Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, March 4, 2013

Mama Tery azindua reality show yake inayoelimisha masuala ya Uhalifu


Mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto Tery Gbemudu, Mama Terry, akiagana na Rais Mstafaau wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi juzi wakati wa uzinduzi wa kipindi cha luninga cha kiitwacho Pamoja Tunaweza cha Mama Terry.

Mdau wa elimubora
MWANAHARAKATI wa muda mrefu katika masuala ya haki za wanawake pamoja na mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi, Tery Gbemudu, Mama Terry, amezindua kipindi chake cha Luninga kiitwacho Pamoja Tunaweza chenye kuendeleza mapambano dhidi ya uhalifu.

Kipindi hicho kilizinduliwa juzi na rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi katika bwalo la Police Officers Mess lililopo Oysterbay, Dar es salaam na kudhuriwa na wakuu mbalimbali wa jeshi la Polis aliwamo Inspekata Jenerali Said Mwema.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzinduzi huo Mama Tery alisema kuwa kipindi hicho kitakuwa kikirushwa katika stesheni ya TBC mara mbili kwa wiki.

Alisema kuwa kipindi hicho kinalenga kuwafundisha wanajamii namna ya kuepuka na kupambana na uhalifu ambao unaonekana kuwa unazidi kuota mizizi hapa nchini.

Alisema kuwa ili kuweza kuieleimisha jamii ya sasa masuala mbalimbali ya kupambana na uhalifu ni lazima uwafuate katika misingi ya kisasa ambapo anaona kuwa kwa kutumia kipindi cha Luninga ni njia mojawapo ya kuwafikia kirahisi.

Alisema kuwa kipindi hicho cha dakika 90 kinagusa nyanja zote za ulinzi na usalama ambapo wanahojiwa watu wa mitaani kuhusiana na wanavyoathiriwa na uhalifu lakini pia kunakuwa na watu ambao watakuwa studio wakihojiwa na kufafanua hoja mbalimbali kuhusiana na uhalifu.

“ Kwa hiki ni kipindi cha kurekodi ambapo watu mbalimbali wanahojiwa na kueleza ulewa wao wa masuala ya uhalifu lakini pia kunakuwa na wau ambao wanafafanua uhalifu huo kiundani na kuangalia namna ya kuwasaidia wote kiujumla” alisema Mama Terry.

Akisoma hotuba ya Rais Mstaafu Mwinyi ambae alifika kweye eneo hilo lakini alipata udhuru, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meki Sadik alisema kuwa kipindi hicho kitakuwa ni chachu yamabadiliko.

Alisema kuwa katika jamii ya sasa iliyobadilika na kuathiriwa na utandawazi inatakiwa kuwepo na watu ambao wanabuni njia za kisasa za kuelimisha mapambano dhidi ya uhalifu.

Kipindi hicho pia kinaendeshwa kwa msaada wa jeshi la Polis ambapo IGP Mwema amempatia ofisi katika bwalo hilo la Police Officers Mess ambayo Mama Tery anaitumia kufanyia kazi zake kurekodia pia.
Mwisho

0 comments:

Post a Comment