Help Children
Love them
Saidia Watoto

Monday, August 5, 2013

Inasikitisha wanafunzi wabakwa kwa muda mrefu huko Sumbawanga


WANAFUNZI  wa kike  wanaosoma  katika Shule ya Sekondari  Mzindakaya
kijijini  Kaengesa  wilayani  Sumbawanga mkoani  hapa   wamekiri kufanyiwa
visa  vya  udhalilishaji  mara kwa  mara   muda mrefu sasa  lakini  wamekuwa
wakiona  aibu  kuripoti  visa  vya ubakaji  wanavyofanyiwa  kwa uongozi wa
shule pia kwa  wazazi  wao .

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi  hivi karibuni  umebaini
kuwa  wanafunzi  hao  wa kike  ambao  wanapanga  vyumba katika  nyumba
ambazo  ni mbovu  wamekuwa  wakibakwa  mara kwa  mara  na watu  ambao  wao
wenyewe  wanadai  ni  vijana  maarufu kama ‘wezi  wa mafuta ‘  waliozagaa
kijijini  humo kutoka maeneo  mbalimbali   mkoan  humo  wakishirikina
na  baadhi
ya wakazi  wa kijiji  hicho .

 Vijana  hao  ambao  wanadaiwa  kujihusisha  na  wizi  wa mafuta  ya
kuendeshea  magari na mitambo kutoka katika  Kampuni  ya Ujenzi wa barabara
ya  kutoka  mjini mdogo wa Laela  mpaka  Sumbawanga mjini  kwa kiwango  cha
lami .

 Uchunguzi  huo   umebaini  kuwa  wengi wa wanafunzi  hao  wa kike
wamelazimika  kupanga  vyumba  kwa bei  ya kutupa  ya sh 1,000-  kwa mwezi
kutokana  na  wazazi  wao  kukataa  kuchangia gharama  ili  watoto wao  hao
waweze kuishi  katika mabweni   mawili yaliyopo  shuleni  hapo  ambapo  sasa
yamelazimika  kubakia tu   wazazi  hao wakidai  kuwa  ni  maskini .

Baadhi  ya wanafunzi  hao  wa kike  waliohojiwa  na mwandishi wa  habari
hizi  hivi  karibuni  shuleni  hapo  walikiri  kukumbwa mara kwa  mara na  visa
vya kubakwa  lakini  wanaogopa pia kuona aibu  kutoa  taarifa kwa mamalaka
husika  hivyo  wamebakia  kukaa kimya na  kujiuguza  kisirisiri .

“Wengi wetu  hatujui hatima yetu  kwani tunaishi  kwa hofu  kubwa hususani
ifikapo  usiku  tunakosa  raha  licha  ya kwamba   kila mmoja  wetu
amepanga  chumba  lakini  kutokana na visa  vya kubwaka  mara  kwa mara
tumeamua  kulala  chumba kimoja  wasichana  kati  ya  watatu hadi  sita .

Tatizo  ni wazazi  wetu  hawataki  tuishi  katika  mabweni shuleni  eti  wao
ni maskini hawawezi  kuchangia gharama za sisi kuishi    bwenini ..... tuna
hofu kubwa basi tu kwani  tunabakwa lakini  hatuwezi   kusema  tunaona  aibu
......” alisema mmoja  wao.

Mwandishi  wa  habari hizi  hivi  karibuni  alitembelea  baadhi  ya  nyumba
walizopanga  watoto hao  wa kike  na  kushuhudia  zikiwa katika hali  mbaya
zingine zikiwa  hazifai  kuishi  binadamu  kwani hazina  vyoo  wala  sehemu
ya kupikia  chakula  pia  hazijazungushiwa kuta  kwa ajili  ya usalama
 wa  wapangaji
wa nyumba  hizo .

“Kama  unavyoona  nyumba   choo  kilichopo  ni  kibovu  hakina  hata  mlango
 na kiko  nje  mita kadhaa kutoka  katika nyumba hii  hivyo kutokana na
hofu ya kutoka  nje  kuijisaidia   wakati  wa usiku  tunalazimika
kujisaidia  kwenye makopo  tunayoyahifadhi  vyumbani  kisha  asubuhi
tunaenda  kumwaga  uchafu huo  chooni .....” alibainisha mmoja wao.

