Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, March 4, 2013

Mbunge Vicky Kamata apatiwa msaada wa kusaidia elimu katika Vicky Kamata Foundation

Hapa akijadiliana jambo na wadhamini wake kabla hawajampatia msaada huo

Akiingia ukumbini

Akila chakula na watoto wake

Akiwa na wakurugenzi wa Taasisi yake

Kwa sababu yeye ni msanii basi aliimba na watoto wake hao wimbo ulitia huruma sana

Akipokea msaada huo kutoka kwa kampuni ya Sayed Corporation LTD

Hapa ni wakati akiagana na mgeni rasmi ambae alikuwa Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Husein Mwinyi

Hapo akipokea baiskeli zenyewe

Akatoa hotuba yake makini

Mmoja kati ya wakurugenzi wa taasisi hiyo akizungumza

Akiagana na ofisa kutoka ubalozi wa Pakistan

Group picha




Group picture na watoto wa kituoni








WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hussein Mwinyi juzi alikabidhi hundi ya shilingi milioni 10 pamoja na baiskeli 30 kwa Taasisi ya Vicky Foundation inayomilikiwa na Mbunge wa Viti Maalum Vicky Kamata.

Akikabidhi msaada huo uliotolewa na kampuni ya Sayed Corporation LTD Mwinyi alisema kuwa serikali inatambua na kuheshimu juhudi zinazofanywa na makampuni pamoja na mashirika mbalimbali katika kusaidia jamii.

Alisema  kuwa suala la watoto wa mitaaani, yatima pamoja na kuwasaidia wajane ni suala muhimu ambalo linahitaji ushirikiano wa dhati kutoka kwa wanajamii na mashirika kama anavyofanya Mbunge Vicky Kamata.

Naye Mbunge huyo alisema kuwa msaada huo ni muhimu kwake kwa kuwa unawasaidia watoto kadhaa wanaolelewa na Taasisi hiyo.

Alisema kuwa ana watoto walemavu, watoto yatima pamoja na wenye mahitaji maalum ambapo alisema kuwa msaada huo unaweza kusaidia katika kupunguza changamoto kadhaa zinawazowakabili.

“ Hii Taasisi yetu makao makuu yake yapo mkoani Geita na tumekuwa tukikabiliwa na changamoto mbalimbali ambapo kwa sasa tunaona kuwa kuna mwanga mkubwa mbele yetu ambao tunatakiwa kuupata na ili kuupata mwanga huo ni vema tukashirikiana watu wote kwa pamoja” alisema Vicky.
Mwisho

0 comments:

Post a Comment