (Live) huku akisaidiwa na bendi ya Wa Kwetu ambayo ilikuwa ikipiga vyombo mbalimbali vya muziki.

Maya alionesha uwezo wa hali ya juu katika kumiliki jukwaa, kuimba, kucheza huku akiwashirikisha kikamilifu wapenzi wa burudani waliohudhuria siku hiyo.

Maya alikuwa pia akitoa ujumbe kuhusiana na haki za wanawake na pia alitumia muda wake mwingi kuzungumza na washabiki wake siku hiyo huku akiwapatia nafasi wasanii chipukizi kuimba nae jukwaani.

Mmoja kati ya wasanii wa juu ambao nao waliweza kuonesha uwezo wa kuimba na kutumia jukwaa ni Linah Sanga wa Tanzania House of Talent (THT) ambae pia alimvutia Maya.

Maya akiwa hapa nchini ametembelea mashirika mbalimbali ya haki za wanawake, watoto pamoja na wadau wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.

 



0 comments:

Post a Comment