Akizungumza  na mwandishi  wa habari  hizi  shule ni  hapo  hivi  karibu
Makamu  Mkuu wa shule  hiyo , Agatha Okumu  alikiri  kuongea  na  wanafunzi
wa kike  wanaosoma  shuleni   hapo  ambao  wanaishi katika  nyumba za
kupanga  kijijini  hapo  kuwa  kumekuwepo  na  visa vingi  tu   vya  kubakwa
kwa  wanafunzi hao  lakini  wamekiri kuwa  wamekuwa wakifisha  kusema
kwa  kile
wanachodai  kuwa  wanaona  aibu  kusema .

“Nyumba  walizopanga  hazifai  wao  kuishi  kwani  hazina  usalama
kwani  kutokana
na  milango  ya  vyumba  wanavyoishi  kuwa mibovu  usiku  wanafunzi hao
wanalazimika  kuegesha  vinu  kuzuia  isifunguke lakini  imekuwa  ni  rahisi
sana  kwa ‘wabakaji ‘  kusukuma  tu  milango  hiyo  na kuingia  ndani  kisha
kuwaingilia  na kutokomea  kusikojulikana “ alibainisha .

Aliongeza kuwa   visa  vya kubakwa  wanafunzi  hao  wa kike   ni  vingi
lakini  ni  vitatu tu  vilivyoripotiwa  hadi  sasa  ambapo  kisa  cha  kwanza
kiliripotiwa  baada ya wanafunzi  watatu  kubwakwa  na mtuhumiwa  alisakwa
na kumatwa  na kufikishwa katika  vyombo  vya dola .

Kwa mujibu  wa Makamu  huyo wa Mkuu wa Shule  hiyo , Okumu  alitaja visa
vingine  ni  pamoja  na  mwanafunzi  wa kidato  cha nne  shuleni  hapo
alijiua  kwa kunywa sumju  ya panya  baada  ya  kubakwa  na  mwenzake na
mtu  asiyefahamika  baada ya  mtu  huyo  kuwavamia chumbani mwao  walimokuwa
wakiishi  watatu  nakuwatishia  kuwaua iwapo  wangepiga  kelele .

“Haya  juzi   tu  wanafunzi  sita  waliokuwa wakiishi  chumba kimoja
wamenusurika  kubakwa  na  watu  wawili  waliowavamia  usiku  wakiwa
wamelala  chumbani mwao ........ lakini  walishindwa  kuwafanyia   vitendo  vya
udhalilishaji  baada ya  kuwakuta  kuwa ni wengi  na  walianza kupiga mayowe
ndipo walipowapora  kiasi cha Sh 1,100-  walizokuwa nazo  kisha wakawapiga
kwa marungu  na kutokomea  kusikojulikana “  alibainisha .

Hata  hiyo   baadhi ya wanafunzi  hao  na Mkuu  wa Shule hiyo  Nicholas
Thomas  wamewatupia lawama wakazi  hususani majirani  wanaoishi karibu
 na  nyumba
walizopanga  wanafunzi  hao   kwa   kutowapatia  msaada wowote  licha
ya  waokupiga
mayowe  ya  kuomba  msaada .

“Kukicha  ndipo  wanapokuja  na kutupa pole  huku wakidai  kuwa licha  ya
kutusikia tukipiga  mayowe  ya kuomba msaada  wanashindwa  kutoka  nje  kwa
hofu ya  kushambuliwa  na watu hao wasiojulikana “  alisema  mmoja  wa
wanafunzi hao  kwa masikitiko .

Kwa mujibu wa Mkuu wa Shule , Thomas  wazazi wanatakiwa kuchangia  gharama
za  watoto  wao  kuishi katika mabweni  shuleni  hapo  ambapo  kwa mtoto  mmoja
kwa muhula  mzazi anatakiwa  kuchangia  magunia  mawili  ya mahindi, debe
moja la  maharagwe  na Sh 40,000- ikiwa  ni  ujira  wa mpishi .

Mwisho



0 comments:

Post a Comment