Help Children
Love them
Saidia Watoto

Sunday, August 11, 2013

Watanzania jiandaeni kwa mchongo huu wa masomo kutoka Japan


SERIKALI ya Japan imeahidi kutoa mafunzo kwa watanzania 1000 kuanzia januari mwakani kuhusu nishati ya geothermal power ili kuwezesha kuwa na wataalam wa aina hiyo.

Kadhalika  japan itachangia kuendeleza miundombini ya Tanzania kama uzalishaji wa nishati pamoja na kuchangia  kuongeza ajira na kujenga uwezo.


Aidha Tanzania imewaomba kufufua chuo chao cha teknolojia ambacho kitawezesha kupata wataalam wengi wa uhandisi.


Waziri wa uchumi,biashara na Viwanda wa Japan, Toshimitsu Motegi alisema hayo jana dare s salaam katika mkutano wa kibiashara baina ya Tanzania na japan uliowakutanisha wafanyabiashara zaidi ya 200 na makampuni ya biashara zaidi ya 25 kutoka japan.Waziri huyo  nimara ya kwanza kufanya ziara nchini.


Akizngumza katika mkutano huo, Motegi alisema katika kuimarisha biashara amekuwa akijadili namna  ya kuwapata wataalam ambapo Japan itachangia kutoa mafunzo katika mradi huo ambao utaanza januari.


“katika mkutano huu wapo wafanyabiashara wawakilishi kutoka japan na Tanzania ambao tunapenda kushirikiana katika masuala mbalimbali,”alisema Motegina kuongeza kuwa juzi alikutana na waziri wa nishati na madini, Sospeter muhongo na kujadili namnaya kuendeleza wataalam wa geothermal power.


Alisema katikamajadilinao hayo walikubaliana kuanza mafunzo hayo januari mwakani ambapo watatekeleza mradi huo katika kuwafunza watanzania kuwa wataalam wa nishati hiyo.


Motegi alisema pia japan inazungumzia namna yakuchangia kujenga miundo mbinu afrika kupitia sekta binafsi ambapo hata rais Jakaya Kikwete amekuwa akisisitiza jambo la muhimu ni miundo mbini ili kufikia maendeleo nchini.


Kadhalika alisema japan inachangia katika kuongeza ajira pamoja nakuwajengea watanzania uwezo ambapo lengo lao ni kuongeza ajira kupitia makampuni ya kijapani kutoka ajira 200,000 hadi 400,000 katika miaka mitano ijayo.


Awali akizungumza, waziri wa viwanda na biashara, Dk.abdallah kigoda alisema serikali imewaomba wajapan kufufua chuo cha teknolojia haswa kuwasaidia wahandisi ambapo walikubali.
“chuo hicho kilikuwepo nchini miaka ya 1981 na kilikufa 1986 ambapo wajapan wamekubali kukifufua katika kuongeza wataalam pamoja na ajira,” alisema Kigoda.


Alisema wamekubali pia kuboresha reli yakati nchini na wataanza kufanya  utafiti ilikuona jinsi watakavyoboresha.


Kadhalika kigoda alisema katika kuongeza ajira japan imekubali kuanza utaratibu wa kuunganisha pikipiki haswa Honda pamoja na kuendelea kuimarisha viwanda nchini.


Akizungumza katika mkutano huo,waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,benard membe alisema ni muhimu kuwa na mikutano wa aina hiyo kwa kuwa inawaanda watanzania kiakili kuondokana na uchumi wa kijamaa na kwenda katika soko ambao pia utaongeza ajira.
Alisema hata rais jakaya kikwete amepongeza mkutano huo na kutilia mkazo katika kukuza miundombinu ya reli na kupanua bandarii.
mwisho

0 comments:

Post a Comment