Help Children
Love them
Saidia Watoto

Friday, August 2, 2013

Mwanafunzi awakilisha vema Tanzania huko Marekani ashinda shindano la dunia la kurika kamba

Akitambulishwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Michezo bwana Dennis kwa waandishi wa habari

Hapa kazi ilianza ya kucheza

Akionesha manjonjo yake


Picha ya pamoja na wadau wa mchezo huo

Mkurgenzi wa Maendeleo ya Michezo akizungumza na Mama anaemlea Kondo huko Marekani

Mimi (kushoto) Kondo na mwandishi wa Nipashe

Akiwa na mdhamini wake

Wdsau wakipiga nae picha huyo mama wa kizungu ndo alimlea

Timu aliyoenda nayo huko Maekani lakini hawa walitokea hapa hapa bongo

Anaruka balaa




Na Evance Ngingo
KIJANA Khamis Kondo (14) ameshinda michuano ya dunia ya kuruka kamba iliyofanyika nchini Marekani Julai 5 hadi 13 nchini Marekani.

Shindano hilo lilishirikisha nchi 14 pamoja na timu 44 ambapo wachezaji walikuwa 480.

Akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jana Kondo alisema kuwa alikuwa akitumia saa tano kujifua katika kituo cha Seattle Jump kilichopo Seattle nchini Marekani.

Alisema kuwa akiwa kwenye mashindano hayo alitumia mbinu mbalimbali za kucheza mchzo huo hali iliyopelekea ushindi wake.

" Kutokana na kujifua kwa miezi sita kwenye kituo hicho nilipata ujuzi wa kujua namna ya kucheza mchezo huo wa aina yake na ndio nikajikuta ninaliletea taifa langu ushindi mkubwa kama huu" alisema Kondo.

Alisema kuwa kila siku baada ya kutoka shule ya Amy Canady anayosoma nchini humo alikuwa akirudia kwenye kituo hicho na kujifua chini ya uangalizi wa mwalimu wake.

Kondo alishiriki na washiriki wengine waliotokea moja kwa moja katika kituo cha dogodogo Center ambao ni Joshua John, Emanuel Joseph, Athuman Sungi na Furaha Mwakisyala.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kituo Cha Michezo Tanzania, Dennis Makoi ambae kituo chake kilishirikiana na Dogodogo Center alipikuwa akilelewa Kondo alisema kuwa ushindi wa Kondo umepelekea kituo chake kupatiw amisaada ya kimichezo.

Alisema kuwa kituo hicho baada ya kumuona kijana huyo akishinda kwenye mashindano ya kuruka kamba ya nchini Kenya mwaka 2010 kiliamua kumuombea udhamini nchini Marekani kwenye kituo cha mafunzo cha Seattle Jump.

Alisema kuwa ushindi alioshinda ni katika michuano iliyofanyika Julai 5 hadi 13 mwaka huu na kushirikisha washiriki kutoka nchi 14 huku kukiwa na timu 44 na wachezaji zaidi ya 300.

"Hii ni hatua nzuri na ya kimafanikio kwa kuwa hata hapo kituoni nchini Marekani anapojifunza amewashinda hata wanafunzi wenzake waliojitokeza kushiriki mchezo huo wa aina yake sasa hiki ni kipaji ambacho tunatakiwa ujivunia na kukiendeleza." alisema Makoi.

Pia Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Idara ya Michezo iliyopo kwenye Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo nchini Juliana Yasoda alitoa wito kwa wadau wa michezo kuwekeza kwenye mchezo huo.

Yasoda alisema kuwa michezo ambayo sio maarufu kama huo wa kuruka kamba ni moja kati ya michezo ambayo inaweza kuwekezwa na kulisaidia taifa kufikia katika ngazi ya kimataifa.

Alisema kuwa kwa hatua ya mshindi wa dunia wa mwaka huu wa mchezo wa kuruka kamba kushinda huku akiwa na miaka 14 ni inashara nzuri kuwa mchezo huo unaweza kulitangaza taifa.

" Sasa kama huyu akiwa na miaka 14 na amejifunza kwa miezi sita tu nchini Marekani kucheza mchezo huu basi inamaana kuwa anaweza kufika mbali hasa mwakani kwenye Olimpiki ambapo mchezo huu utakuwapo" alisema Yasoda.
Mwisho


0 comments:

Post a Comment